Peter (RIP) kaondoka kishujaa

Yaani mshkaji kapiga pushups kafariki unasema kaondoka kishujaa... Na huyu mh rais wetu amepiga nyingi tu na ka survive si inabidi useme anaishi kishujaa...
Napiga za ukweli kafa, kapiga za kuibia kaishi... Maisha hayana formula

Jr
 
Ameondoka kishujaa, ametoka kanisan kuimba akaenda IDM kwenye kikao cha viongoz wa kwaya, baada ya kikao wakaenda Kilimahewa kupiga picha za mwaka mpya,,, moja ya picha alipenda apige akiwa anapiga push up,, akapiga ya kwanza, ya pili hadi ya nne akaanguka hapo hapo na kuaga dunia


Push up alizopiga Peter hadi wakati wa mwisho wa maisha Yake... hapo wakati anaamka ndio alirudi chini. anaondokaView attachment 984617

Jr
Mazoez yeyote unapotaka kufanya lazima uuandae mwili kwanza mfano stretching ya viungo nk, nahic ndio kosa la marehemu . .

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tujengeni tabia ya kupima afya zetu hasa sisi wanaume. Tuko wazembe sana na kwenda hospitalini mpaka tuumwe hata kama tuna bima. Utakuta katatizo kadogo kwenye moyo unakaa nako miaka na miaka na siku moja unazimika.

Mwanaume wa kisasa ni lazima ujue presha yako ikoje. Sukari yako imekaaje. Lehemu (cholesterol) kiwango gani, hali ya jumla ya moyo, figo, ini na tezi dume. Yote haya yanahitaji vipimo rahisi tu vya damu, EKG na vinginevyo. Kila mwaka tupime japo mara moja. Ni muhimu sana jamani.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom