Pete kubwa kubwa wavaazo wanasiasa, wanamuziki na wafanyabiashara kwenye vidole vya mikono maana yake nini?

Hayo mambo yanatisha ndiyo maana wakiongea wanahakikisha hizo pete zinawaelekea wasikilizaji. Kuna siku nilikutana na kiongozi fulani kavaa hayo mapete nikajikuta nashindwa hata kuongea yaani full kubabaika.
Hivyo vitu vina nguvu ya kiza.
Alafu baadhi ya wenye Pete hizo, wakiongea huweka mkono mfukoni mwa suruali kama anapapasa kitu kisha huchomoa mkono wake. Hasa anapoongea na jumuiko la watu wengi.
 
Hizo pete ni agano, kati ya mvaaji na mtoaji. Kila agano lina sadaka na sacrifie yake... na agano ni kama mkatana wa pande mbili.

Pia sio kila pete ni ya agano, wengin ni urembo au kumbukumbi flani tu, na zinakuwa hazina nguvu aina yoyote ile.

Wengine hawavai ma pete , lakini wana mahirizi viunoni na mikononi..

Wengine hawana vyote, ila walimezeshwa madude dude,

Wengine walikufa na wakafufuliwa na kupata nguvu za giza...

Nikianza andika hapa nitajaza server za Jf
Dunia ina mengi sana
 
Habari kwako mwana wa JF. Hongera kwa jumapili tulivu.

Nimekuwa nikiwaona watu mbalimbali wenye dhamana ktk jamii wakivaa Pete kubwa kwenye vidole vya mikono. Sio hao tu bali pia wanamuziki, wafanyabiashara na watu wengine uchwara kabisa.

Jana pia kwenye video nilimwona Rais mstaafu wa SA Thabo Mbeki katinga bonge la mpete.
Je Pete hizi za kazi gani? Changia bila assumptions au mabunio tu yasiyo na tija na uwe na uhakika kabisa na usemacho ili tutoane matongotongo humu jukwaani.
"Changia bila assumptions au mabunio tu yasiyo na tija na uwe na uhakika kabisa na usemacho ili tutoane matongotongo humu jukwaani." Mkuu hili angalizo litaogopesha watu sana kuchangia,ungeacha open tu watu waka kanyaga tope ungepata mawazo mazuri sana.Kwani what do you lose by letting them provide what they know?
Anyway tuachane na hili.

Kwa kawaida pete zinavaliwa kwa madhumuni mahususi.
Ifuatayo ni maana halisi ya uvaaji wa pete na maana yake katika kila kidole.

Usivae tu pete bila kujua nini maana ya kile unachokivaa,kwani kinaweza kukuletea shida zisizo za msingi,kwani uvaaji wa pete waweza kuchukuliwa kawaida kwa mhusika,lakini hali ikawa tofauti kwa watu wanaokutazama,hivyo ni muhimu japo kufahamu baadhi ya maana zifuatazo.

Kidole kidogo.Kuvaa pete katika kidole kidogo ni kwa ajili ya kuvuta mtazamo ( to draw attention).

Chanda. Pete inayovaliwa katika kidole hiki ni kwa ajili ya uchumba na ndoa. Utafiti unaonyesha kwamba pete hii huvaliwa kidole hiki kwa sababu inasemekana kuna mshipa wa damu ambao hutoka moja kwa moja moyoni. Hivyo watu wanaamni kwamba mchumba au mwanandoa akikuvisha pete kidole hiki ni ishara ya kujiunga moyoni mwako.

Kidole cha kati. Pete inayovaliwa kidole hiki mara nyingi inaonyesha uwezo na majukumu,maana ni kidole kirefu kuliko vingine.Hapa ndipo panapo weza kuwa na maloloso.Watu walio wengi huvaa pete za kishirikina katika kidole hiki ili kuweza kufanikisha kishirikina malengo yao.Hapa wapo viongozi,wana muziki,wafanyibiashara nk.Jinsi pete ilivyo na germstones zinazowekwa inategemea malengo na maagizo.

Kidole cha kwanza. Kwa ajili ya utambulisho, mfano wa kundi ulilopo (affiliation).

Dole gumba. Huvaliwa tu kwa fasheni na kupamba.

Hivi ni lazima kila mtu achangie? tupotezeane muda kukagua reply mojamoja za makisio kutafuta ukweli wakati wajuzi wapo? Aah jamani! Mtoa mada uko sahihi kabisa Wengine tukae kimya wajuzi waseme tupate jibu Clear.
 
"Changia bila assumptions au mabunio tu yasiyo na tija na uwe na uhakika kabisa na usemacho ili tutoane matongotongo humu jukwaani." Mkuu hili angalizo litaogopesha watu sana kuchangia,ungeacha open tu watu waka kanyaga tope ungepata mawazo mazuri sana.Kwani what do you lose by letting them provide what they know?

Anyway tuachane na hili.Kwa kawaida pete zinavaliwa kwa madhumuni mahususi.

Ifuatayo ni maana halisi ya uvaaji wa pete na maana yake katika kila kidole.

Usivae tu pete bila kujua nini maana ya kile unachokivaa,kwani kinaweza kukuletea shida zisizo za msingi,kwani uvaaji wa pete waweza kuchukuliwa kawaida kwa mhusika lakini hali ikawa tofauti kwa watu wanaokutazama,hivyo ni muhimu japo kufahamu baadhi ya maana zifuatazo.

Kidole kidogo.Kuvaa pete katika kidole kidogo ni kwa ajili ya kuvuta mtazamo ( to draw attention).

Chanda. Uchumba na ndoa, na tafiti huonesha pete hii huvaliwa kidole hiki kwa sababu inasemekana kuna mshipa wa damu ambao hutoka moja kwa moja moyoni. hivyo mtu akikuvisha ni ishara ya kujiunga moyoni mwako.

Kidole cha kati. Uwezo na majukumu maana ni kidole kirefu kuliko vingine.Hapa ndipo panapo weza kuwa na maloloso.Wetu wengine huvaa pete za kishirikina katika kidole hiki ili kuweza kufanikisha kishirikina malengo yao.Hapa wapo viongozi,wana muziki,wafanyibiashara nk.Jinsi pete ilivyo pia na gemstones zinazowekwa pia inategemea malengo.

Kidole cha kwanza. Kwa ajili ya utambulisho, mfano wa kundi ulilopo (affiliation)

Dole gumba. Huvaliwa tu kwa fasheni na kupamba.

Nashukuru sana
 
Habari kwako mwana wa JF. Hongera kwa jumapili tulivu.

Nimekuwa nikiwaona watu mbalimbali wenye dhamana ktk jamii wakivaa Pete kubwa kwenye vidole vya mikono. Sio hao tu bali pia wanamuziki, wafanyabiashara na watu wengine uchwara kabisa.

Jana pia kwenye video nilimwona Rais mstaafu wa SA Thabo Mbeki katinga bonge la mpete.
Je Pete hizi za kazi gani? Changia bila assumptions au mabunio tu yasiyo na tija na uwe na uhakika kabisa na usemacho ili tutoane matongotongo humu jukwaani.
Ukiona mtoto wa kike kavaa pete kubwa wakati hajaolewa unaelewa nini
 
Hakika haya ni mahirizi. Kuna mipete ina macho, ndani ya yale macho ni hirizi. Mapete yale ni mahirizi. Cha ajabu ati hata maaskofu wanakuwa na mapete yake ati ya kiaskofu!
MAASKOFU PETE ISHARA YA MAMLAKA NOT MORE THAN THAT.
 
pete huvaliwa na wanandoa, wasanii, viongozi,waganga na matajiri. hapa ka sijakutoa matongotongo rudi kalale
 
Back
Top Bottom