Petroli inayopokelewa Tanga, ilishuka bei kwa mwezi Juni

OLS

JF-Expert Member
Oct 12, 2019
419
669
Ukiangalia Mkeka uliotolewa na EWURA umeonesha mafuta yanayoshuka katika bandari ya Tanga yakiwa na bei ya Tsh. 3,137 kabla ya ruzuku ambapo bei hiyo ni ndogo kwa 1% kulinganisha na bei ya mafuta kwa mwezi Mei ambayo ilikuwa 3,161.

Hata hivyo bei ya mafuta yanayopokelewa bandari ya Dar yalipanda kwa 5% kabla ya ruzuku na yale ya mtwara yalipanda kwa Tsh. 3% kabla ya ruzuku. Hii inaonesha mafuta yanayopokelewa Tanga ni bei rahisi zaidi.

Wito wangu ni serikali kuangalia kwa nini Tanga kunakuwa na bei rahisi ikibidi kuhamishia bandari kuu kuwa Tanga, au kuchukulia mafuta sehemu ambayo watu wa Tanga wanayanunua.

Signed

OLS
 
Basi hao watanga wanaweza sambaza nchi nzima ukiondoa arusha na moshi?
Ila kiukweli tanga kama wangepunguza hizo Tshs 300 basi yangekuwa nafuu zaidi.
 
Back
Top Bottom