yamindinda
JF-Expert Member
- Jul 29, 2011
- 1,581
- 1,318
Mtangazaji; Mnafanya mchakato upi ili kupata wagombea?, yaani mna aina gani ya viongozi ambao mnao? Kama mna viongozi ambao wanaweza wakarubuniwa kwa rushwa na wakapokea hii inaleta twaswira gani ndani ya chama kizima kwamba kuna viongozi wanaoweza kurubunika na kukisaliti chama, tusaidie ndani ya CHADEMA kuna viongozi wa aina gani?
Msigwa: Tuelewe kwanza rushwa ni ushawishi, kutoa na kupokea rushwa yote ni makosa. Rushwa ni kosa la jinai ikiwa imefanywa na watu wa Chadema au CCm au kwa mtu ambaye hana chama. Ila tuangalie mazingira ya hii rushwa yapoje, watu walijaribu kutumia hii rushwa kudanganya umma kwa maslahi yao binafsi.
Kwa kudanganya kwamba watu wanatoa sifa, kuna utendaji wa kazi mzuri ili waonekane wanafanya kazi vizuri kwa kuwanunua watu hicho nicho kikubwa tunachokifanya na kujaribu kukomesha. Kwa hiyo sio swala la chadema ni kosa la jinai
Mtangazaji: Sasa kwa nini washawishiwe madiwani wa CHADEMA tu na sio wa vyama vingine, kuna Madiwani wa CUF na vyama vingine kwanini hao? Ndio maana nikauliza mna viongozi wa namna gani?
Msigwa: Tukizungumza hivyo lazima tuangalie katika muktadha wa siasa za kitanzania, sisi tupo katika upande wa upinzani, tunajaribu kuipinga serikali tunajaribu kuwachochea wananchi waione serikali haifai. Na ndio kazi ya kiongozi wa siasa wa upinzani kukosoa serikali iliopo madarakani kwa mujibu wa sheria na taratibu tulizoziweka ili wananchi waione haifai katika kuleta maendeleo
Mtangazaji: Kwa hiyo lengo ni kuwafanya wananchi waione serikali haifai?
Msigwa: Ndio, ndio, ndio kazi yetu
Mtangazaji: Je, ni kweli haifai?
Msigwa: Ndio
Nadhani hapa ndipo wapinzania wetu mnakosea.......sidhani kama maana ya opposition ni kuwafanya wananchi waichukie serikali.........hiyo sio kweli.....lengo la upinzani ni kushika dola.....wasipofanikiwa lengo lao ni kutoa mawazo endelevu katika kuifanya serikali iongeze bidii katika kuleta maendeleo na kama ikishindwa hayo mawazo yao yanageuka kuwa sera katika uchunguzi mkuu.....ila hii ya kuwafanya wananchi waichukie serikali yao nadhani sio sahihi