Peter "mmanga" alisifika kwa wizi wa vioo vya magari miaka ya 80,90 na mwanzoni 2000

Mleta mada anasema eti peter ndiyo vijana wa mwanzo mwanzo kutumia madawa miaka hiyo ya 80, uyu mleta mada ni janga la taifa.
Inawezekana binafsi mateja nilikua nawaonaga tu ila kumwona mtu anavuta unga kabisa ilikua ni 2015.
 
Simjui bhana, nenda kaulizie hapo Lumumba, au mnatafuta vijana wa kuwafanya punda mpate hela za kuendesha kampuni ya propaganda hapo Lumumba?
 
Huyu jamaa nilimuona mwezi mmoja uliopita ila afya yake imetengemaa kidogo,baba yake anaitwa mzee kikwasi,huyu mzee naona nae kama anachanganyikiwa sasa
 
Ndugu zangu,

Kwa wale waliowahi kuishi Mwenge na maeneo jirani ya Sinza na Kijitonyama miaka ya 80 na 90 mtakumbuka uwepo wa wizi wa vioo vya magari ndani ya fensi za nyumba mida ya usiku na sehemu za starehe kama mabaa na kumbi za starehe zisizokuwa na ulinzi wa kutosha.

Kijana ambaye ni mkazi wa Mwenge akijulikana kwa jina la Peter "mmanga",shombeshombe mwenye asili ya Kigiriki ambaye ni mmoja wa vijana wa mwanzo jijini Dar kutumia madawa ya kulevya.Kwa hakika Peter alikuwa na kipaji hususani kwa kutumia muda mchache kuchomoa kioo cha mbele cha gari lolote litakalokuwa katika anga zake,wengi waliamini kuwa ni "hakimu" wa vioo sababu ya umahiri wake wa kung'oa na kutoweka bila ya kukamatwa.Vioo hivyo vilipelekwa "mnadani" jirani kabisa na kituo cha polisi cha Msimbazi na endapo utatoa ushirikiano kwa kulipa kiasi cha pesa kwa makubaliano utarudishiwa ila ukienda polisi hupati na vibaka hao wakizidiwa hukipasua kioo na kuondoka.

Miaka ya mwanzoni 2000 Peter alijiingiza pia kwenye fani ya ukabaji ili kujikidhi na uraibu wa madawa ya kulevya hata hivyo katika fani hii alikumbana na dhoruba ya kutupwa jela mara kwa mara kiasi cha kumfanya kudhoofika sana na ilipofika mwaka 2005 Peter "mmanga" aliokoka na kujiunga katika kanisa na Nabii Josephat Mwingira na kwa muda akaacha tabia za uraibu wa madawa ya kulevya na ukabaji.Afya yake ilitengemaa sana.

Nakumbuka kati ya mwaka 2010/11 nilikutana naye akiwa mdhoofu nikahisi kuwa karudia tena kwenye uraibu ni takribani miaka minane (8) sijawahi kuonana naye na wala sijui anafanya shughuli gani.

Mwenye kujua zaidi atujuze.
CCM ndiyo chanzo cha kuharibikiwa kwa hao vijana maana hiyo sembe inaletwa na makada wa kijani
 
Peter yupo, na week jana nmeonana naye.
Sasa hivi anasali .
Ni pm ukiwa na shida naye
 
Back
Top Bottom