Indume Yene
Platinum Member
- Mar 17, 2008
- 2,958
- 718
Ni jambo la kushangaza kuona Mtanzania Halisi ambaye amewahi kushika madaraka katika serikali ya SISEMU leo hii kumshambulia Mbunge Anne Kilango kwa vita dhidi ya VISADIZ.
Naamini anatumia haki yake kikatiba kutoa maoni yake ila siamini kama umri wake unapelekea fikra zake kuzeeka vilevile. Si ajabu hii itakuwa ni kujipendekeza kwa serikali na chama chake angalau wamuangalizie hata ubunge wa kuteuliwa if Makamba atakuwa sacked.
Soma hii habari hapa kutoka Tanzania Daima kisha utoe maoni yako.
Kisumo amlipua Mama Kilango
na Charles Ndagulla, Moshi
MOTO aliouwasha Mbunge wa Same Mashariki (CCM), Anne Kilango Malecela, kuhusu wizi wa fedha za akaunti ya malipo ya madeni ya nje (EPA), umeendelea kuzua makubwa, baada ya mwanasiasa mkongwe nchini, Peter Kisumo, kumshutumu mbunge huyo machachari kuwa ana idhalilisha CCM.
Akizungumza na waandishi wa habari mjini Moshi, Kisumo alisema Mama Kilango amejivisha jukumu la wapinzani kuishutumu serikali juu ya tuhuma za ufisadi, wakati yeye mwenyewe (Mama Kilango), anatokea CCM, inayoongoza serikali.
Alisema kutokana na kauli zake kali bungeni kuhusu suala la EPA, Kilango hastahili kabisa hata unaibu waziri, kwani alichokuwa akikisema ni sawa na kumtukana mkuu wa nchi, serikali na CCM.
Kisumo alisema matamshi yaliyotumiwa na Kilango kwenye kikao cha Bunge la bajeti kinachoendelea mjini Dodoma kwamba kama fedha za EPA hazitarejeshwa bungeni hapatatosha, ni maneno mazito na yasiyostahili kutolewa na mbunge wa chama kinachoshika madaraka.
Alibainisha kuwa matamshi ya Kilango yameonyesha jeuri ya hali ya juu kwa chama chake, kwa kuongea kwa ukali bungeni juu ya sakata la ufisadi katika akaunti hiyo ya EPA.
Alisema alichokifanya Kilango ni kutotii maelekezo ya chama chake yaliyotolewa kwa wabunge wote wa CCM na Katibu Mkuu, Yusuf Makamba, katika kikao cha wabunge wote wa chama hicho.
Kwa mujibu wa Kisumo, maagizo hayo ya CCM kwa wabunge wake kuhusu suala hilo, yalitaka mjadala huo usiendelee kuwa ajenda bungeni, kwani tayari lilikuwa linafanyiwa kazi na tume iliyoundwa na Rais Jakaya Kikwete.
Huyu Kilango jeuri hii ya kuzungumza mambo kama haya kaipata wapi wakati CCM walisema mjadala huo usiendelee bungeni kwa kuwa linatafutiwa ufumbuzi? Hafai hata kupewa unaibu waziri, alisema Kisumo.
Alisema wizi uliotokea Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kupitia akaunti ya malipo ya madeni ya nje (EPA), ulishaanza kufanyiwa kazi na Rais Jakaya Kikwete, kwa kumfukuza aliyekuwa Gavana wa Benki Kuu (BoT), Daudi Balali, pamoja na kuunda tume iliyomaliza kazi hivi karibuni.
Alipotafutwa kwa simu kuzungumzia shutuma hizo, Mama Kilango alisema kwa ufupi kuwa, anatafakari kauli hiyo nzito iliyotolewa na mtu aliyedai anamheshimu sana.
Wakati Rais Kikwete alipochukua fomu kuwania nafasi hiyo, Kisumo alieleza msimamo wake wa kumuunga mkono, huku akipiga vijembe kuwataka wazee wamwachie Kikwete kushika nafasi hiyo.
Ingawa hakumtaja jina mzee aliyemlenga katika maelezo yake, lakini ni dhahiri kwamba alikuwa akimzungumzia mzee John Samwel Malecela, mume wa Mama Kilango, ambaye naye aliwania nafasi hiyo.
Katika hatua nyingine, Kisumo ameweka wazi tofauti zake dhidi ya mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM taifa, Aggrey Marealle, ambaye pia ni Naibu Kamanda wa Umoja wa Vijana wa CCM, Manispaa ya Moshi.
Kisumo amedai kuwa, kama CCM itampitisha Marealle kuwania ubunge katika Jimbo la Moshi Mjini, katika uchaguzi mkuu ujao mwaka 2010, jimbo hilo litaendelea kuwa kambi ya upinzani.
Alisema hata kama mbunge wa sasa wa jimbo hilo, Philemon Ndesamburo (CHADEMA), hatagombea katika uchaguzi mkuu ujao na Marealle akashindanishwa na mtu mwingine kutoka kambi hiyo ya upinzani, bado jimbo hilo litanyakuliwa na upinzani.
Ameongeza kuwa pamoja na jitihada za makusudi zinazofanywa na Marealle kutoa misaada ya kijamii katika maeneo mbalimbali ya mji wa Moshi kupitia Kampuni yake ya mahusiano ya Executive Solutions, jitihada hizo hazitamsaidia.
Hii ni mara ya pili kwa Kisumo kutoa maneno makali dhidi ya Marealle, ambapo mara ya kwanza ilikuwa kwenye mkutano mkuu wa CCM Manispaa ya Moshi mwaka jana.

Last edited by a moderator: