Pete ya uchumba

believer

JF-Expert Member
Dec 22, 2012
633
213
wadau nataka kupata uzoefu kidogo,jamaa yangu mmoja analalamika kuwa amekuwa na mahusiano na mpenzi wake kwa mwaka mmoja na nusu sasa,imefikia hatua wametambulishana na amemvalisha pete ya uchumba,tatizo ni kuwa huyo mchumba muda wote anaokua nyumbani havai pete hiyo,so huyu jamaa yangu anajiuliza na kabla hajamuuliza mhusika kanielezea mm,so wadau kwani kuna tatizo hapo?
 
Sasa anajiuliza nini wakati hajui sababu zinazomfanya huyo mpenzi wake kutovaa hiyo pete? inatakiwa apate majibu ndo ayapime kama yanamantiki ndo aombe ushauri,binafsi sijui mwanamke anatakiwa avae muda gani hiyo pete kama ni muda wote au kuna muda tu ndo anatakiwa kuvaa!
 
labda amegundua hiyo pete ni ya kichina. so anaogopa isije ikapauka haraka anapoivaa nyumbani. huku akiwa na shughuli ndogondogo hasa zile za kushika maji.
 
labda amegundua hiyo pete ni ya kichina. so anaogopa isije ikapauka haraka anapoivaa nyumbani. huku akiwa na shughuli ndogondogo hasa zile za kushika maji.

hahaaa itakua bidhaa ya GUANZHOU hiyo pete
 
mwambie huyo nduguyo aache uoga wa kizembe,kwani pete kitu gani? Watu wanavalishana hiyo mipete na wanaachana kama kawaida bwana! Cha msingi anapendwa ama hapendwi! Jambo la msingi upendo tu
 
Pete ni urembo tu na umagharibi..kunachomatter ni emotional commitment.
 
pete ya uchumba ki ukweli kabisa sio utamaduni wetu
sio dili kivile na mbaya zaidi zingine zinaunganishwa na mizimu.
kwa hiyo kwangu sawa tu ningekuwa kuna kuoa tena nisingemvalisha mtu pete hii haina maana kabisa mke wangu nimemwambia sitaki kuiona kwenye kidole chake tena. ( una mke zaidi ya miaka 10 alafu bado anavaa pete ya uchumba kwa mchumba upi na ndoa ipi anayoitegemea baada ya kwenu kwisha)
nimemwambia kaiuze anunue kiatu kuliko kuiona tena
du! teh..teh... nimekuwa mnoko!
 
mh! Mkuu pete miaka kumi kidoleni? Atakua ni LORD OF THE RINGS huyo!
 
mh! Mkuu pete miaka kumi kidoleni? Atakua ni LORD OF THE RINGS huyo!

hapana haijafikia hapo ila inakama miaka saba sema naziona za washika dau waliotutangulia mpaka leo wanazo tu.
 
labda hajui,ngoja rafikie amfikishie ujumbe na akamuulize ni pete ya wapi hahaa

Mkuu sio cha wale jamaa wenye macho madogo,wakati anataka kununua hiyo pete kuna factors kadhaa alizihusisha,sonara wengi wa kibongo unachakachuliwa kirahisi,so alienda mtaa wa indra gandhi kuna maduka makini ya wahindi,by the way thanks kwa wote waliochangia,i ll share with him.
 
Hakuna usalama hapo anavuaje pete km ishu kua ya kichina la msingi iwe kidoleni ikipauka kwn ni kesi kuna kitu anaficha uyo mdada kwa ss wenye mboni za kifisi babu mshikaji wako anamegewa.
Mtazamo wng.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom