Rev. Kishoka
JF-Expert Member
- Mar 7, 2006
- 4,526
- 1,531
Baada ya kupitia kanuni za Bunge letu kama nilivyoambatanisha, mimi kama Mtanzania naomba kutoa tamko na ombi kwa Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwa wawasilishe muswaada wakuondolewa Viongozi hawa wakuu wawili ambao wameshindwa kufanya kazi na kutekeleza wajibu wao kutokana na mujibu wa Sheria na Madaraka waliyopewa.
Mengi tumeyasema hapa ambayo yametokea katika miaka miwili ya uongozi wao na kwa kweli uongozi na ufanisi wao ni mtupu na unashamirisha Uhujumu, Ufisadi, Uzembe na kukosekana kwa Uwajibikaji na maadilikatika Serikali na Bunge.
Zitto pamoja na wabunge wengine pamoja na Watanzania wote wenye kupenda kuleta mabadiliko ya kuhakikisha uwajibikaji, haki, ufanisi na usawa unatumika katika kuleta maendeleo na Kujenga Taifa, naomba kutoa hoja!