Pete ya uchumba ya kiume | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Pete ya uchumba ya kiume

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Raia Fulani, Sep 3, 2009.

 1. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #1
  Sep 3, 2009
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,220
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Mi nadhani imefika wakati sasa na mabinti kuwavisha watarajiwa wao pete za uchumba kama wao wavishwavyo. Hii pia itasaidia kumwepusha mchumba mume na mabinti. Tumeona kichen pati za kiume, mwanaume kuvishwa pete ya uchumba itashindikana? Em wadada mtoe mawazo katika hili maana linawahusu direct. Mi nitafurahi nikivishwa na atakayekuwa mtarajiwa wangu
   
 2. Safina

  Safina JF-Expert Member

  #2
  Sep 4, 2009
  Joined: Jun 18, 2009
  Messages: 498
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mziwanda umepinda, hii haijakaa vyema hata kidogo. Unajua wanawake tumewaachia wanaume wawe vichwa vya familia na kama ni kichwa cha familia wewe ndio unatakiwa kuwa msemaji mkuu, kingine nilichokuwa nasemea ni kwamba wanaweke c ambao huwa tuna-propose inamaana nikikuvisha pete halafu useme haujawa tayari inakuwaje? Nyie wanaume huwa mkiulizwa jamani tutaona lini unaona ni kero kubwa haya sasa aseme anaku-engage utasubiri yeye ndo apropose na tarehe ya harusi. Kwa maana hiyo utakuwa umempa mamlaka mkeo na hivyo hata mkioana yeye ndio atabaki kuwa kichwa cha familia.

  Swali kwako wewe mziwanda umeshamwambia huyo msichana wako kwamba unasubiri yeye akiwa tayari akuvishe pete?
   
 3. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #3
  Sep 4, 2009
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  No comment
   
 4. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #4
  Sep 4, 2009
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,220
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  dada yangu nimekusoma. Suala la uongozi wa familia bado ni la mume. Mwanamke nae ana wajibu wa kummiliki mumewe mtarajiwa na njia mojawapo ni hiyo pete. Msione hili ni geni sana au tusubiri wazungu watuanzishie ndo tujue linawezekana
   
 5. syba

  syba New Member

  #5
  Sep 4, 2009
  Joined: Aug 7, 2009
  Messages: 2
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mimi sitaki kuwekwa uchumba, nisije nikawa mwanamume kibinti bure...........! Shaulilo wewe unayeintertain hayo mambo.......!
   
 6. Mvina

  Mvina JF-Expert Member

  #6
  Sep 5, 2009
  Joined: Aug 2, 2009
  Messages: 1,000
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  Hapa ndo karibu tutakuja na hoja kwamba kwanini mwanamke asilipe mahari badala ya mwanaume?
  Kwa ushauri tu ni kwamba utaratibu tulionao ni mzuri tuache uendelee.
  Zidumu fikira za kila mmoja wetu hapa!
   
 7. Asprin

  Asprin JF-Expert Member

  #7
  Sep 5, 2009
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 50,841
  Likes Received: 23,459
  Trophy Points: 280
  Kama ni hivyo da safina, then hata pete ya ndoa msiwavishe wanaume.
   
 8. Mwana va Mutwa

  Mwana va Mutwa JF-Expert Member

  #8
  Sep 5, 2009
  Joined: Jun 9, 2009
  Messages: 429
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  duh labda ikiaza hii itakuwa ndio ya kwetu ya kwanza kuazisha wenyewe bila kuiga huko tunakoiga kila kitu,mkuu anzisha,mshauri shem akuvishe bwana,mi nilishachelewa.
   
 9. Kisoda2

  Kisoda2 JF-Expert Member

  #9
  Sep 5, 2009
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 1,240
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Kazi ipo,....
   
 10. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #10
  Sep 7, 2009
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,220
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  waambie mkuu. utaratibu mzuri huanzia awali, so awali ni pete ya uchumba kuvishana wote si mmoja kumvisha mwenzake. kwa maana nyingine ni kuwa katika uchumba, mwanamke ndiye anayebanwa na mwanaume yuko huru ila katika ndoa wote wanabanana. kwa nini wasibanane kuanzia uchumba?
   
 11. Johas

  Johas Senior Member

  #11
  Sep 7, 2009
  Joined: Feb 13, 2009
  Messages: 141
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Waheshimiwa! Nimezisoma hizo contributional zenu lakini mimi niko na mtazomo tofauti kidogo kuhusu issue yenyewe lakini bado ndani ya mstari PETE.
  Je? nini hasa maana(the logic behind) ya pete ya uchumba/ Ndoa kwa coupes.

  Maandiko Matakatifu ya Biblia na quran yanasemaje kuhusu Pete?

  Kimtazamo wangu Pete ya uchumba/Ndoa haina mantiki yeyote kwa coupes ila ni western culture ambazo tunajaribu kuiga sisi waafrika, ebu jiulize wazee wetu wa zamani walikuwa wanavishana nini? na ndoa au uchumba vilishamili tuu.

  Kwahiyo issue ya nani amvishe na nani avishwe between Man and woman nafikili sio issue, regardness kuwe na dhamila ya kweli kwa wahusika.
   
 12. Sinkala

  Sinkala JF-Expert Member

  #12
  Sep 7, 2009
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 1,505
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Nadhani pete za uchumba zisiwepo kabisa hata kwa wanawake, kwani hazina maana tena baada ya ndoa. Zinaongeza tu gharama kwa mwanaume.
   
 13. Kobe

  Kobe JF-Expert Member

  #13
  Sep 7, 2009
  Joined: Jun 17, 2009
  Messages: 1,756
  Likes Received: 361
  Trophy Points: 180
  Mi saifiki bana.! haingii akilini kidume aliye timilifu akavishwe pete ya uchumba na m/ke
  swali kwako mziwanda.
  Unawezaje kuibadili fikra hii kwa wazazi na familia yako bila kutiliwa shaka yeyote na wanajamii wako juu ya utimilifu wako kama mtoto wa kiume.?
   
 14. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #14
  Sep 7, 2009
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,220
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  mkuu mbona unatulia mbele ya kadamnasi na kuvishwa pete ya ndoa?
   
 15. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #15
  Sep 7, 2009
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,220
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  ila mzee pete zina nafasi yake na aliyeleta hiyo falsafa hakuibuka tu. tukisema tumeiga kwa wazungu basi ni mengi sana tunadaiwa na hao wazungu. mi binafsi nikiona mkono wa mwanamke una pete hata kama nilikuwa na nia fulani basi hutoweka
   
 16. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #16
  Sep 7, 2009
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  makubwa hayo!!!
   
 17. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #17
  Sep 7, 2009
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,220
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  duh! thanks 2749!!! for the newly married couple. ila angalia mama watoto mtarajiwa asikusikie mkuu
   
 18. Sinkala

  Sinkala JF-Expert Member

  #18
  Sep 7, 2009
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 1,505
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Haa haa haaa !! Yupo humu humu JF lakini hajui ID yangu, labda aunganishe events na post ninazozibandika !!!
   
 19. A

  Alvin Member

  #19
  Sep 7, 2009
  Joined: Sep 7, 2009
  Messages: 9
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hapo mnaniua wakuu
   
 20. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #20
  Sep 8, 2009
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,220
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  sasa nyie si mwili mmoja? ila kama ni janjauri atajua tu. umetangaza kufunga ndoa humu nae si anaona? si ajabu alichangia mawazo, hadi kufikia ndoa bado asikujue tu? na wewe hope unaijua ID yake
   
Loading...