PhD Queries: Hivi ni lazima uchukue miaka mingi kupata PhD au ni mpangilio wa vyuo vyetu uwachelewesha wanaosaka PhD?

Kabulala

JF-Expert Member
Oct 13, 2019
695
935
Je ni kweli, lazima usote darasani miaka 2 - 5 kutafuta PhD, au inategemea na program ya yule anayekufunza?

Natambua full time students uchukua maximum 2 years na part - timers ni 5 years max.

Je, muda wa kukaa darasani ndio unadetermine uhalali wa PhD yako au ni programs na brilliance ya both mwalimu na mwanafunzi?

Na je, sio kweli kwamba soko la ajira ndio linasema institutions zipi zinawapika wahitimu vyema kutokana na programs zao na umahiri wa wahitimu?

Lastly who cares kama individual anapata degree kwa miezi sita na kuiweka kabatini kwake?

Nadhani wale wanaotegemea ajira za vyeti mtakua na insights kubwa sana kwenye hili.

Karibuni.
 
PhD is a doctoral degree with an academic focus. A PhD course is usually of three years duration and candidates need to complete the course within a maximum time span of five to six years. However, the course duration may vary from one institute to the other..
Sijui nimepatia ?
Wengine tuliishia darasa la saba.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
PHD 2 years? Where.
 
Lengo lako nini? Maana naona kama una zunguka around the bush.

Kimsingi kikubwa kwenye PhD ni lengo. Lengo lako likitimia hata ndani ya nusu saa utapata PhD.

PhD haina sylubus, haina mtaala wa haina material. PhD hufanywa na mtu ambaye anaona kuna tatizo fulani katika eneo fulani na analifanyia utafiti ili alitatue au kuboresha. Mara nyingi PhD hufanywa ili kuboresha knowledge wa eneo fulani.

Ili PhD iwe PhD ni lazima ichangie knowledge kwenye eneo husika. Hii ndo tofauti ya utafiti wa taaisisi kama Twaweza na utafiti wa PhD
 
Wewe hujaishia darasa la saba....PhD inategemea mambo matatu makubwa: (1) Aina ya chuo ...vyuo vingi vya nje na hasa vya ulaya vina fixed time ya kumaliza..masters plus PhD up to 4 years - one year masters and 2-3 years PhD...Kule ulaya hakuna blah blah...mwanafunzi unalazimika kusoma na kumaliza on time...(2) Discipline binafsi ya mwanafunzi na hasa kwa vyuo vya kwetu.....unakuta mwanafunzi hana discipline kabisa ya kujisomea yaani hata kuandika proposal tu inamchukua mwaka au zaidi...mwingine anasoma na kufanya kazi kwa hiyo muda unakuwa mchache...pengine ni uvivu tu....kukusanya data eti miaka hata miwili...kuandika first draft mpaka miaka minne...kwa hiyo utaona ni lazima uchukue miaka hata nane ---inahitaji self discipline...wanafunzi wengine wabishi kwa supervisors wao katika kufanya marekebisho fulani fulani (3) Discipline ya supervisors ..wako wengine ambao hawako serious kabisa...wana mikwara ya hapa na pale,,,wana miradi yao na hawataki usumbufu...Yaani profesa kukusomea draft yako tu anachukua miezi nane ...
 
Nje ya mada.

Kuna mtoto mwenye miaka 9 wa kibelgiji anasoma degree Netherlands na anamaliza mwezi wa huu...

Anasema akimaliza anaunganisha PhD....anaitwa Simons. Very interesting.

Tena anasoma Electrical..
 
Lengo lako nini? Maana naona kama una zunguka around the bush.

Kimsingi kikubwa kwenye PhD ni lengo. Lengo lako likitimia hata ndani ya nusu saa utapata PhD.

PhD haina sylubus, haina mtaala wa haina material. PhD hufanywa na mtu ambaye anaona kuna tatizo fulani katika eneo fulani na analifanyia utafiti ili alitatue au kuboresha. Mara nyingi PhD hufanywa ili kuboresha knowledge wa eneo fulani.

Ili PhD iwe PhD ni lazima ichangie knowledge kwenye eneo husika. Hii ndo tofauti ya utafiti wa taaisisi kama Twaweza na utafiti wa PhD
Nusu saa? Mind humu kuna academicians hivyo kuwa macho!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
2_4 yrs ni wapi hapo Masters na PhD, kuna mtu unalenga kumtetea kitaje
Wewe hujaishia darasa la saba....PhD inategemea mambo matatu makubwa: (1) Aina ya chuo ...vyuo vingi vya nje na hasa vya ulaya vina fixed time ya kumaliza..masters plus PhD up to 4 years - one year masters and 2-3 years PhD...Kule ulaya hakuna blah blah...mwanafunzi unazimika kusoma na kumaliza on time...(2) Discipline binafsi ya mwanafunzi na hasa kwa vyuo vya kwetu.....unakuta mwanafunzi hana discipline kabisa ya kujisomea yaani hata kuandika proposal tu inamchukua mwaka au zaidi...mwingine anasoma na kufanya kazi kwa hiyo muda unakuwa mchache...pengine ni uvivu tu....kukusanya data eti miaka hata miwili...kuandika first draft mpaka miaka minne...kwa hiyo utaona ni lazima uchukue miaka hata nane ---inahitaji self discipline...wanafunzi wengine wabishi kwa supervisors wao katika kufanya marekebisho fulani fulani (3) Discipline ya supervisors ..wako wengine ambao hawako seriosus kabisa...wana mikwara ya hapa na pale,,,wana miradi yao na hawataki usumbufu...Yaani profesa kukusomea draft yako tu anachukua miezi nane ...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
2_4 yrs ni wapi hapo Masters na PhD, kuna mtu unalenga kumtetea kitaje

Sent using Jamii Forums mobile app

Viko vingi tu nje...kuna mwalimu wangu mmoja alienda kusoma Uingereza ...alienda akiwa na masters ya hapa kwetu lakini kule akalazimika kusoma tena masters na in four years akarejea na PhD yake at a very young age, below 30 nadhani....
 
Je ni kweli, lazima usote darasani miaka 2 - 5 kutafuta PhD, au inategemea na program ya yule anayekufunza?

Natambua full time students uchukua maximum 2 years na part - timers ni 5 years max.

Aah PhD inategemea na chuo. Kuna aina tofauti au njia tofauti za kupata hilo lidude. Wengi tumezoea PhD by research-unaanza kwa kuandika proposal na ikipita unafanya utafiti na kuandika thesis ambayo ndiyo msingi wa tathmini utakayofanyiwa ikiandamana na kutokea mbele ya jopo la wakali na uwaridhishe kama kweli kazi ile ni yako na wewe umebobea kwenye hilo eneo uliofanyia kazi. Hizi kawaida zilikuwa zinachuchukua kati ya miaka 2.5 na 3.
Kule America wao kawaida unafanya course work (darasani) kwa kama mwaka mmoja halafu ndio unafanya utafiti na kumalizia na thesis kama ilivyo hapo juu. Nayo ilikuwa kawaida ya miaka 3.
Kuna nchi na vyuo fulani hasa europe na Japan kuna Phd ambazo wewe unakuwa mtafiti na unapublish matokeo ya utafiti wako peke yako au na watu wengine. Ukiona umefanya kazi ya kutosha unapanga papers zako kama 3 na kuendelea kwenye hiyo field yako na unawakilisha hiyo kazi yako kama thesis by papers ikiwa ni pamoja na synthesis ya eneo lako. Halafu unaingia kwenye mitihani (thesis examination na thesis defence). Hapa utaona ni vigumu kusema itachukua muda gani kwani kiukweli huhesabiwi kuwa mwanafunzi bali unapopeleka maandishi yako unakuwa candidate.
Baada ya kusema hayo siku hizi kuna aina mbili kubwa kwa hapa Tanzania: by research and by course work and research na thesis kwa format ya monograph (kitabu kimoja na sections zake hazijirudii) by papers and manuscripts (papers ziko published and manuscripts zjko tayari kupelejwa kwa journals lakini bado hazijawa published) na pia thesis by manuscripts tu. Na muda wa kawaida una range kutoka 3 hadi 5 years kutokana na chuo na sponsor. Sasa ukikutana na supevisor kibongo bongo au mwanafunzi kibongo bongo unaweza ukala miaka hadi 6-7.
Kuna pia fulltime na part-time studies. Mara nyingi part time huchukua muda wa mara 1.5 hadi 2 ya full time.
Kuna wanasiasa nao hufanya PhD usually by part-time kwani by definition huwezi kuwa kazini kwako kwenye siasa na ukawa mwanafunzi part time. Kwa Africa hizi kawaida huleta utata hasa kama mtu atachukua muda mfupi. Chiluba alifanya MPhil by research na ikawa na gunzo kama kweli alifanya mwenyewe au ni kazi ya wale vijana waliokuwa wasaidizi wake wengi wakiwa wahadhiri kutoka UNZA (University of Zambia). Mama Grace Mugabe ndie nae alileta sintofahamu pale wahadhiri wa idara husika waliposema hawakumbuki kujadili kazi za mwanafunzi huyo. Hapa kwetu nasikia kuna wanajiuliza baba ya kwake kaipataje ndani ya miaka hiyo nasikia 3. Chuo kilichompa ndiyo kinajua, wengie wanashangaa tu. Lakini ni kazi ngumu sana kuiopoa PhD parttime ndani ya muda huo, lakini baba si mchapa kazi?
Namfahamu mtanzania mmoja huko nyuma kabisa 70's alichukua 2.5 years UK akapata PhD.
 
Viko vingi tu nje...kuna mwalimu wangu mmoja alienda kusoma Uingereza ...alienda akiwa na masters ya hapa kwetu lakini kule akalazimika kusoma tena masters na in four years akarejea na PhD yake at a very young age, below 30 nadhani....
Chuo kipi hicho
 
Nje ya mada.

Kuna mtoto mwenye miaka 9 wa kibelgiji anasoma degree Netherlands na anamaliza mwezi wa huu...

Anasema akimaliza anaunganisha PhD....anaitwa Simons. Very interesting.

Tena anasoma Electrical..
Tatizo sio muda tatizo ni je anaijua ohms law? Anaweza kutatua matatizo? Kama jibu ni yes basi yuko on the right track.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nusu saa? Mind humu kuna academicians hivyo kuwa macho!

Sent using Jamii Forums mobile app

Ndiyo. Jumuia ya Ulaya wana utaratibu wa kutoa PhD kwa mtu yoyote aliyefanya utafiti na kuandika machapisho katika majarida yanayotambulika. Machapisho matano akiyakusanya, anaenda kujiandikisha chuo chenye taaluma kama yake, na kumtunuku PhD.

Sherehe za kutunuku PhD Ulaya aghalabu huweza kuchukua nusu saa (Happy Hour afterwards :D ).
 
1. Kumbe ni sherehe...
2. Unajua kutoa machapisho matano siyo kitu chepesi, labda kama ni Nguin! Hard science siyo kirahisi hivyo. Publication to add new knowledge katika field of research, siyo kirahisi hivyo! Hizo publicatons 5 zinaweza kkugharimu hata miaka 5.
3. Unachapisha katika journal za ranking ipi? Impact factor ya ngapi? (JIP)

Journal Citation Reports (JCR) -2017

Impact FactorNumber of JournalsRanking (Top % of Journals)
10+2391.9%
9+2902.4%
8+3562.9%
7+4473.6%
6+6104.9%
5+8717.1%
4+1,39911.4%
3+2,57521%
2+4,84039.4%
1+8,75771.2%
0+12,298100%

Ulale unono!
 
1. Ukiwa umetimiza masharti ya machapisho, hawana longolongo... wanakupatia gamba lako la PhD. Well... award ceremony is in order.

2. And that, kiongozi Retired, is exactly the point.

3. Sikumbuki exact specifics, lakini nakumbuka maelezo ya kwamba anyone -- literally anyone -- aliyefanya publications tano za ukweli kwenye journals zinazotambulika, only has to compile them and then walk to any EU university (who will award him a PhD).

Asante kwa kunitakia usingizi mnono. Nawe pia.
 
Back
Top Bottom