PhD. ya Katibu Mkuu wa Chadema Wilbroad Slaa, ni sahihi?

Jamani,
Msipoteze muda.
Hapa MISSION kubwa ni kuvuruga mjadala wa Posho ZA wABUNGE na Mgomo wa Madaktari!
Wengine hawa ni makuwadi wa Rwakatare, wamekuja kupotezea ile thread inayomcheza unyago!
So dont loose direction brodas and Sistos, pigeni pale panapouma!

Wewe ni nani unataka kupangia watu mada za kuchangia kama wewe upendi nenda jukwaa la siasa kuna thread nyingi.
 
OOOH
ipo njia nyingine kama hii ya kutafuta air time kutumia mtumbwi
406441_344190875602332_100000342668655_1188426_1329537665_n.jpg

hivI HUYU SI NAPE MNAUYE?
 
Rizt maswali kuhusu PHD ya Slaa yamejibiwa kwa kina sana. Ni vema ukaelewa mfumo wa elimu ndani ya kanisa katoliki. Hata hivyo naomba niweke majibu (kwa msaada wa mwanabidii mmoja) yanayoeleza walau kwa kifupi elimu elimu ya Dr Slaa ndani ya mfumo huo wa kanisa katoliki.

PhD ya Slaa siyo ya heshma, ni PHD kwa kupitia research na kama unajua lugha za wenzetu utagundua kuwa alifanya vizuri sana.

Dr Slaa alisoma Kipalapala, hapa mwanafunzi anasoma form 5 & 6 pamoja na masomo ya Theology na baada ya hapo huunganisha na degrii ya theology.

"Kipalapla kama ilivyo Institutions zote za Kanisa Katoliki (kwa level ya Philosophy na Theology) iko affiliated na vyuo vikuu mbalimbali duniani.

Mfano, wanaosoma Zomba Theological College Malawi (Theology) na Kachebere Philosophical College (Philosophy) mpakani mwa Malawi na Zambia wanafuata marking scheme ya Chancellor College - University of Malawi. Kuna chuo kingine kiko Balaka Consorsium Philosophical College nadhani kiko affiliated na St Urban University, Rome.

Missionary Institute London (MIL) iko affiliated kwa Middlesex University (chuo cha serikali cha Uingereza) na Luvein University (Belgium). Wanaofuata mfumo wa Middlesex University kupata BA wanasoma miaka 3 na passmark yao ni 40%. Wanaofuata mfumo wa Luvein University kupata BA wanasoma miaka 4 na passmark yao ni 60%. Muhula unaanza Oktoba na kwisha Juni (miezi 8).

Mfumo wa kutoa final mark ni 1) class presentation na participation 2) essay writing 3) oral examination 4) defence of dissertation mbele ya internal & external examiners. Pia mtu anayepata first class, papers zake lazima ziwe marked na internal na external examiners na ajadiliwe kama anastahili first class degree na siyo tu kupata kwenye karatasi. Pia anayeshindwa, paper zake zinasahishiswa na examiners tofauti ili kuonesha kashindwa kweli au kama amepunjwa marks.

Kwa Tanzania, kwa sasa vyuo vyote kwa level ya Philosophy na Theology viko affiliated na St Urban University, Rome. Zamani, falsafa ilikuwa miaka 2 (sasa ni 3) na teolojia ilikuwa miaka 3 (sasa 4).
Mtu akimaliza (Tanzania) alikuwa anapata certificate siyo kwa sababu masomo yalikuwa level ya chini ila kwa sababu maaskofu walikuwa hawajaridhia wahitimu wao kupata digrii licha ya kuwa walikuwa wanaombwa wanafunzi wapewe magamba kama ilivyokuwa kwenye vyuo vingine. Ilichukua muda kidogo.

Lakini kama mtu aliendelea na masomo ya juu walithamanisha masomo yale kwa chuo ambacho mtu anaenda kusoma maana content ya syllabus ya masomo ya falsafa na teolojia ni (universal) kwa vyuo vyote vya Kanisa Katoliki duniani tofauti ni kwa kila nchi wanaongeza mambo yanayohusu cultural understanding ya nchi husika including its legal system.

Uganda mtu akimaliza Jinja Philosophical College (Philosophy) anapata BA katika Philosophy. Akiendelea na Theology chuo kingine, anapata BA katika Theology na kuna vyuo vingine akimaliza Theology anapata MA. Inategemea chuo kina mfumo gani na kinafundisha nini - maana kuna baadhi ya masomo kama mtu hakuyafanya wakati wa philosophy atayafanya wakati wa theology.

Kwa baadhi ya vyuo, mtu mwenye BA ya Philosphy na BA ya Theology, akiendea na masomo ya juu 'specialisation', anaenda moja kwa moja kusoma PhD kulingana na vigezo walivyoweka (mfano, vyuo ambavyo vinafundisha Philosophy na Theology kwa pamoja).
Kwa baadhi ya vyuo masomo haya yanatenganishwa - yaani, mwanafunzi anaamua ku'specialise' kwenye pure philosophy au pure theology. Na katika masomo yote mwanafunzi anafundishwa the secular view na religious view.

Maana ni hasa kumwezesha mwanafunzi kupata "solid and consistent knowledge of man, the world and God... The students should rely on that philosophical patrimony which is forever valid, but should also take account of modern philosophical studies, especially those which have greater influence in their own country, as well as recent progress in the sciences. Thus, by correctly understanding the modern mind, students will be prepared to enter into dialogue with their contemporaries." ( Vatican II, Training of Priests, Paragrapah No 15).

Kuna vyuo kama alikosoma Dr Slaa lecturers wote ni wa level ya profesa na kwenda kusoma huko mpaka uwe 'exceptional student' nadhani kama sikosei wanachukua wale tu wenye 'first class'.

Pale anaposoma "Canon Law" au "Catholic Education" usidhani padre anasoma tu biblia au mafundisho ya Kanisa. Mfano, Dr Slaa amespecialise katika Canon Law ambayo ndiyo mother of secular law na kusoma Canon Law ni lazima kuanza na how law developed na mpaka kuja kugawanyika into secular na religious laws.

Advantage ya Dr Slaa si tu kwamba ana'knoweldge' ya Canon Law lakini pia nini kwa inaitwa secular law na kwa nini - tofauti na similarities. Mfano, definitions of what is an irregurality, malice aforethought, the difference between legality and validity of an act, what is a valid marriage and a legal marriage, etc.

All Catholic Universities undertake secular studies mfano ni Catholic University of East Africa (CUEA), Kenya, ambako hata Waislamu wanasoma huko, St Augustine, Mwanza, Luvein University etc. kwa hiyo mtu akihitimu kwenye vyuo hivyo, huwa haangaliwi kuwa amesoma elimu ya dini bali kwamba ni mtaalamu katika taaluma fulani aliyoisomea.

Tofauti kwa mapadre ni kwamba mfumo wao wa mafunzo unachukua muda mrefu na wanajifunza mambo mengi - maana hadi kufikia upadre ni mpaka uwe walau umesoma miaka 10 baada ya Form VI". (mwisho wa kunukuu)

lol! mkuu basi kanisa katoliki ni balaaa.
ahsante kwa kutudadavulia kwa kina. ninamashaka sijui kama huyo ritz kakuelewa.
 
Achana nae huyo........anatafuta airtime kwa lazima, akili yenyewe ya kuunga kwa manati, tabu tupu!!!

Kuuliza PhD ya Slaa, ndio natafuta airtime? Chadema-kata bana.

Hilo ndio jibu la PhD ya Slaa?
 
Kuuliza PhD ya Slaa, ndio natafuta airtime? Chadema-kata bana.

Hilo ndio jibu la PhD ya Slaa?

Achana na magwanda ukiwashika pabaya either watapiga campaign thread ifungwe au watakutafutia ban

Sent from my HTC Incredible S using Tapatalk
 
Dokta wa Kanoni.

Kanoni = Kanuni. Ni neno la kiarabu lililochakachuliwa. Na hizo ni kanuni za Kanisa Katoliki ambazo Padre Slaa zilimshinda na akaamuwa asizifate kwa hiyo si vyema kumuita Dokta wa sheria ambazo kazikiuka na kazikana.
 
Wanabodi.

Ili kupata PhD (Doctor of Philosophy) lazima huwe na BA (Bachelor of Arts) na MA (Master of Arts).

Nimepitia CV ya Katibu Mkuu wa Chadema Wilbroad Slaa, nimeona kapata PhD yake mwaka 1977 St. Urban University Rome Italy.

Kwenye CV yake hukuna sehemu yoyote kuwa ana BA ama MA.

Kuna njia nyingine ya kupata PhD bila kuwa na MA na BA?

Kwanza, Mtoto gani wa gerezani usiejuwa kuwa hakuna "huwe", kuna "uwe"...!!!

Pili, unaposema lazima mtu awe na Masters of Arts na Bachelor of Arts, Je na wale wenye Ph.D katika sayansi ama katika uhandisi nao utahoji Ph.D zao kwakuwa hawana MA na BA?

Jaribu kuwa makini unapozungumzia taaluma, hapo hakuna siasa za maji taka, ni facts tu.
 
Dada FF, tangu nisome ile thread yako kuhusu kujenga hoja na namna ya kutofautina....kila nikiona post yako naikumbuka ile thread yako!
 
Dokta wa Kanoni.

Kanoni = Kanuni. Ni neno la kiarabu lililochakachuliwa. Na hizo ni kanuni za Kanisa Katoliki ambazo Padre Slaa zilimshinda na akaamuwa asizifate kwa hiyo si vyema kumuita Dokta wa sheria ambazo kazikiuka na kazikana.

@FaizaFoxy, kwa uelewa wangu Canon ni neno la kilatini. Na canon law imetangulia 'secular' law. Ukielwa vizuri canon utaona a point of departure kwenda kwenye secular law. I can see kwanini watu wanahoji, ni kwa sababu ya kutotelewa mifumo ya elimu katika sehemu tofauti. Ujerumani hawana kitu kinaitwa Degree (i.e BA, Bcs etc) wanatumia neno Diploma ikimaanisha Degree. Hivyo kama mtu amekariri BA lazima atapa tabu akiona Diploma. Ni wapi uliona Diploma inasomewa kwa miaka 3 au 4?

Kwa kifupi kama hujui physics itakuwa vigumu sana kuelewa pale mtu atapoanza kuongea kuhusu Newton law!
 
Kwanza, Mtoto gani wa gerezani usiejuwa kuwa hakuna "huwe", kuna "uwe"...!!!

Pili, unaposema lazima mtu awe na Masters of Arts na Bachelor of Arts, Je na wale wenye Ph.D katika sayansi ama katika uhandisi nao utahoji Ph.D zao kwakuwa hawana MA na BA?

Jaribu kuwa makini unapozungumzia taaluma, hapo hakuna siasa za maji taka, ni facts tu.

Kwa hiyo PhD ya Slaa ni ya Kanisa tu?
 
NDUGU YANGU RITZ;
MFUMO WA ELIMU INATOFAUTIANA KUTOKA NCHI MOJA KWENDA NCHI NYINGINE, HIVYO HUTEGEMEA NCHI HUSIKA NI MFUMO UPI WANAOUFATA. HIVYO, YAWEZEKANA KWAKO IKAWA VIGUMU KUELEWA KWASABABU YA UELEWA WAKO NI KWAMBA ILI UFANYE PhD ni lazima uwe na BA na MA. Sijui wale wengine wenye B.Sc. na MBA/MSc, n.k wao tunaweka wapi. Ndiyo, kwa mfumo wa Elimu yetu ni kweli kwamba ni lazima uwe na Bachelor na Master, ndipo uweze kuwa na uwezo wa kufanya PhD, halafu Professor; lkn si kwa nchi zote mfumo unakuwa ni huo. Kuna nchi zingine kama USA in most cases hawaitambui hiyo masters yako hasa za nchi zetu na ndiyo maana wengi waliokwenda kufanya PhD USA huanzia na Master Degree ndipo hujiunga kwenye PhD Programme. Ndiyo maana wengi USA hutumia hadi miaka 5 kufanya PhD zao USA.

Kuna nchi kama Ujerumani; kuwa Professor si lazima uwe na PhD. Unaweza kuwa Professor lkn PhD hauna, na hii ni kwasababu ya mfumo wao wa elimu. Na katika nchi kama ya Ujerumani, admission requirements kwenye PhD zinatofautiana kutoka Chuo kimoja kwenda chuo kingine kwa utaratibu wa mfumo wao wa elimu. Hivyo, kuwa admission na chuo husika katika programme za masters au PhD ni jukumu la chuo husika kuona kama unacomply na requirements zao.

Ndiyo maana inawezekana mfumo wa elimu aliyosoma Dr. Slaa hauoni BA na MA lkn alifanya PhD yake. Na watu wa Dunia kwa kutambua kwamba kuna mifumo tofauti ya elimu kati ya nchi na nchi, ndiyo maana kukawa utaratibu wa kuangalia mifumo ya Elimu katika nchi mbalimbali ili kuona kama Chuo unachosoma kinakidhi vigezo. Kwahiyo, naomba ukae ukilijua hili kwamba tuna mifumo tofauti ya Elimu na vyote hutegemeana na nchi husika.

Kwako FF;
Jaribu kusoma na kuangalia Mapadri wa Kikatolliki wanasoma nini? Ungejua kwamba mfumo wa Kanisa lao pia unacover hata maeneo mengine ambayo hayahusiani na mambo ya Kanisa. Je unajua contents za Philosophy? Jaribu kuwa muungwana hasa kwenye mjadala ambao unahitaji jamii waelewe na si kuanza mashambulizi tu kwasababu ya malipo unayyolipwa.
 
Inshort mzee slaa elimu yake ni kuongoza kanisa ... Nchi yenye waumini wa dini tofauti hawezi lazma atakuwa biased .. hivi kwa nini aliacha kazi ya kutumikia kondoo ..? Ilikuwa haina dili ama..?

Slaa ni male version ya lwakatare ..

Nawe umeanza kutembea kinyumenyume?

Udhanie ndiye kumbe siye!

Kilaza wewe!
 
Kwani kuna Phd za aina ngapi na ya Dk Slaa ni kwa ajili ya Kanisa tu au hanaweza kwenda kufanyia kazi sehemu yoyote hivyo PhD yake?
 
@FaizaFoxy, kwa uelewa wangu Canon ni neno la kilatini. Na canon law imetangulia 'secular' law. Ukielwa vizuri canon utaona a point of departure kwenda kwenye secular law. I can see kwanini watu wanahoji, ni kwa sababu ya kutotelewa mifumo ya elimu katika sehemu tofauti. Ujerumani hawana kitu kinaitwa Degree (i.e BA, Bcs etc) wanatumia neno Diploma ikimaanisha Degree. Hivyo kama mtu amekariri BA lazima atapa tabu akiona Diploma. Ni wapi uliona Diploma inasomewa kwa miaka 3 au 4?

Kwa kifupi kama hujui physics itakuwa vigumu sana kuelewa pale mtu atapoanza kuongea kuhusu Newton law!

[h=2][/h] Greek kanon / κανών, Arabic Qanon / قانون, Hebrew kaneh / קנה, "straight"; a rule, code, standard, or measure; the root meaning in all these languages, including Latin, is "reed."
 
Wanabodi.

Ili kupata PhD (Doctor of Philosophy) lazima huwe na BA (Bachelor of Arts) na MA (Master of Arts).

Nimepitia CV ya Katibu Mkuu wa Chadema Wilbroad Slaa, nimeona kapata PhD yake mwaka 1977 St. Urban University Rome Italy.

Kwenye CV yake hukuna sehemu yoyote kuwa ana BA ama MA.

Kuna njia nyingine ya kupata PhD bila kuwa na MA na BA?

WanaJF,
Sidhani kama kuna sababu ya kujibizana. Hoja imejibiwa kwa kina. Wahusika wangekuwa na nia njema wangeandikia vyuo husika na kuomba Prospectus ya vyuo hivyo. Nashauri msihangaike nao na kupoteza muda muhimu kwa ajili ya ajenda za Taifa letu.. Wanayoyasema yaliwaponza Karatu 1995 wakiamini Dr Slaa hajui jukwaa. Hawakujua jambo dogo tu kuwa "Oratory" ni somo katika mfumo wa elimu wa Kanisa Katoliki. Tuliwatandika na tutaendelea kuwatandika. Bado hatujawaambia kuhusu Epistemology, Cosmology, Logic, Philosophy na branches zake zote.. Kama ritz na wenzake inawaburudisha waachieni tu waandike wapendavyo.
 
A stomach-blow to the miserable ill-hearted perpetrators!
Shame on damn them.
Thanx Dr.Slaa
 
Back
Top Bottom