Peter Kisumo: Toka 1995 hadi sasa hakuna kama Kinana!

Mandla Jr.

JF-Expert Member
Dec 15, 2013
3,100
1,195
Mwanasiasa Mkongwe Peter Kisumo amemsifia Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahaman Kinana kwa kusema toka mwaka 1995 mpaka leo hakuna aliyemfikia Kinana katika nafasi hiyo.

Pia Kisumo amemtaka Rais Kikwete kuiga Marais waliomtangulia kwa kufanya maamuzi dhidi ya viongozi wa serikali na sio kusubiri mpaka Wabunge wapige kelele.
 
Frank Wanjiru

JF-Expert Member
Apr 12, 2012
14,150
2,000
Naona sasa huyu Mzee zile njaa zilizokuwa zinamsumbua kwa kubwabwaja bwabwaja hovyo kuhusu Magamba tayari zishapata chakula eeh?. Ama kweli Nchi hii sasa hivi haina Wazee wenye Busara na Maono,kila Mtu anajali tumbo lake,huyo Mzee wa Ndovu amefanya nini cha maana zaidi ya kumaliza Tembo wetu,au anamaanisha hakuna mwingine kwa kuua Tembo wetu kama kinana?
 
Bulesi

JF-Expert Member
May 14, 2008
8,691
2,000
Huyu Mzee ndiye alikuwa mtu wa kwanza kumpigia debe Kikwete aukwae URAIS 2005, inaelekea matarajio yake kutoka kwa urais wa Kikwete hayajatimia na ndio maana naona anaanza mapema kujipanga upya!!! Njaa haina uzee....!!!!
 
Mandla Jr.

JF-Expert Member
Dec 15, 2013
3,100
1,195
Huyu Mzee ndiye alikuwa mtu wa kwanza kumpigia debe Kikwete aukwae URAIS 2005, inaelekea matarajio yake kutoka kwa urais wa Kikwete hayajatimia na ndio maana naona anaanza mapema kujipanga upya!!! Njaa haina uzee....!!!!

Kwa umri alionao mzee Kisumo kaona mengi sana. Hivyo ni lazima amuonye bwana mdogo kutoka Tanzania- Kikwete.
 
Bulesi

JF-Expert Member
May 14, 2008
8,691
2,000
Kwa umri alionao mzee Kisumo kaona mengi sana. Hivyo ni lazima amuonye bwana mdogo kutoka Tanzania- Kikwete.

Mbona hata wakina Mzee Mustapha Songambele wameona mengi lakini hawapigi kelele kama huyu? Lazima huyu Mzee Kisumo atakuwa na lake jambo ambalo Kikwete hakumtimizia, sio bure!!!
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom