Peter Msigwa: Sisi hatuwashawishi Wananchi ili tupate ajira bali tunataka Demokrasia ifanye kazi

Sidhani kama kurushiana maneno huku kunasaidia upinzani, ilipaswa tuwe wamoja kuelekea 2025 ila kama tunagawanyika hivi hyo tume huru tutaidai vp bungeni.

Kama ambavyo ACT hawakuingilia suala la kina Mdee nadhani CHADEMA nao wangepotezea suala la Maalim maana ni chama chao wana uhuru wa kujiamulia.

Lissu kma presidential aspirant hakupaswa kuchukua upande mapema hivi. Angekua neutral tu coz bado ataihitaji Zanzibar uchaguzi wa 2025. Hii misuaguano haisaidii zaidi ya kudhoofisha upinzani tu na kuwapa credit CCM.

Just saying.....
Lisu hajui siasa mkuu, ni mbumbmbu wa siasa!

Hukuona wakti wa kampeni alienda Zanzibar akasema chadema haina maslahi na Zanzibar?

Mwacheni Lisu aendelee na uana harakati.
 
Zito kachukua dola milion 5 wamegawana na maalum seif na baadhi ya viongozi wa juu ACT ndiyo maana Zito kawa na kiburi cha kuwatukana chadema na kujiona mjanja
Unaweza kuweka ushahidi hapa
 
Aliyekuwa mbunge wa Iringa mh Msigwa amewashukia na Seif. Peter Msigwa: "Sisi hatuwashawishi Wananchi ili tupate ajira bali tunataka Demokrasia ifanye kazi, sisi tukitaka ubunge tunapata tu hata kupitia CCM ila Sisi tunataka katiba mpya, tume huru na haki ipatikane.

"Maalim Seif na Zitto waliochofanya ni sawa na Mbwa kurudia matapjshi yake na kilichowafanya wafanye hivyo ni mambo ma4 Uongo, Unafiki, Uoga na kujipendekeza, si wawe tu CCM. -:~ Peter Msigwa Mbunge wa zamani wa jimbo la Iringa kupitia Chadema.View attachment 1649744


Msigwa amesahau mwaka 2015
 
Zito kaokota dola milion 5 toka CCM kaamua kujitoa fahamu zote kawaona wapinzani wengine hawana maana na pia hajali roho za wazanzibar waliokufa na kujeruhiwa wakati wakipigania chama chake
Tamaa ndiyo iliyo mtawala
 
Sidhani kama kurushiana maneno huku kunasaidia upinzani, ilipaswa tuwe wamoja kuelekea 2025 ila kama tunagawanyika hivi hyo tume huru tutaidai vp bungeni.

Kama ambavyo ACT hawakuingilia suala la kina Mdee nadhani CHADEMA nao wangepotezea suala la Maalim maana ni chama chao wana uhuru wa kujiamulia.

Lissu kma presidential aspirant hakupaswa kuchukua upande mapema hivi. Angekua neutral tu coz bado ataihitaji Zanzibar uchaguzi wa 2025. Hii misuaguano haisaidii zaidi ya kudhoofisha upinzani tu na kuwapa credit CCM.

Just saying.....
Lissu alitakiwa kukaa kimya kabisa kama hajasikia chochote. Inaonyesha hana washauri wazuri, ama la hajafunzwa kunyamaza na kupotezea yasiyomuhusu.

Siasa za zanzibar ni mbali tofauti kabisa na siasa za bara. Hajiepushe nazo...
 
Shikamoo Msigwa,maneno yako yamenipa faraja kubwa sana.Ubarikiwe sana baba.
 
Aliyekuwa mbunge wa Iringa mh Msigwa amewashukia na Seif.
Peter Msigwa: "Sisi hatuwashawishi Wananchi ili tupate ajira bali tunataka Demokrasia ifanye kazi, Sisi tukitaka ubunge tunapata tu hata kupitia CCM ila Sisi tunataka katiba mpya, tume huru na haki ipatikane.

"Maalim Seif na Zitto waliochofanya ni sawa na Mbwa kurudia matapjshi yake na kilichowafanya wafanye hivo ni mambo ma4 Uongo, Unafiki, Uoga na kujipendekeza, si wawe tu CCM. -:~ Peter Msigwa Mbunge wa zamani wa jimbo la iringa kupitia Chadema.View attachment 1649744

Kukubaliana kutokubaliana ni jambo la muhimu sana katika demokrasia.

Kama ambavyo mawazo ya mchungaji Msigwa yanavyoheshimiwa si haba kuheshimu ya wengine.

Ukweli mchungu:

1. Seif na ACT kama chama ni watu wawili tofauti.
2. Seif ni Mzanzibari zaidi kuliko ACT.
3. Seif kaipigania, anaipigania na ataendelea kuipigania Zanzibar kwa nguvu zake zote na kwa maisha yake yote.
4. Matatizo yetu Bara si kipaumbele cha Seif. Mtu kwao.
5. Alipo Seif wazanzibari wengi wako hapo. Hii hata kama Seif akiamua kwenda chama kingine chochote.
6. Seif akiamua kukinukisha Zanzibar kinanuka wakati wowote.
7. Seif kajijengea uhalali huo hayupo anayeweza kuutia doa.

Yapo mengi yanayoweza bado kuandika kuhusu Seif au hata ACT.

Ilikuwa busara kujipanga namna ya kufanya shughuli na Seif na hivyo ACT.

Seif si kibaraka. Angekuwa kibaraka angekuwa imejionyesha hivyo muda achilia mbali uchaguzi wa 2015.

mi-CCM inafurahishwa sana na migogoro ndani na hasa ya baina ya vyama.

Umoja ni nguvu utengano ni udhaifu.

Jitihada za kupunguza mivutano isiyokuwa na tija tokea pande zote lilikuwa jambo la tija sana.

Wakati mwingine ni heri sana hata kubakia kimya. Heko bwana Mbowe kwa hili.
 
Back
Top Bottom