Ph. D za Wabongo na Dr. Edward Gamanya Hosea pamoja na Lugha ya Kiwahili | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ph. D za Wabongo na Dr. Edward Gamanya Hosea pamoja na Lugha ya Kiwahili

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by KakindoMaster, Dec 4, 2007.

 1. K

  KakindoMaster JF-Expert Member

  #1
  Dec 4, 2007
  Joined: Dec 5, 2006
  Messages: 1,349
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 145
  Jamani nimeweza kupata majina na title za waheshimiwa madaktari waliokwaa udaktari chuo kikuu cha Bongo. Kizuri sana ni Lugha ya kiswahili ambayo nimegundua kuwa ni ngumu kuliko kiswahili.

  Pia nimeona title ya Dr. E. G . Hosea kwa kweli kama ameifanya hiyo PhD kwa uhakika nafikiri inaweza kuwa nyenzo muhimu kwake katika kupambana na rushwa. Sina haja ya kuwachosha jadili wenyewe.

  1.Boneventure Bernard Saanane (Ph.D Electrical Engineering):
  Madhumuni Anuwai ya Uboreshaji Mashine za Umeme Zinazozunguka katika kupunguza upotevu nguvu ulioko katika mabati ya chuma ya mashine hizo kwa kutumia mantiki tim tim.

  2.Edward Gamanya Hosea (Ph.D Law): Mapambano dhidi ya Rushwa
  nchini Tanzania: Nguvu ya Ushahidi wa Mazingira

  3. Justinian Anatory (Ph. D Telecommunications Engineering): Uchunguzi Wa Upatikanaji wa masafa Mapana kwa Kutumia Nyaya Za Umeme Katika Kutoa Huduma Za Mawasiliano Katika Nchi Zinazoendelea.

  4. Hannibal Bwire (Ph. D Transportation Engineering): Mahitaji Na Taratibu Za Kuchagua Moduli Inayofaa Zaidi Katika Kupanga Mipango Ya Usafirishaji Katika Nchi Zinazoendelea.

  5. Anthony Donald (Ph. D Geography): Mfumo Wa Maafa Asilia Ya Mazingira Inyohusiana Na Mabadiliko Na Aina Za Usimamizi Wa Vyanzo Vya Maji Katika Maeneo Nusukame Nchini Tanzania: Uchunguzi Kifani Wa Bonde La Mto Mara

  6. Ester Inocent (Ph. D Chemistry): Terpenoidi na Kemikali Nyingine Zinazozuia na Kuua Mbu Kutoka Mimea Iliyochaguliwa ya Tanzania

  7. Israel Bashurwile Katega (Ph. D Geography): Uhamiaji Wa Watu Kutoka Vijijini Kwenda Mijini Na Umasikini Tanzania: Uchunguzi Kifani Katika Wilaya Ya Kondoa.

  8. Johnson Malissa (Ph. D Water Resources Engineering): Utafiti Wa Usalama Wa Mabwawa Kwa Kutumia Mfano Halisi Na Wa Kimahesabu Kwenye Mabwawa Madogo Ya Tanzania: Uchunguzi Kifani Wa Mkoa Wa Arusha.

  9. Muhsini Salim Masoud (Ph. D Business Administration): Athari Za Sifa Za Wadau Na Maadili Ya Mameneja Katika Ushughulikiaji Wa Maslahi Ya Wadau Kwenye Mashirika Yaliyobinafsishwa Na Yale Ambayo Bado Yanamilikiwa Na serikali.

  10. Omary Khalifa Mbura (Ph. D Business Administration): Upatikanaji wa nyenzo zenye taarifa kuhusu masoko: Mifano toka baadhi ya makampuni madogomadogo ya uzalishaji

  11. Prekesedis Marco Ndomba (Ph. D Water Resources Engineering): Moduli ya mmomonyoko wa udongo na kutuama kwa tope ndani ya Bwawa la nyumba ya mungu katika Bonde la mto Pangani

  12. Anna Kokuberwa Nkebukwa (Ph. D. Sociology): Uandaaji na usambazaji wa habari kuhusu kinga dhidi ya ukimwi, vijijini Tanzania: Mtazamo wa kijinsia.

  13. Francois Dominicus Nzabuheraheza (Ph. D Engineering): Ufanisi wa mabwawa ya kuchuja majitaka katika kuchuja na kutibu maji taka mchanganyiko.

  14. Datius Kananura Rweyemamu (Ph. D Sociology): Majadiliano kuhusu taratibu za mahusiano ya kijinsia kwa vijana sehemu za mijini: uchunguzi kifani katika jiji la Dar es Salaam.

  15. Maureen Were (Ph. D Economics): Ajira Na mapato wakati wa soko huria nchini Kenya: uchunguzi kifani sekta ya uzalishaji.

  Nawasilisha.
   
 2. M

  MzalendoHalisi JF-Expert Member

  #2
  Dec 4, 2007
  Joined: Jun 24, 2007
  Messages: 3,869
  Likes Received: 116
  Trophy Points: 160
  1. Du ni jambo zuri- kama UD wanweza kutoa PhD 15 mwaka huu. Sijui trend ya miaka mingine.

  2. Hivi Boneventure Bernard Saanane (Ph.D Electrical Engineering):
  Madhumuni Anuwai ya Uboreshaji Mashine za Umeme Zinazozunguka katika kupunguza upotevu nguvu ulioko katika mabati ya chuma ya mashine hizo kwa kutumia mantiki tim tim.
  .

  Maana ya mantiki tim tim ni nini? Hapo nimenoa!
   
 3. K

  KakindoMaster JF-Expert Member

  #3
  Dec 4, 2007
  Joined: Dec 5, 2006
  Messages: 1,349
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 145
  Mkuu hiyo inaitwa: Fuzzy Logic
   
 4. M

  MzalendoHalisi JF-Expert Member

  #4
  Dec 4, 2007
  Joined: Jun 24, 2007
  Messages: 3,869
  Likes Received: 116
  Trophy Points: 160
  Kakindomaster,
  Shukrani- basi hiyo lugha tu ya Kiswahili iliyotumika ni safi kweli -ila ni changamoto pia!
  Heshima mbele Mkuu!
   
 5. j

  joshua_ok JF-Expert Member

  #5
  Apr 20, 2016
  Joined: Jun 27, 2012
  Messages: 4,581
  Likes Received: 2,690
  Trophy Points: 280
  Hongera wasomi wetu
   
Loading...