PF3 FORM - TUNDU LISSU, CHADEMA/CCM, WANASHERIA na BUNGE BADILISHENI UTARATIBU HARAKA. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

PF3 FORM - TUNDU LISSU, CHADEMA/CCM, WANASHERIA na BUNGE BADILISHENI UTARATIBU HARAKA.

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by Sikonge, Apr 8, 2012.

 1. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #1
  Apr 8, 2012
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,502
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Utaratibu wa kuchukua PF3 FORM kwanza kituo cha POLISI na ndipo upeleke mgonjwa hospital ambaye kila Sekunde inayogonga ni muhimu sana kuokoa maisha yake, imapitwa na wakati.

  Kuna uwezekano mkubwa kuwa Ngosha wetu Kanumba (RIP) angeliweza kupona kama si uzembe fulani wa kucheleweshwa kufika hospital na ndiyo hiyo form PF3 ianze kutafutwa.

  Ombi kwangu kwa ndugu Tundu Lissu ambaye najua akijipanga vizuri kwa hili, anaweza kuliteka Bunge letu na hii sheria ikabadilika.
  Ombi kwa Waziri wa Sheria, waziri wa mambo ya ndani ambao nao kama kweli wameguswa na kifo cha Kanumba, basi watumie muda huu kufikiri utaratibu wa kubadilisha hii sheria ambao imeshapoteza maisha ya wengi na itaendelea kupotea.
  Ombo kwenu Wabunge wote mnaoingia Bungeni leo hii, kukaa na kujadili na hadi mwisho kupitisha utaratibu mpya wa huduma ya kwanza na ikibidi kama haipo sheria basi iwekwe kuwa "ni lazima kutoa msaada kwa majeruhi." Usipotoa msaada hata kama ni kuita jirani au kuita ambulance, basi uhukumiwe.

  Mwisho kwa wadau wote wa Sheria na Watanzania kwa ujumla, tumeshaona kuwa PF3 form inapoteza muda mwingi sana wa majeruhi kufika hospital, muda ufike sasa huu utaratibu ubadilike. Tulipigie kelele hili swala kwa wabunge wetu popote wanapopita.

  Kwa Wabunge waliopo hapa JF kama Homeboy Kigwangallah, Nchemba Mwigulu, Zitto, Mnyika, Mo, na wengine mliojificha kwenye NICKNAME, Waziri Mkuu na Rais ambao nafahamu mnapita humu ndani, tafadhali sana tunaomba huu utaratibu MUUBADILISHE. Huduma ya kwanza iwe namba moja na ndiyo form ya PF3 ije.

   
 2. C

  Celestinepc Member

  #2
  Apr 8, 2012
  Joined: Jul 8, 2011
  Messages: 12
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ni kweli hili suala liangaliwe upya na wanasheria wetu!!
   
 3. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #3
  Apr 8, 2012
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,502
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Hivi unajua kuna wangapi wanaogopa kwenda bila ya hii form? Unajua kuna wangapi wamekataliwa kupokelewa bila ya hii form? Miaka ya 90 niliona pale Ilala wakimgomea jamaa hadi ikabidi ndugu waende kwanza Polisi.

  Inatakiwa sheria iwe wazi na si "wakikuona upo Serious wanakupokea bila PF3." Nani aamue kama upo na hali mbaya upokelewe bila PF3 au una hali nzuri na ulete kwanza PF3?

  Nafikiri ingelitakiwa Wauguzi wenyewe waamue kama ni kesi ya kuita POLISI au laah. Kwa nchi za wenzetu, ukiita AMBULANCE na kusema mtu kaumia, basi POLISI wanakuja pia. Au Ambulance ikija na kukuta mtu kajeruhiwa, basi palepale wanaita na POLISI ila kwa utaratibu, POLISI wanakuwa wa kwanza maana wapo wengi na magari kibao.

  Ikitokea mtu kapata sijui ugonjwa moyo, kazidiwa sijui alikuwa anafanya nini? Basi inakuja ambulance peke yake.
   
 4. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #4
  Apr 8, 2012
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,502
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  By djochuku [​IMG]
  Umegandisha mno mawazo yako. kama mgonjwa ana hali mbaya anapokelewa Hospitali, PF-3 inafuata baadae baada ya taarifa kufika polisi. kwa kukusidia,ukiona mtu yupo serious,wengine wanampleka Hospitali na wengine wanakwenda Polisi.
   
Loading...