Petition: Wito wa vyuo vikuu nchini kumpa Dr Slaa Udaktari wa Heshima

Kutokana na kazi nzuri sana aliyoifanya bungeni kuhusiana na utetezi wa Watanzania juu ya rasilimali zao, kuikalia serikali kooni na kuiwajibisha vyema mbele ya wananchi. kuleta hamasa kubwa na ya kihistoria kwa wananchi ili kufanya mabadiriko nchini katika uchaguzi wa mwaka huu, basi ni dhahiri kwamba juhudi zake hizo zimesaidia sana kuujenga upinzani nchini na hivyo kupanua demokrasia , kwa maana hiyo basi ni dhahiri siasa za nchi hii hazitakuwa kama zilivyokuwa tena.

kutokana na mchango wake huo ninatoa wito vyuo vikuu nchini kutoa udaktari wa heshima kwa mh: Wilbroad Peter Slaa.

Kuna Vyuo Vikuu na Vyoo Vikuu kama vile vinavyochakachua tafiti. Akipewa "Udaktari wa Heshima" na Choo Kikuu haitakuwa na harufu nzuri.
 
Udakitairi wake wa bibilia sasa mmeshauona hauwezi kuongozea nch manmuombea Digrii/DR ya kweli, aendeshule kama wenzake kwanza ndio ataweza kufikiriwa kutunukiwa udakitari

Kwani mavi ya ng'ombe yanaitwaje kwa Kiingereza?
 
Pamoja na maneno yako Rutashubanyuma, Hosea alipewa degree baada ya kuwa ameisomea, kama mawazo yako ni sahihi basi hata Magufuli amepewa tu kwa sababu yeye ni waziri/Mbunge, na kama ni hvyo basi hata vijana waliopo pale hamna kitu, labda tuwashauri waondoke hapo, maana pananuka sasa, tunapojadili tuweni makini wana jamii.
 
By the way PhD ya mezani unaweza kunyanganywa. Muulize Robert Mugabe alinyanganywa

"Mugabe holds several honorary degrees and doctorates from international universities, awarded to him in the 1980s; at least three of these have since been revoked. In June 2007, he became the first international figure ever to be stripped of an honorary degree by a British university, when the University of Edinburgh withdrew the degree awarded to him in 1984. On 12 June 2008, the University of Massachusetts Board of Trustees voted to revoke the law degree awarded to Mugabe in 1986; this is the first time one of its honorary degrees has been revoked. Similarly, on 12 September 2008, Michigan State University revoked an honorary law degree that it awarded Mugabe in 1990"

Source: Robert Mugabe - Wikipedia, the free encyclopedia

Zinatolewa kulinda maslahi na ukitofautiana kidogo nawahisani wa degree hizo cha moto unakiona so msishangae mnaamuka siku moja na kukutana na Mr.JK

Ndiyo, akileta fujo baada ya Tar. 31, tuongee na wakenya ili wamnyang'anye hiyo Doctorate ya mezani :A S 39:
 
Dr slaa hatumpi kura na nataka ujue siyo watanzania wote wanaoikubali chagaism nchi hii,mpe wewe na wale mliodanganyika hakuna haja ya kutushawishi tumesoma tunajua nani anafaa na kwa sababu zipi.

Kipenga cha mwisho ni Octoba 31.
 
Nisingeshauri Dr. Slaa kushushiwa hadhi na shahada za mezani. Hivi fikiria Chuo Kikuu cha Dar-Es-Salaam kilimtunukuu Bw. Hosea mara tu alipoteuliwa kuwa kibosile pale Takukuru kwa kazi ipi aliyotufanyia watanzania?

Shahada hizo zina harufu kali ya ufisadi na isingefaa kwa Dr. Slaa kuchafuliwa na ufisadi huo. Hata mimi leo wakitaka kunipa hizo shahada za heshima nitazikataa kabisa kwani zimepoteza maana kabisa...zinatolewa kwa kujuana tu..........

Dr Hosea kaisomea PHD yake tena UDSM na Marekani...hakupewa/kutunukiwa bila kuhenya jamani.. penye ukweli tuuseme na tusiongezee chumvi.
 
Dr slaa hatumpi kura na nataka ujue siyo watanzania wote wanaoikubali chagaism nchi hii,mpe wewe na wale mliodanganyika hakuna haja ya kutushawishi tumesoma tunajua nani anafaa na kwa sababu zipi.

Is Dr.Slaa a Chaga labda mimi sijui na hata kama angekuwa mchaga kwani hana haki ya kugombea uraisi wa taifa hili ama wachaga sio watanzania. tumeambiwa mafisadi hawatofautiani hata siku 1 katika misingi ya makabila au dini zao. kwa nini sisi wenye shida na maisha duni tunakaa kutafuta kufarakana kwa kutumia misingi ambayo haitusaidii kwa chochote kile.
 
Kutokana na kazi nzuri sana aliyoifanya bungeni kuhusiana na utetezi wa Watanzania juu ya rasilimali zao, kuikalia serikali kooni na kuiwajibisha vyema mbele ya wananchi. kuleta hamasa kubwa na ya kihistoria kwa wananchi ili kufanya mabadiriko nchini katika uchaguzi wa mwaka huu, basi ni dhahiri kwamba juhudi zake hizo zimesaidia sana kuujenga upinzani nchini na hivyo kupanua demokrasia , kwa maana hiyo basi ni dhahiri siasa za nchi hii hazitakuwa kama zilivyokuwa tena.

kutokana na mchango wake huo ninatoa wito vyuo vikuu nchini kutoa udaktari wa heshima kwa mh: Wilbroad Peter Slaa.

PhD aliyonayo inamtosha, tena hiyo ndo ya ukweli. Hizo za kupewa wapewe tu hao vilaza walioogopa umande na sasa wanatafuta ufalme kwa bei yoyote hata kama wananchi hawawataki.
 
Ya nini PHD ya mezani kwa DR slaa?,ambaye ana PHD ya ukweli?hizo Phd za mezani, awaachie vilaza kama kina JK.
 
Dr slaa hatumpi kura na nataka ujue siyo watanzania wote wanaoikubali chagaism nchi hii,mpe wewe na wale mliodanganyika hakuna haja ya kutushawishi tumesoma tunajua nani anafaa na kwa sababu zipi.
Hopeless utterance!
 
PhD ya heshima kwa Dr. SLAA ni kumpa kura zote kwa asilimia 99.99% hiyo ndiyo ya ukweli. Huyu ni mtu wa heshima hastahili kupewa za mezani. Hizo za mezani ni za mazumbukuku tusizishabikie. Yeye anayo ya ukweli na tukimpa kura zetu tarehe 31 basi tumefunga kazi.
 
Back
Top Bottom