Petisheni dhidi ya Diamond Platnamz ili kumzuia kushiriki BET Awards haina mashiko

Hao anaowasaidia wampigie kura. Uzuri ujumbe umefika kuwa siku nyingine asijihusishe na siasa za kiongozi dhalimu, kisha atake kura za wote hata waliokuwa wakinyanyaswa na kiongozi muovu...
Muovu kwako na wenzako wenye mtazamo huo...ambao tunauheshimu.

Ila swala likija kuwa la kimataifa tuwe wamoja maana Diamond anapeperusha bendera ya Tanzania au labda mwenzetu sio mtanzania..hii dhambi ya kunyoosha vidole itaendelea kuwatafuna mnaojiita wapenda haki...kuna usemi unaosema ukinyoosha kidole kumbuka vitatu vinapoint kwako.

Haki zilianza kukiukwa tokea enzi za mababu zetu msiproject pain zenu kwa kijana wetu let’s stay United..vote for Diamond..

Tanzania nakupenda kwa moyo wote..

Hongera Diamond kwa kazi nzuri ya kuitangaza Tanzania 🇹🇿...Mwenyezi Mungu akulindee
 
Muovu kwako na wenzako wenye mtazamo huo...ambao tunauheshimu..

Ila swala likija kuwa la kimataifa tuwe wamoja maana Diamond anapeperusha bendera ya Tanzania au labda mwenzetu sio mtanzania..hii dhambi ya kunyoosha vidole itaendelea kuwatafuna mnaojiita wapenda haki...
Mbona waganda hawakusimama na Idd Amini wakati Tanzania inaivamia? Huyo Diamond anapeperusha bebe ya ccm na sio ya nchi, ndio maana alivyoteuliwa kuingia kwenye hiyo award alienda kuwashukuru ccm.

Mpeni nyie mnaojiona watanzania na Diamond, sisi wengine hatutaki umoja na watu wanaotukuza uovu kisa eti ni watanzania. Tena ingekuwa tunaingia kwenye hiyo award tungemzomea vibaya sana. Hatutaki umoja wa kinafiki fullstop.
 
Kwa kweli inasikitisha sana...watanzania tunapoelekea tutachekwa na dunia...Diamond akipewa tuzo ni heshima kwa nchi yetu..anaiweka nchi yetu kwenye ramani ya dunia..hizi frakasi za siasa zibaki ndani nchini kwetu....
Umenena vyema!
Tumelogwa watanzania!
Hao bet hawana athari yoyote kwa siasa zetu

Mimi naona njaa ndio chanzo cha yote hayo
 
Hao anaowasaidia wampigie kura. Uzuri ujumbe umefika kuwa siku nyingine asijihusishe na siasa za kiongozi dhalimu, kisha atake kura za wote hata waliokuwa wakinyanyaswa na kiongozi muovu...
Kwamba, mshirika wa shetani obviously naye ni shetani tu...!
 
Kwa kweli inasikitisha sana...watanzania tunapoelekea tutachekwa na dunia...Diamond akipewa tuzo ni heshima kwa nchi yetu..anaiweka nchi yetu kwenye ramani ya dunia..hizi frakasi za siasa zibaki ndani nchini kwetu...
HERE BELOW ARE UNDENIABLE FACTS:

1. Ni kweli kila mtu humpenda kiongozi ama msanii fulani kwa namna na kwa jinsi yake. Hakuna anayebisha. What matters, is number...!

2. Ingekuwa vyema sana waliobusu barabara wakati maiti ya Mwendazake inapita wakampigia kura huyu msanii wenu huyu...

3. Sisi ambao tulikataa hata kuisogelea maiti yake, we are against every oppressive actions and those who support it..

4. Kwa taarifa yenu, Petition mpaka sasa unaposoma andiko hili tayari ina saini za watu karibu 21,000 usiku huu. It is the most and highest signed petition up to now...!

5. Ili petition i - qualify kupewa attention na uchunguzi kufanyika ili muhusika aondolewa inahitajika saini za watu 15,000 tu. Sasa tunakwenda hadi 25,000...!

6. Disqualification ya Diamond Platinumz kushiriki 2021 BET AWARD is obvious wala hakuna cha kudhani wala kufikiri mara mbili au tatu..

7. Hii ishu ya Diamond Platinum iwe ni reference point ili kila mtu ajue kuwa, sasa ni wakati wa upande dhalimu kutambua na kuelewa kuwa, NGUVU YA UMMA (People's Power) inapo prevail, basi ina uwezo ya kuangusha mlima Kilimanjaro na kuusawazisha kabisa hata kuwa nchi tambarare...!!!

5. Sisi tunaopinga tabia na mwenendo wa Diamond Platinumz wote tunaitwa "CHADEMA" au "Wapinzani" na wale wanaounga mkono udhalimu na unyanyasaji wao wanajiita CCM au Wazalendo wa nchi ya Tanzania..

SASA IKO HIVI:
å Hii ndiyo FREE and FAIR ground ya ushindani kati ya WATETEZI WA HAKI (CHADEMA, tusio na vyama vya siasa, wanaharakati & normal citizens) na WANAOTETEA UDHALIMU NA UVUNJIVU WA HAKI ZA RAIA/BINADAMU (CCM, Diamond supporters, Sabaya, Makonda and the likes)...

å Huku hakuna PoliCCM, NEC - CCM wala TISS CCM wanaoweza ku - influence upendeleo wa matokeo. Huku ni ubaya ni ubaya, ama kizuri ni kizuri tu...

å Sasa mtashangazwa na matokeo yake na mtatambua kuwa nyie hamna lolote zaidi ya kutetea matumbo yenu kwa njia dhalimu na uuaji...!!
 
Mfano wa pili: Askofu Mkatoliki aliyekula kiapo cha useja anazaa mtoto na muumini wake. Habari zinasambaa kwa waumini. Lakini, jambo hili linavumiliwa na waumini, kwa mujibu wa kanuni ya matokeo pacha, kwani waumini wanaendelea kuhudhuria ibada zinazoongozwa na askofu huyo.

Kwa kitendo hiki waumini wanachagua ibada na kuvumilia uovu wa askofu, wakiwa wanasubiri mamlaka za juu kuchukua hatua stahiki. Nje ya kanuni ya matokeo pacha, waumini wanapaswa kumsusa askofu.

Hebu niambie ni akofu gani wa kanisa katoliki amewahi kuthibitika kuzaa na muumini na hajachukuliwa hatua?

Naona wewe unahitaji mifano zaidi. Hii hapa:

Mfano wa nne: Askofu anaweka utaratibu wa kutoa nadhiri za milele kwa sharti kwamba sista anayetaka kupokea nadhiri lazima kwanza apokee sakramenti ya uroda kutoka kwa Baba Askofu. Masista wakiwa konventi wanajadiliana na kushangaa. Wanakubali kupikea sakramenti hiyo, lakini wanashitaki kwa Balozi wa Papa. Wanaendelea na utii kwa Askofu huku wakisubiri jawabu la Balozi wa Papa. Wanachagua nadhiri na kuvumilia sakramenti ya uroda.

Niendelee?
 
The predicament of democracy is in this: 2+2=7. This is crucification of truth. Do you know the answer often given by national security organs? Stay well
 
Naona wewe unahitaji mifano zaidi. Hii hapa:

Mfano wa nne: Askofu anaweka utaratibu wa kutoa nadhiri za milele kwa sharti kwamba sista anayetaka kupokea nadhiri lazima kwanza apokee sakramenti ya uroda kutoka kwa Baba Askofu. Masista wakiwa konventi wanajadiliana na kushangaa. Wanakubali kupikea sakramenti hiyo, lakini wanashitaki kwa Balozi wa Papa. Wanaendelea na utii kwa Askofu huku wakisubiri jawabu la Balozi wa Papa. Wanachagua nadhiri na kuvumilia sakramenti ya uroda.

Niendelee?
Hii mifano yako ni very very very irrelevant. Tafuta mifano ambayo walau itaendana na mada yako.
 
Sijakuambia sielewi. Nimekuambia mifano yako ipo very irrelevant. Inaonekana una chuki na kanisa katoliki kwa mifano yako mfu.

Adios.

Hiyo ni mifano hai kutoka Dar na Songea ya enzi zile. Mwenye chuki na kanisa ni watendaji. Au unataka niongeze mwingine?
 
Mkuu, hao wasimtakia mema huyo dogo kutoka Tandale ni vile tu wamejaa na wivu na husda za za kichawi juu ya mafanikio ya huyo kijana,uzuri wa Mungu alivyoweka ni kwamba unapomuombea mabaya adui yako,yeye ndio anazidi kumpaisha ili umkufuru akuonyeshe cha mtema kuni
 
View attachment 1812671

Nimesoma petisheni dhidi ya Diamond Platnamz ili kumzuia kushiriki BET Awards lakini haina mashiko.

Naona petisheni inaratibiwa na mwanaharakati anayejitambulisha kwa jina la Liberatus Mwang'ombe, na kunadiwa mitandaoni na kupitia akaunti za twitter za Maria Sarungi, Hilda Newton, kigogo2014, Ansbert Ngurumo kupitia gazeti lake la Mtandaoni la Sauti Kubwa, na wengine kadhaa.

Kuna hoja sita zilizotajwa katika petisheni nazo ni hizi hapa:

  1. Kwamba, Diamond Platnamz hakupaza sauti wala kuonyesha mshikamano na wasanii kama vile Roma Mkatoliki, Nay wa Mitego na Idris Sultan, waliopinga utawala dhalimu wa hayati Magufuli.
  2. Kwamba, Diamond Platnamz alitumia bishara yake ya sanaa ya muziki kutakatisha ukatili wa hayati Magufuli na washirika wake kwa kuwajengea taswira chanya mbele ya jamii. Anatajwa kutunga wimbo wa "Magufuli Baba Lao," kupanda katika majukwaa ya kampeni za CCM mwaka 2015 na 2020, na kumfanya Paul Makonda Mlezi wa biashara zake, wakati Marekani tayari imetoa taarifa ya kusema kuwa Makonda anahusika katika kusababisha utendwaji wa uhalifu dhidi ya ubinadamu.
  3. Kwamba, Tuzo za luninga ya BET zimekuwa na heshima mbele ya Waafrika wengi kwa sababu ya kutambua kazi za wasanii ambao wanazo sifa za kuinuliwa kwa sababu wao ni mfano wa kuigwa katika jamii, wakati Diamond Platnamz hana sifa hiyo, kwani yeye ni mbinafsi, mchoyo, bendera fuata upepo, na mtu mwenye kufungamana na mifumo dhalimu.
  4. Kwamba, Diamond Platnamz alitumia bishara yake ya sanaa ya muziki kutakatisha ukatili wa Paul Makonda aliyetajwa na Marekani kuwa anahusika na makosa ya uhalifu dhidi ya ubinadamu kwa kumjengea taswira chanya mbele ya jamii.
  5. Kwamba, Diamond Platnamz alitumia bishara yake ya sanaa ya muziki kutakatisha ukatili wa Paul Makonda aliyetajwa na Marekani kuwa anahusika na makosa ya uvunjaji wa haki za watu wenye jinsi tata (GLBITs) kwa kumjengea taswira chanya mbele ya jamii
  6. Kwamba ni mwanachama wa CCM chama kilichokuwa kinaongozwa na hayati Magufuli anayelaumiwa kwa udikteta

Ninazo sababu kadhaa za kupinga petisheni hii yenye msingi wake katika falsafa ya jino kwa jino. Nitaeleza kwa kifupi.

Mosi, kitendo cha mfanyabiashara kutafuta faida kwa kuuza huduma kwa mteja mwenye tabia tofauti na yake sio kosa kimaadili wala kisheria.

Pili, kuchagua kukaa kimya juu ya tabia mbaya ya mteja wako ili kukinda uteja kati yenu sio kosa kimaadili wala kisheria.

Tatu, kuchagua itikadi na sera za chama kinachoongozwa na watu wenye tabia mbaya sio kosa kimaadili wala kisheria.

Nne, matamko ya Marekani juu ya uchaguzi na Makonda yanatana makosa ya jumla (statements of offense) bila kutaja mchanganuo wa tuhuma (particulars of offense) na hivyo hayawezi kutumika kama msingi wa maamuzi huru.

Tano, kumshambulia Diamond kwa sababu zilizotajwa hapo juu ni sawa na kubomoa umagufuli kwa mkono wa kushoto na kuujenga kwa mkono wa kulia. Umagufuli unajumuisha tabia kama vile kutengeneza habari feki na kuzisambaza (disinformation), kusambaza in habari feki (misinformation), kusambaza habari binafsi bila ridhaa ya mhusika (malinformation), kujipa mamlaka ya kubadilisha ukweli kuwa uwongo na kinyume chake (constructivism), kuthamini matokeo bila kujali njia za kufikia matokeo hayo (machiavellism), kutumia neno lenye maana zaidi ya moja bila kubainusha maana kuaudiwa kwa makududi (equivocation), kutafsiri maneno ya mtu baki kinyume na maana aliyokusudia yeye (spinning), etc

Sita, Diamond Platnums ni mfanyabiashara anayeuza sanaa ya muziki kwa yeyote bila kujali itikadi ya kisiasa. Sanaa ni huduma inayonunuliwa kama bidhaa baki, kama vile nguo, mabango, vitabu, vipeperushi, fremu za biashara, magari ya abiria, na kadhalika. Walaji wa huduma hizi wanaweza kuwa na mitazamo tofauti na mitazamo ya muuzaji.

Na muuzaji anaweza KUTABIRI kuwa kwa kuwauzia huduma/bidhaa yake ILI APATE FAIDA wao wataweza kutumia bidhaa/huduma hiyo kuendeleza mitazamo yao, ambayo hata hivyo, muuzaji hazikubali, bali ANAZIVUMILIA tu.

Kwenye sayansi ya maadili hali hii inaelezeka vema kwa kutumia kanuni ya matokeo pacha (principle of double effect). Ni sawa na ambavyo, msanifu wa mipango mikakati ya habari, mwenye kuamini katika itikadi ya Chadema, ataajiriwa na chumba cha habari cha UHURU Media kuwafanyia kazi ya malipo.

Kazi atakayofanya itampa UJIRA na KUENDELEZA ITIKADI ASIYOIUNGA MKONO. Hili la pili ni matokeo yanayotabiriwa, na kuvumiliwa, japo hayachaguliwi moja kwa moja.

Na saba, kukataa kutumia kanuni ya matokeo pacha (principle of double effect) katika kisa cha Diamond Platnums, maana yake ni kwamba tusiitumie katika visa vingine pia, vyenye kufanana na kisa hiki. Kwa kuamua kutoitumia tutalazimika kuandika petisheni kwa kila kisa.

Nitatoa mifano michache ya visa vinavyofanana na kisa cha Diamond Platnums, lakini ambavyo havijaandikiwa petisheni.

Mfano wa kwanza: Julai 2020, Msajili wa Vyama, Jaji Mtungi, alitamka kuwa kanuni ya 6.5.2(d) ya Chadema ni batili kwa kuwa inapingana na ibara 5.2.4 ya katiba ya Chadema, toleo la 2019. Lakini Novemba 2020, Kamati Kuu ya Chadema ilitumia kanuni batili ya 6.5.2(d) kuwaadhibu kina Mdee, na hivyo kuvunja ibara 5.2.4 ya katiba ya Chadema.

Sasa hivi wajumbe wa Kamati Kuu wanazunguka nchi nzima kueneza chama, na wanapokelewa na wanachama wa Chadema. Kitendo cha wananchi kuwapokea wajumbe waliovunja Katiba ya chama kinamaanisha matokeo mawili: kuendeleza kazi za chama na kushirikiana na viongozi waliovunja Katiba.

Hili tokeo la pili linavumiliwa, kwa mujibu wa kanuni ya matokeo pacha, kwa kuwa chombo chenye mamlaka juu ya Wajumbe wa Kamati Kuu ni Baraza Kuu na sio wanachama wa ngazi za chini. Nje ya kanuni ya matokeo pacha wanachama wa mikoani wanapaswa kuwasusa wajumbe wa Kamati Kuu.

Mfano wa pili: Askofu Mkatoliki aliyekula kiapo cha useja anazaa mtoto na muumini wake. Habari zinasambaa kwa waumini. Lakini, jambo hili linavumiliwa na waumini, kwa mujibu wa kanuni ya matokeo pacha, kwani waumini wanaendelea kuhudhuria ibada zinazoongozwa na askofu huyo.

Kwa kitendo hiki waumini wanachagua ibada na kuvumilia uovu wa askofu, wakiwa wanasubiri mamlaka za juu kuchukua hatua stahiki. Nje ya kanuni ya matokeo pacha, waumini wanapaswa kumsusa askofu.

Mfano wa tatu: Kuna wafanyabiashara wengi ambao ni wanachadema wanafanya biashara zinazowahudumia vongozi wa CCM waliokuwa maswahiba wa Magufuli. Lakini hawa hawajaandikiwa petisheni.

Kwa hiyo, kama tunakubaliana na hoja kwamba tunapaswa kuepuka tabia ya kujipinga katika maamuzi yetu, basi, hatupaswi kusaini petisheni dhidi ya Diamaond Platnums. Naongelea kanuni ya consistency ambayo ni kiashiria cha kanuni ya ukamilifu, yaani integrity.

Kwa ujumla, umagufuli ni itikadi hatari kwa usalama wa nchi bila kujali kwamba inatekelezwa na wana CCM, wana CHADEMA, watu walio ndani ya nchi, watu walio nje ya nchi, au vinginevyo.

Na propaganda hasi zinazotegemea fallacy of association ni mkakati wa kupakana matope bila uhalali. Ni vivyo hivyo kwa tamathali ya semi iitwayo satire.

Yaani, "the use of humour, irony, exaggeration, or ridicule to expose and criticize people's stupidity or vices, particularly in the context of contemporary politics and other topical issues."
Tatizo kuu na hoja zako zote ni kuwa hazizipi nafasi subjective perceptions/choices au mitazamo/maamuzi binafsi ambayo mara nyingi huwa hayaendani na hoja zenye mantiki haswa kwenye masuala kama ya Muziki/Wanamuziki, michezo kama soka na dini ambayo huwezi kulyajadili kwa kutumia hoja za mantiki. Haya mambo ni beyond the realm of logical evaluation. Hater's will hate, regardless. There's no "metaphysics" behind all this.
 
Naona wewe unahitaji mifano zaidi. Hii hapa:

Mfano wa nne: Askofu anaweka utaratibu wa kutoa nadhiri za milele kwa sharti kwamba sista anayetaka kupokea nadhiri lazima kwanza apokee sakramenti ya uroda kutoka kwa Baba Askofu. Masista wakiwa konventi wanajadiliana na kushangaa. Wanakubali kupikea sakramenti hiyo, lakini wanashitaki kwa Balozi wa Papa. Wanaendelea na utii kwa Askofu huku wakisubiri jawabu la Balozi wa Papa. Wanachagua nadhiri na kuvumilia sakramenti ya uroda.

Niendelee?
Endelea!!!
 
Back
Top Bottom