Msechu ambaye ametoa video ya ‘Malava’ hivi karibuni inayoonekana kuwavutia wengi kutokana na jinsi alivyoutumia unene wake kufanya video ifurahishe, amesema kuwa watu inabidi wafahamu kwamba kwenye familia yao yeye ndiye mwembamba kuliko wote.
“Kuna kitu ambacho watu hawafahamu, watu wanaofahamu familia ya mzee Msechu, wajaribu kufatilia watawaambia yaani mimi ndio model,” alisema Msechu kupitia 255 ya XXL. “Yaani mimi na kitambi changu na mwili wangu nilivyo watu wanasema mimi mnene lakini katika familia yetu mimi ndio model, mimi ndio mtu ninayeangaliwa, yaani watu wananiangalia lini nitapungua hata kama Msechu. Sisi tuko hivyo marehemu mama yangu alikuwa yuko hivi, baba yangu amepungua tu kwasababu ya uzee lakini tuna miili.”
Msechu ambaye pia ana kipaji cha kuchekesha hakuacha kuongeza utani kuhusu unene wake kwa kumtania swahiba wake Baba Levo.
“Miili kama hii ni rahisi sana kupata mkopo, ukiwa na mwili kama huu ukiingia nao benki hawakuulizi…lakini sasa una mwili kama Baba Levo, ukienda sehemu kama Ubalozi wa Marekani ukitaka kwenda michongo yako ya nje…lazima upimwe kwasababu watu wanahisi unaweza ukawa na maebola, kwahiyo kidogo kuna sehemu zingine unapenya tunatereza kwasababu kidogo watu wanaona huyu jamaa ana afya ingawa ni wrong perception ya Waafrika wengi.” Alisema Msechu.