Pete hailazimishwi, hujachumbiwa wee ushapost FB live na vijembe juu, mwanaume huyoo katokomea

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Jun 12, 2012
4,572
26,868
PETE HAILAZIMISHWI!
Umeanza na mtu mahusiano! Wewe ni "mgeli" umejiachia weeee, ukagundua mwanaume yupo kimaslahi! Si ukaanza kumbania salamu huku unamlazimisha akuvishe pete! Mwanaume akakukata jicho akaona dawa yako akupe matumaini, kwamba "ataangalia"... Shoga yako akakupasukia, akakuzodoa, kwamba "wach iti" wanaume hawalazimishwi, wanabembeleeeezwa taaaratibu!

Pepo mchafu akakuchochea, ukabwabwaja, kwamba waonewa wivu! Mara, shogako hakutakii mema, ukamnanga na kumchafua! Haikutosha ukamvizia usiku akienda kwake, ukiwa umebeba mawe kama selasini hivi, ukamrushia! Lengo umkomeshe! Kwa bahati shogako akatenguka kiwiko na goti.....

Hapo umepewa kideti kabisa, kwamba ujiandae kupokea booooonge la sapraiz, ambalo ni "wini wini" kwenu wawili! Basi bichwa limekujaa! Umeshakusanya matarumbeta, kukuimbia! Paukwa, pakawa, siku ikafika....
Pati si pati, kisherehe cha kimagumashi kikaanza! Nawe kwe umbea ukaanza kukirusha laivu fesbuk.... Muda ukafika, mwanaume amekuja mikono nyuma! Kashika dubwasha humo...ukajua leoooooooo, watakukoma!

Mwanaume akakusogelea! Mapigo ya moyo "kuchu! Kuchu! Kuchu" unajua umemuweza!
Mwanaume akapiga goti! Kabla hajaanza kusema kitu ukajibu "YEEEEEEEEES! Akafungua boksi! Ndani kuna KALAMU aina ya BIC! na ujumbe unaosema "UTUMIAPO KALAMU HII MKUMBUKE MHENGA ALIYESEMA "MALI BILA DAFTARI HUISHIA BILA HABARI"

Hapo ushuzi wa huzuni na kuchanganyikiwa utakuhusu!
Ndo ivo

©Bibi Happy J.
 
Na hili jambo ndilo linamuumiza JPM. Kukimbilia kila kitu kwenye media. Ikienda kinyume inakuwa aibu sana. Hata good faith ilikuja kumpooza mkuu kwa jinsi alivyoaminisha watanzania
 
Nahahhaahaa aina hii ya uandishi nimeikubali kama si OKWI BOBAN SUNZU nisingeelewa lolote
 
Dah! Kwa hiyo huyo "demu" kwa aibu akaachia "ushuzi wa ngomani"!? Huzuni sana! Ila nimecheka sana sehemu uliyoandika eti" akapost jinsi anavyo detiwa fesibuku "! Hakujiua?
 
Fasihi, kila na tafsiri take. Kwangu ni msichana maarufu kachumbiwa, lakini wazazi wa mwanaume bado hawajiridhia na kijana hataki kuwaudhi, binti katangaza ndoa, marafiki zake wanapa support mchumba hataki kuweka wazi juu msimamo wa wazazi wake.
 
Back
Top Bottom