Petition ya Mabadiliko ya jina la Ziwa Victoria

Nchi tatu zina share hilo ziwa, usitegemee Kenya na uganda kuukubali hilo wazo. Ila mnaweza kuliita vyovyote mpendavyo ila kwenye ramani za google na nyinginezo duniani wataendelea kuliita Victoria kama dunia wanavyoita ziwa nyasa lake Malawi sisi tukiliita ziwa nyasa
Wakikataa ni sawa tu, sisi tuliite kwa jina letu na wao kivyao....kwenye ncha ya kusini mwa Afrika bahari zimeungana na kila moja ina jina lake, Hindi na Atlantiki.
 
Lake NYANJA au NYANZA ndilo jina lake halisi kabla ya wakoloni kutwa madaraka ya kubadirisha jina.
 
Nyanza ni ziwa kwa kisukuma, kwahiyo kuita ziwa nyanza ni sawa na kuita ziwa 'ziwa'....hata hivyo siyo mbaya....kuhusu majirani siyo mbaya kuwashirikisha.
Sasa kwani majina yalitakiwa yatokana Nini Kama sio lugha za asili za wenyeji? Kwani mlima Kilimanjaro, ukiitafsiri kwa lugha ya wenyeji pia inaleta hivyohivyo maneno double
 
Liitwe ziwa NYANZA.

Hapa Wahaya na Watutsi na Wanyakole wazee wa katerelo, kachabari wanakitu inaitwa KUNYANZA tutakuwa tumeelewana. Waziiiiiiii
 
Sasa kwani majina yalitakiwa yatokana Nini Kama sio lugha za asili za wenyeji?

Kwani mlima Kilimanjaro, ukiitafsiri kwa lugha ya wenyeji pia inaleta hivyohivyo
maneno double
Mimi nakubaliana na wewe kwamba majina yanatakiwa kutokana na lugha za asili, Ila yawe ni maneno yenye maana sahihi isiyo na mkanganyiko. Kuhusu Kilimanjaro, hilo ni neno muunganiko(compuond word) Kilima na Njaro(kyaaro) kwahiyo kusema Kilimanjaro/Kilimakyaaro ni sawa maana inaleta maana sahihi, tofauti na kama ingetafsiriwa na kuwa Kilima-kilima.
 
Mukuruta Victoria akukusu vibroni , cheee mkukuru alisu ashinduku akurawe, huyuku iddi amini sukuruza mkurunzinza akusuwe nyerere kisurunga marusu mgerumani sukukumu 1982 kiizukuru madebe msururu mwanza, kiboroko.
 
Hadi kizazi chako cha million mia nane hakitashuhudia hilo.
Usihangaike na mambo yasiyowezekana yatakayokupa sonona
Kama huwezi au huna balls, usimkatishe tamaa mwenzako, sio poa, tabia za kichawi. Pita tu kimya sumtyms
 
Nyanza au Nyanja ni jina lenye maana ya Ziwa ( kiswahili) au Lake ( kiingereza)

So, nyanza inaweza kuwa Nyanza Victoria au Nyanza Tanganyika (Means lake Tanganyika)


Sisi kwetu Bukoba, Ziwa Victoria tunalijua kama Ziwa Rweru

Enyanja ya RWERU


asanteni
 
kwa kuwa wengi ni kizazi cha jana na leo ...huenda hatufahamu historia halisi ya ziwa hilooo... libaki na jina hilo hilooo

Muhusika alisafiri milage/kms za kutosha na alipofanikiwa safari yake 1858 ndipo akatamka Ushindi/Mafanikio/Victory (Ukitaka elewa zaidi uliza marafiki kwa nini walipewa majina waliyo nayo?)

Lake Victoria Tanzania Africa | Lake Victoria Travel

Victory
1. a success or triumph over an enemy in battle or war.
2. an engagement ending in such triumph: American victories in the Pacific were won at great cost.
3. the ultimate and decisive superiority in any battle or contest: The new vaccine effected a victory over poliomyelitis.
4. a success or superior position achieved against any opponent, opposition, difficulty, etc.: a moral victory.
5. (initial capital letter) the ancient Roman goddess Victoria, often represented in statues or on coins as the personification of victory.

*Vita dhidi ya Iddiamini ---TZ ilishinda ==Victory
 
Wewe liite utakavyo hilo ziwa letu sote, hakuna mwenye ziwa zaidi yako, petition ya nini?!

Hiyo petition unataka uipeleke wapi, nani ana hati miliki ya ziwa hilo?!
 
Kama huwezi au huna balls, usimkatishe tamaa mwenzako, sio poa, tabia za kichawi. Pita tu kimya sumtyms
Maana ya hilo neno ni nini na ni la lugha gani?

Uchawi wajua ni nini?
Unajua unafanyaje kazi?
Tabia za kichawi wazijua?

Mtu mwenye ndoto ya kuona muungano wa Tanganyika na Zanzibar siku moja ukivunjika nikimwambia hata kizazi chake cha billion 7 hakitashuhudia hilo ni kumkatisha tamaa au ndio ukweli?
 
Back
Top Bottom