Danken Mbombo
JF-Expert Member
- May 30, 2015
- 651
- 339
Walikuwepo wenye PhD ma-wizarani hadi Ikulu , lakini pia TRA walikuwepo waliobobea masuala ya kodi (Taxation). Moja ya mbinu wanayofundishwa katika kukusanya kodi ni kuwawekea walipa kodi mazingira rafiki yanayovutia kulipa kodi. Sina hakika kama JPM amesomea masuala ya kodi, lakini uamuzi wake wa kutoa bure mashine za EFD kwa wafanyabiashara ulikuwa na maana kubwa sana…..yaani ni kama JPM ana PhD ya Taxation …. Ufike wakati hawa wanajiona wasomi waisaidie serikali kwa taaluma zao na siyo kuwa mizigo tu kwa kudai safari, mikopo ya magari, warsha, makongamano na semina endelevu/elekezi zisizokuwa na tija yoyote.