Petition ya Mabadiliko ya jina la Ziwa Victoria

Mtyela Kasanda

JF-Expert Member
Oct 13, 2018
554
818
Nina petition kunadilishwa kwa jina la Ziwa Victoria. Jina la Victoria halijabeba maana wala asili ya Ziwa linalopakana na nchi kuu tatu za Afrika Mashariki.

Kuendelea kukubali Ziwa letu liitwe Victoria ni kukumbatia ukoloni. Mimi napendekeza liitwe Ziwa Mashariki, mwenye pendekezo zuri zaidi anaweza kulijumuisha kwenye petition hii.
 
Tuwe tunauliza kama hatujui kiongozi wangu.
Nairobi hakuna Ziwa Victoria ni Kisumu
Uwe unauliza sio kukurupuka ,lengo la jina linalohakisi Afrika Mashariki na Nairobi ina present Kenya!! Sio kwamba Ziwa kwa Kenya ndio lipo Nairobi.

Halifiki Nairobi, umechemka! Ziwa lipo Kisumu. Kwa ufupi ziwa hili linajulikana kama Ziwa Nyanza kutokana na wenyeji wote wanaolizunguka huliita Nyanza kwa lugha za makabila yao. Ingawa sina uhakika na Wajaluo.

Naelewa sana Mkuu....Sijaandika kwa sababu ya ziwa lipo karibu na sehemu gani bali umaarufu wa eneo ili kurepresent Kenya zaidi ,Kisumu vs nairobi ,Nai ina umaarufu sana.
 
Mleta mada ana hoja nzuri lakini inashangaza kuona baadhi ya watu wanamdhihaki.

Ukweli ni kwamba hilo jina siyo asilia, wazungu walipofika Afrika walidhani mababu zetu hawakuwa na utamaduni uliostaharabika na ndio sababu ya kumagharibisha utamaduni wetu.

Jina Victoria ni la malkia wa zamani wa kiingereza, alishakufa zamani huko....kuendelea kulitumia tena kwa ajili ya nembo muhimu kama hilo ziwa ni kuitukuza mizimu ya wazungu, siyo ajabu ndo sababu ya watu wetu kumezwa na hilo ziwa mara kwa mara.

Ni muda sahihi wa kulibadili jina na kulipa jina asilia lenye kutukuza asili na uzalendo wetu. Naamini Rais JPM mzalendo wa kweli atapokea hili wazo na kulifanyia kazi kama alivyobadili Stieglers gorge na kuita Nyerere Gorge, inaleta maana Sana.
 
Nchi tatu zina share hilo ziwa, usitegemee Kenya na uganda kuukubali hilo wazo. Ila mnaweza kuliita vyovyote mpendavyo ila kwenye ramani za google na nyinginezo duniani wataendelea kuliita Victoria kama dunia wanavyoita ziwa nyasa lake Malawi sisi tukiliita ziwa Nyasa.
 
Back
Top Bottom