Pete kubwakubwa wavaazo wanasiasa, wanamuziki na wafanyabiashara kwenye vidole vya mikono maana yake nini?

Freed Freed

JF-Expert Member
Jun 27, 2017
6,224
6,467
Habari kwako mwana wa JF. Hongera kwa jumapili tulivu.

Nimekuwa nikiwaona watu mbalimbali wenye dhamana ktk jamii wakivaa Pete kubwa kwenye vidole vya mikono. Sio hao tu bali pia wanamuziki, wafanyabiashara na watu wengine uchwara kabisa.

Jana pia kwenye video nilimwona Rais mstaafu wa SA Thabo Mbeki katinga bonge la mpete.
Je Pete hizi za kazi gani? Changia bila assumptions au mabunio tu yasiyo na tija na uwe na uhakika kabisa na usemacho ili tutoane matongotongo humu jukwaani.
 
Kuna pete za urembo tuu kufurahisha nafsi, kuna pete za ishara kuonyeshea status fulani kama pete za uchumba, ndoa, maaskofu, wafalme etc.
Kuna pete za Vito vya urembo tuu na kuna pete za Vito vya bahati, kuna pete za maagano kama kinga and mafanikio fulani na kuna pete za majini za kufanyia mambo au kuleta mafanikio au kufanya maangamizi. Pia kuna pete za miujiza hadi za utajiri.
P
 
Niliambiwa kwa wale wenye pete zenye kama vito huwa ni kwa ajili ya mvuto au bahati.
Wale wanaovaa gold au silver plain wanavaa urembo tuu
 
Kila avae Pete uvaa Kwa maana yake Kwa Urembo,fashion, imani,hobby,maagano.nk hakuna maana moja.
 
Kwa wanaoamini elimu ya nyota,pete yenye kito chenye kulingana na siku ya kuzaliwa,basi huamini kuwa zina nguvu kubwa katika shughuli afanyazo
Sijajua kwa maaskofu na mashekhe kwa nini wanavaa
 
Kuna pete za urembo tuu kufurahisha nafsi, kuna pete za ishara kuonyeshea status fulani kama pete za uchumba, ndoa, maaskofu, wafalme etc.
Kuna pete za Vito vya urembo tuu na kuna pete za Vito vya bahati, kuna pete za maagano kama kinga and mafanikio fulani na kuna pete za majini za kufanyia mambo au kuleta mafanikio au kufanya maangamizi. Pia kuna pete za miujiza hadi za utajiri.
P
OK, asante kwa muangaza huu
 
Dahhh....
Afadhali umedadavua, maana nilipoona heading ya pete kubwa basi akili yote ikakimbilia kwenye zile zenye tunavaaga ili kuzuwia isi ingie yote kwenye kipenyo....
 
Walau nimekuelewa kidogo
Mfano kuna baadhi ya imani viongozi wa dini wakifika daraja Fulani uvaliwa Pete ikimaanisha ni maagano matakaitifu kwamba umefunga maagano na Mungu au shetani kwamba utamtumikia maisha yako yote.
 
Back
Top Bottom