Peter Msigwa(CHADEMA): Polisi waache kuisaidia CCM, ninachofanya ni sehemu ya majukumu yangu kama Mbunge wa Upinzani

radika

JF-Expert Member
Jul 15, 2014
20,427
32,193
Mbunge wa Iringa Mjini kwa tiketi ya CHADEMA, Mchungaji Peter Msigwa amefunguka na kulitaka jeshi la polisi nchini kutokisaidia Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kusema wamuache yeye na CHADEMA wapambane kukiondoa chama hicho madarakani kwani kimeshachoka.

Msigwa amesema kitendo cha polisi juzi kummamata wakati akiwa kwenye majukumu yake ya kibunge kimemuudhi sana na kusema ni jukumu la Mbunge yoyote yule kuelimisha jamii, kuwapa habari wananchi pamoja na kuikosoa serikali.

"Mimi nilikuwa sifanyi uchochezi kazi ya Mbunge kuelimisha, kuhabarisha, kuikosoa, kuisimamia serikali na kuchochea maendeleo katika jimbo kwa hiyo kama Mbunge ninayo haki ya kuzungumzia Demokrasia na haki ya kuzungumzia mambo ya utawala bora, nina haki ya kuzungumzia haki za binadamu. Kitendo cha Polisi kunikamata juzi kimeniudhi sana hao polisi waniache mimi na chama changu tupambane na CCM, wasiisadie CCM kwani saizi imechoka ipo dhohofu yaani ipo taabani wanajaribu kuitetea CCM, wajitokeze CCM wenyewe wajibu hoja"alisema Msigwa

Msigwa aliendelea kusema kuwa yeye ni Mbunge ana haki ya kuikosoa serikali iliyopo madarakani hata kuichonganisha na wananchi ili wasiichangue tena mwaka 2020 anadai huo ndiyo wajibu wake kisiasa na ndiyo maana anakuwa mpinzani.
 
Msigwa aliendelea kusema kuwa yeye ni Mbunge ana haki hata kuichonganisha na wananchi ili wasiichangue tena mwaka 2020 .

HA HA HA kazi ya mbunge wa upinzani ni kuichonganisha serikali kwa wananchi???? msigwa anaandika biblia mpya inayosomeka "HERI WACHONGANISHI MAANA WATAMUONA MUNGU".MSIGWA ni fake pastor
 
HA HA HA kazi ya mbunge wa upinzani ni kuichonganisha serikali kwa wananchi???? msigwa anaandika biblia mpya inayomeka HERI WACHONGANISHI MAANA WATAMUONA MUNGU.MSIGWA ni fake pastor
Mama rwakatale?
 
HA HA HA kazi ya mbunge wa upinzani ni kuichonganisha serikali kwa wananchi???? msigwa anaandika biblia mpya inayomeka HERI WACHONGANISHI MAANA WATAMUONA MUNGU.MSIGWA ni fake pastor
Da! ungekua umepungukiwa damu tungekuongezea, tatizo umepungukiwa akili tunakuhurumia.
 
Kati ya Polisi wote Tanzania mimi namheshimu RPC wa Geita,, huyu jamaa ameonesha kujitambua wazi kabisa na anajua majukumu ya Polisi siyo kuibeba CCM hata kwenye maovu. Ka Musukuma kakijidai tunakavunja miguu na radhi hatuombi!!
 
M/kiti wenu achomoki kwenye hili....

Kwanini haya mauza uza huwa yanatokea kipindi chama kinaelekea kwenye uchaguzi????
Na ukifatilia kiundani zaidi LISSU hili asimame 2020 kama mgombea rais kupitia chadema ILIKUWA NI LAZIMA AWE M/KITI wa CHAMA au mtu mwingne tofauti na mbowe,na to be honest hata kesho LISSU akisimamishwa na MBOWE uenyekiti ndani ya CHAMA lazima MBOWE akae.

Na mkumbuke kabsa LOWASSA ana nguvu ndani ya CHADEMA zama hivi kwa mgongo wa MBOWE na si LISSU hivyo moja kwa moja LISSU alikuwa ni threat kubwa sana kwa mustakabali wa hawa BOYS TWO MEN wa hiki chama....

Na the only option waliokuwa nao ni kumwondoa LISSU tu ili LOWASSA awe safe kusimama 2020 ndani ya CHADEMA......

NA hii uponyaji wa MWENYEZI MUNGU JUU YA LISSU....ni maumivu makubwa sana kwa hawa wawili......na pia ni HATARI PIA KWA MUSTAKABALI WA CHADEMA kuelekea 2020 NA CHAGUZI ZA NDANI YA CHAMA
 
Kipindi kifupi ( kisichozidi siku 60) kabla ya uchaguzi mkuu kufanyika huwa kinatolewa kwa wanasiasa kuongea maneno kama hayo. Kipindi hicho huitwa kipindi cha kampeni na hutolewa kwa mjibu wa sheria na tume ya uchaguzi ambayo pia hubainisha maneno yanayoruhusiwa na yale yasiyoruhusiwa. Kipindi hicho huwa kipindi tete sana kwa taifa na shughuli nyingi za kiuchumi hususani utalii huzorota. Usalama wa taifa huwa kwenye hali tete. Bahati nzuri kipindi hicho huwa ni kifupi, mkiisha kivuka salama ni hadi miaka 5 ipite ndipo kitakuja kingine.

Shida ya wanasiasa kama akina Msigwa na kundi lake la chadema ni kuamini kuwa dhana ya vyama vya upinzani wa kisiasa inafanya kipindi hicho cha kampeni kuwa hakina kikomo. Hawataki kuamini kuwa maneno ya aina hiyo yakisemwa nje ya kipindi hicho ni uchochezi au uhaini kwa mjibu wa katiba na sheria zetu. Katiba imeruhusu yasemwe kwenye kipindi hicho kifupi cha kampeni za kuelekea uchaguzi mkuu kwa kiwango kitakachokubalika kati ya tume ya uchaguzi na vyama vya siasa.
 
Mbunge ana haki ya kuikosoa serikali iliyopo madarakani hata kuichonganisha na wananchi ili wasiichangue tena mwaka 2020 huo ndiyo wajibu wake kisiasa na ndiyo maana anakuwa mpinzani-Msigwa
 
Back
Top Bottom