Peter Msigwa: Ujio wa Katibu UN, Rais amepoteza fursa kimataifa!

Francis12

JF-Expert Member
Sep 30, 2016
7,533
22,278
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Ujio wa Katibu UN, Rais amepoteza fursa kimataifa!

Nimesikitishwa na kushangazwa sana na hatua ya Mhe Rais, John Magufuli, kutofanya mazungumzo ya ana kwa ana na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN), Antonio Gutteres, aliyepita nchini jana akitokea Ethiopia na Kenya, alikofanya mazungumzo na viongozi wakuu wa nchi hizo.

Hatua ya Rais kumtuma Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Agustino Mahige, kuzungumza na Katibu wa UN huku Rais mwenyewe akiwa yupo nchini, haikuwa sawa kiitifaki wala kimkakati.

Hatua hiyo imezidi kupunguza ushawishi wa Tanzania kwenye jumuiya ya kimataifa kwa kushindwa kuzitumia vizuri fursa za kimataifa zinazojitokeza katika kufanikisha utekelezaji wa sera ya diplomasia ya uchumi na Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs) ifikapo mwaka 2030.

Ujio wa Katibu huyu mpya wa UN aliyeingia madarakani tarehe 1 Januari mwaka huu, ulikuwa ni fursa kubwa na ya kipekee sana kwa Rais, ambaye ndiye Mwanadiplomasia namba moja, kufanya mazungumzo na kupenyeza si tu maslahi na ushauri wa Tanzania kwa UN, bali pia kupenyeza changamoto na maslahi mapana ya jumuiya nzima ya Afrika ya Mashariki ambayo Rais ndiye Mwenyekiti wake. Ni jambo la aibu kwa Rais kuukimbia wajibu wake huu muhimu kwa nchi!

Wakati Rais Kenyata wa Kenya alivunja ratiba zake zote na kuona ulazima wa kufanya mazungumzo na Katibu wa UN; na wakazungumza juu ya kushughulikia matatizo ya njaa, ukame, ugaidi na changamoto za hali mbaya ya usalama hasa kwa nchi jirani za Somalia, Burundi na Sudani; Mwenyekiti Magufuli anayeongoza Jumuiya nzima ya Afrika ya Mashariki, alichagua kwenda 'kujificha' Dodoma! Huu ni ushahidi wa wazi wa Rais kukosa ajenda na kushindwa kuona fursa.

Ikumbukwe kuwa matatizo ya ukame na njaa ambayo Rais Kenyata aliyazungumza na Katibu wa UN, ni sehemu ya matatizo makubwa yanayoisibu Tanzania pia hivi sasa. Matatizo haya pia yams kwenye Malengo ya Maendeleo Endelevu yaliyopitishwa na wakuu wa nchi wanachama wa UN ikiwemo Tanzania. Kwa mujibu wa Malengo hayo, wajibu wa UN, pamoja na mambo mengine, ni kuhamasisha jumuiya ya kimataifa hasa nchi tajiri kuwekeza mikakati na raslimali za kutosha ili kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi (climate change), kusaidia mikakati ya kuboresha kilimo na kukabiliana na njaa hususani kwa nchi zilizo kusini mwa jangwa la Sahara ikiwemo Tanzania. Wakati Wilaya mbalimbali nchini zikiwa kwenye baa la njaa na ukame, inasikitisha kwa Kiongozi Mkuu wa nchi kushindwa kuona fursa na ulazima wa kuyazungumza kwa uzito masuala haya na Kiongozi huyu wa UN!

Wakati serikali ya Rais Magufuli ikidai inapambana na madawa ya kulevya na wakati madawa hayo yakiwa yanaingizwa nchini kutoka nchi mbalimbali duniani; nilitarajia kumuona Mkuu wetu wa nchi akikutana na Katibu wa UN na kujadili suala hili. Alipaswa kuishawishi UN kuchukua hatua madhubuti ya kuzibana na kudhibiti uzalishaji wa madawa ya kulevya kwani kushamiri kwa biashara hiyo kunahatarisha pia amani na maendeleo ya watu hasa vijana duniani kote. Jitihada za kupambana na madawa ya kulevya hapa nchini zitakuwa ni za "kutwanga maji kwenye kinu" kama hazitaishirikisha vizuri jumuiya ya kimataifa. Ni ajabu kuwa Rais hakuiona fursa adhimu ya kukutana na Katibu wa UN ili kutanua vita dhidi ya madawa ya kulevya kwa kuvitafutia msukumo wa kimataifa.

Kwa uzito wa majukumu yake na ushawishi wa nafasi yake kwa kimataifa, Katibu wa UN ni Kiongozi mwenye hadhi na umuhimu mkubwa sana Duniani. Kwa kawaida huyu ndiye msemaji na muwasilishaji mkuu wa maslahi ya nchi wanachama katika mikutano mikuu ya UN na kwenye vikao vya mabaraza yake likiwemo Baraza la Ulinzi na Usalama na Baraza linalohusika na Maendeleo ya Uchumi na Jamii (Economic and Social Council). Mkataba wa Umoja wa Mataifa (UN Charter) pamoja na majukumu mengine, umempa Katibu UN, fursa ya kuwasilisha jambo lolote kwenye vikao hivyo, ambalo kwa mtazamo wake, linaweza kusaidia katika kudumisha amani na usalama` na` ustawi wa nchi wanachama. Kwa namna yoyote ile, Kiongozi mwenye hadhi na umuhimu mkubwa hivi duniani, alipofunga safari kuitembelea Tanzania, hata kama ni kwa mazungumzo ya dakika chache, haikupaswa apokelewe na kuzungumza na Waziri pekee. Hadhi inayolingana na Kiongozi mwenye dhima ya kidunia, ni Rais wa nchi.

Haikuwa sawa hata kidogo kwa Rais kumkwepa Katibu wa UN na kukimbilia Dodoma kwa kisingizio cha majukumu ya chama, ilihali alishajua mapema juu ya ujio wa Kiongozi huyo;. Na kulikuwa uwezekano wa Rais kutoka Dodoma na kufanya mazungumzo mafupi na Kiongozi huyo na kurudi kwenye majukumu yake ya kawaida, lakini ha kufanya hivyo. Kwanini vikao vya CCM viwe muhimu zaidi kwake kuliko maslahi ya Watanzania wote?

Kwa mara nyingine tena, namtaka Mhe Rais kuyapa umuhimu na ulazima wa kutosha masuala ya kimataifa. Tanzania si kisiwa...hata akusanye kodi nyingi kiasi gani, hata atumbue majipu mengin kiasi gani, bado Tanzania haitaweza kupata maendeleo ya haraka kama Rais atapuuza ushirikiano wa kimataifa.

Ninaamini hatua ya Rais Magufuli kutokupata msukumo ndani ya nafsi yake wa kukutana na Katibu wa UN, kunatokana na kutokuwa na ajenda yoyote iliyobayana ya kimataifa anayoisimamia. Ni dhahiri kuwa Ikulu ni kitu gani Tanzania inakitafuta au inakisimamia kwenye Jumuiya ya kimataifa. Wangekuwa na ajenda, Rais asingeiacha fursa hiyo ipite hivi hivi.

Kwa mara nyingine tena, namshauri Mhe Rais awatumie vizuri wataalam na wasomi wa nchi hii ili wamwongoze vizuri zaidi jinsi ya kuongoza nchi. Wamsaidie kuipata ajenda ya Tanzania kimataifa na wamshauri jinsi ya kuzitumia vizuri fursa adhimu za kidiplomasia zinazojitokeza kushawishi na` kusukuma maslahi ya nchi kimataifa. Asione tabu kuutekeleza ushauri wangu. Tanzania ni yetu sote!

Imetolewa leo tarehe 10 March, 2017

Peter Simon Msigwa
Waziri Kivuli wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Kikanda.
 
Imetolewa leo tarehe 11 March, 2017

FB_IMG_1489094801901.jpg

Mwambieni hakupoteza Fursa walishakutana kwenye mkutano wa AU mjini Addis Ababa na wakaongea Mengi.
 
Hii ndio akili ya huyu Msigwa?
 
Back
Top Bottom