Peter Msigwa: Kama Mbunge unaweza kutungiwa kesi, hali lazima iwe mbaya kwa raia wa kawaida

Ghazwat

JF-Expert Member
Oct 4, 2015
23,718
66,262
cda099f0b9f2353572c1283bf022eeb8.jpg
Mbunge wa Iringa Mjini (CHADEMA), Peter Msigwa ametamaushwa na hali ambayo ameikuta kituo cha polisi Iringa Mjini na kusema kuwa hali lazima iwe mbaya kwa raia wa kawaida.

Kulingana na taarifa ambayo ameelezea kupitia ukurasa wake wa Twitter, Msigwa amesema;

"Kama Mbunge unaweza kutungiwa kesi. Hali lazima iwe mbaya sana kwa raia wa kawaida. Nimekuta kituo cha polisi Iringa Mjini kuna watu wapo mahabusu polisi zaidi ya siku ishirini hawajapelekwa mahakamani. Vijana wa Chadema wamekaa mahabusu zaidi ya siku saba bila kupelekwa mahakamani".

Ameandika Mbunge huyo Peter Msigwa.
 
Majuha wameshika usukani wakiendesha Lori lililopakia makondoo. Na kwa ukimya uliotawala ndani ya lori, licha ya maumivu makali, majujuha wanapata ujasiri wa kuwasifia makondoo ati yanafurahia safari ya Lori. Tutafungwa sana.
 
Kamanda Msigwa aliwai kumwambia Polepole kuwa viatu vya Nape havimtoshi, Polepole akamjibu kamanda Msigwa kama ifuatavyo, wewe Msigwa mwaka 2020 hutopata tena.
Sasa nachelea kusema isije kuwa babu Polepole ndo keshaingia vitani.
 
Ukiona mtu anajiita kiongozi huku form IV anaziro unategemea maendeleo gani? Visasi ndivyo vinatawala
 
Kabisa na wengine wanauwawa na miili yao kutupwa baharini. Ben Saanane tunaingia mwaka wa pili, Mwandishi wa Mwananchi mwezi wa tatu huu hajulikani aliko baada ya kuchukuliwa na “watu wasiojulikana”

cda099f0b9f2353572c1283bf022eeb8.jpg
Mbunge wa Iringa Mjini (CHADEMA), Peter Msigwa ametamaushwa na hali ambayo ameikuta kituo cha polisi Iringa Mjini na kusema kuwa hali lazima iwe mbaya kwa raia wa kawaida.

Kulingana na taarifa ambayo ameileza kupitia ukurasa wake wa Twitter, Msigwa amesema;

"Kama Mbunge unaweza kutungiwa kesi. Hali lazima iwe mbaya kwa sana kwa raia wa kawaida. Nimekuta kituo cha polisi Iringa Mjini kuna watu wapo mahabusu polisi zaidi ya siku ishirini hawajapelekwa mahakamani. Vijana wa Chadema wamekaa mahabusu zaidi ya siku saba bila kupelekwa mahakamani".

Ameandika Mbunge huyo Peter Msigwa.
 
Kabisa na wengine wanauwawa na miili yao kutupwa baharini. Ben Saanane tunaingia mwaka wa pili, Mwandishi wa Mwananchi mwezi wa tatu huu hajulikani aliko baada ya kuchukuliwa na “watu wasiojulikana”
Hali ya kusikitisha mno..!
 
  • Thanks
Reactions: BAK
kiukweli kwa haya yanayoendelea...akifa ,au akiugua ndg yang waccm sitokuwa tiyar kushiriki kwa lolote...
 
Alishasema hajaribiwi
Hapa ni hakuna kubip ukileta za kuleta utapambana na hali yako
Nchi kuongozwa kistaarabu ilishapitwa na wakati
Tunyooshe baba jeska tupo pamoja nawewe,,Heshima lazma irudi Nchini
 
Alishasema hajaribiwi
Hapa ni hakuna kubip ukileta za kuleta utapambana na hali yako
Nchi kuongozwa kistaarabu ilishapitwa na wakati
Tunyooshe baba jeska tupo pamoja nawewe,,Heshima lazma irudi Nchini
Kulikuwa na katili kama jammeh wa Gambia leo hayupo na huyu ipo siku atakuwa fala tu
 
Back
Top Bottom