Pesa zinazobanwa zipo wapi?

Njaro

JF-Expert Member
Mar 19, 2016
356
786
Tangu Rais Magufuli aingie madarakani ametilia mkazo mno suala la ukusanyaji kodi na kuziba mianya ya upotevu wa kodi hadi kufikia hatua pesa za kiujanja janja kupotea mitaani na pesa zote kufika Serikalini moja kwa moja.

Kitendo cha pesa kwenda Serikalini moja kwa moja na kupotea mitaani baadhi ya Watu wamekuwa wakihoji Rais Magufuli kukumbatia pesa zote bila ya Wananchi kunufaika. Hiyo ni hoja nyepesi endapo utatazama majukumu ya Serikali na kipi ambacho Serikali imeshakifanya mpaka sasa.

Twende pamoja, Serikali ya JPM imetekeleza ahadi ya kutoa elimu bure kuanzia ngazi ya shule ya Msingi mpaka kidato cha nne ambapo kwa mwezi mmoja tu unagharimu zaidi ya Tsh. bilioni 18.77, mabilioni ya pesa yamekuwa yakitumika kutoa elimu bure tu. Watoto wetu (Mimi, wewe na yule) wamekuwa sehemu ya kunufaika na elimu bure pamoja na kukalia madawati mapya na si tena kukaa sakafuni. Hayo ndio tu manufaa ya kodi zinazokusanywa na baadhi ya watu kusema JPM anakumbatia pesa.

Serikali ya Rais Magufuli inajenga barabara (zikiwemo za flyovers zilizoanza kujengwa), madaraja pamoja na kununua vivuko ambavyo vinatusaidia sisi wananchi kwenye usafiri na usafirishaji wa mizigo. Ujenzi huu wa miundombinu umekuwa ukitumia mabilioni ya pesa ambazo JPM amekuwa akizikusanya kupitia kodi.

Serikali ya JPM imenunua ndege 2 mpya ambapo mabilioni ya pesa zimetumika kununua ndege hizo ambazo zitakuwa mkombozi wa usafiri wa anga kwa bei nafuu na makusanyo ya kodi yataelekezwa kutoa huduma kwa jamii. Hapa kuanzia matajiri mpaka maskini watakuwa wanufaika wa ndege hizi.

Sio tu ndege bali hata upande wa usafiri wa reli umeimarishwa ambapo Serikali ya Magufuli imenunua vichwa na mabehewa ya treni mapya kabisa na hivyo kufufua usafiri wa treni ya kati ya Dar - Kigoma ambao ni kimbilio kwa watu wa kipato cha kati na cha chini. Tutasemaje hatunufaiki na makusanyo ya kodi zinazoenda Serikalini?

JPM amekuwa akilipa mishahara ya watumishi wa umma pamoja na kutoa pesa za uendeshaji wa shughuli za kiserikali. Mishahara hiyo inayolipwa kwa watumishi ndiyo inayowasaidia wafanyakazi hao na familia kuendesha maisha. Tutasemaje pesa hatuzioni wakati mishahara inalipwa?

Serikali imeendelea na ulipaji wa madeni ya ndani na nje. BoT imeanza kulipa madeni yote ya ndani na nje kwa fedha zake za ndani ambapo tayari imeshalipa kiasi cha Sh bilioni 96 za deni la ndani huku ikilipa dola za Kimarekani milioni 90 (sawa na Sh bilioni 190) za deni lake la nje.

Serikali hii inatumia mabilioni ya pesa kununua madawa, mashine, vitanda na vifaa tiba kwenye mahospitali ambapo leo hii suala la huduma za kiafya zimekuwa bora zaidi. Tutasemaje kodi inayokusanywa na Serikali haina manufaa kwa Wananchi?

Ndugu zangu, tumeona baadhi tu ya mifano ya Mabilioni ya pesa yanavyotumika na Serikali, tutasemaje JPM anakumbatia pesa?

Shilatu E.J
 
Hoja dhaifu ndo hizo za hapo juu manake mnashindwa kufahamu kwamba uchumi una pande mbili, macroeconomic and microeconomic! Uchumi bora kama sio endelevu ni ule ambao kuna better macro- and microeconomic policies! Uchumi bora ni ule unaozingatia the growth of both, macroeconomic and microeconomic sectors!

Utawala wa JPM ume-impose TIGHT macroeconomic policy kiasi cha ku-affect microeconomic part of the economy! Hakuna mwenye akili timamu anayeweza kupinga harakati za JPM katika kuhahakisha kila anayepaswa kulipa kodi basi alipe kodi ili hatimae serikali iweze kutoa public services kwa wananchi wake! Na kwa hili NAMPONGEZA SANA!

Lakini ikiwa katika kuhakikisha watu wanalipa kodi kunaathiri miserably the development of microeconomic sector basi hapo LAZIMA kutakuwa na tatizo kwa sababu, hakuna inversely proportionality kati ya ukuaji wa macroeconomic and microeconomic sectors... maana yake ni kwamba; si kwamba, unavyo-impose better macroeconomic practice, automatically microeconomic sector inaathirika... HELL NO! Ukiona hilo linatokea basi maana yake ni MOJA TU... kuna tatizo mahali na hili sio la kujivunia!

Ni kweli, serikali inapokusanya kodi inaweza kutoa huduma za elimu! REMEMBER, hiyo elimu inatakiwa kutolewa kwa wanafunzi walioshiba! Majority ya hawa hawatapata shibe yao kutokana na better macroeconomic policy bali better microeconomic policy!

Itoshe tu kusema kwamba, uchumi unajengwa kwa ajili ya watu na si vinginevyo! Kusanya hata Trilion 1000 kwa mwezi. Lakini ikiwa bado majority ya wananchi wako hawana uhakika wa kesho; basi Trillion 1000 hiyo ni upuuzi mtupu kwa mwananchi ukilinganisha na makusanayo Billion 1 yanayompa uhakika wa kesho! Hata ukijenga barabara za vioo wakati sina uwezo hata wa kununua baiskeli; barabara hiyo nayo itakuwa ni upuuzi mwingine kupata kutokea duniani! Hata kama shule zetu zitajaa walimu kutoka Harvard lakini watoto wakirudi nyumbani wanalala njaa; basi walimu hao nao itakuwa ni moja ya upuuzi mwingine! Hata kama hadi shule za msingi zitakuwa na viyoyozi hadi chooni wakati watoto wanaenda shule bila viatu; basi viyoyozi hivyo vitakuwa ni upuuzi mwingine! Upuuzi huo utakosa nafasi endapo tu kutakuwa na better microeconomic policy kwa sababu ndiyo inayotoa ugali wa walio wengi!
 
Kuna kahoja kanatumiwa kujikinga na awamu hii ya 5. Eti wanaolalamika ni wale waliokuwa wanaishi maisha ya malaika wakitumia mamilioni.

Nafikiri haka kahoja kanawafaa zaidi kujitetea kuliko mrundikano wa hoja zisizokuwa na mashiko. Over
 
Ahsante Mungu... nimeweza kujizuia kutoa lugha ya hovyo manake ukweli ni kwamba, hakuna "hoja" inayokera kama hiyo! And trust me, hiyo hoja inatolewa na wale wenzangu mimi... kichwani hamna kitu zaidi ya kukariri kila kinachosemwa na wanasiasa wao!
 
Hoja ya kusema kuwa eti wanaolalamika maisha magumu ni wale waliokuwa wakipiga madili,ni kichaka cha kujifichia,maana hata walimu wasiokuwa na posho zozote wanalalamika,watumushi wengi wanalalamika,watu wa mitaani wanalalamika,serikali irudishe ajira,iwape watumishi stahiki zao,maana wanasema wamepanda vyeo lakini serikali imewabania,nyongeza ya mshahara piaimewabania japo hii si ya lazima.irekebishe hayo ione kama kutakuwa na malalamiko.
 
Shilatu wabheja sana, endelea kutetea lakini hata wewe rohoni kwako unakiri kuwa tunaisoma namba
 
Hoja ya kusema kuwa eti wanaolalamika maisha magumu ni wale waliokuwa wakipiga madili,ni kichaka cha kujifichia,maana hata walimu wasiokuwa na posho zozote wanalalamika,watumushi wengi wanalalamika,watu wa mitaani wanalalamika,serikali irudishe ajira,iwape watumishi stahiki zao,maana wanasema wamepanda vyeo lakini serikali imewabania,nyongeza ya mshahara piaimewabania japo hii si ya lazima.irekebishe hayo ione kama kutakuwa na malalamiko.
Kuna siku hapa niliuliza ikiwa wale waliopiga pesa za Escrow nao ni sehemu ya wanaolalamika! Niliuliza hapa ikiwa wale waliotorosha makontena badarini ni miongoni mwa watu wanaolalamika! Nilihoji hapa ikiwa watoto wa Masamaki, yule Kamishina wa TRA ni moja ya vijana waliopo hapa JF wakilalamika ugumu wa maisha!! Niliuliza na kuuuliza na kuuliza lakini sikupata jibu na wala haielekei nitakuja kupata jibu! Siku hizi hata huko serikalini watu wanaiba na wanawekeza kwa sababu hizi si enzi za Nyerere za kwamba mtu ataulizwa "amepata wapi pesa alizonunua daladala 10!" Sasa mtu ambae kaiba sana na akawekeza sijui atalalamika nini zaidi ya kwamba wanaolalamika ni wale masikini wenzetu ambao ni tusi kubwa kusema walikuwa wanaishi kwa kupiga madili.
 
Mleta uzi ni waziri ktk serikali hii mbovu au ni JPM mwenyewe, raia wa kawaida ni vigumu kuandika hayo yaliyo andikwa inatia ukakasi.
Maana hayo na mengine zaidi ya hayo enzi za JK yalifanywa na hali mtaani aikuwa hivi, embu fikiri enzi ya awamu ya nne mtu kuchukua bill 1 lilikuwa jambo la kawaida na maisha yalikuwa kawaida lakini kwa mwendo wa awamu hii ukichukua hiyo bill 1 Tanzania yote inatikisika.
 
Wanabody habari?? Kuna swali ninalojiuliza na sipati jibu,labda wengine mnajua ..hivi raisi wetu Magufuli anapeleka wapi hela? Maana anabana matumizi na kuwakamua vilivyo mafisadi ila huku mtaani huu ni mwaka wa pili tangu aingie madarakani hela haipo,hapo sijaongelea kuhusu mikopo ya wanafunzi,na ajira..yaani ni sawa na mtu ambaye anafanya kazi kwa bidii ,kila siku anaamka asubuhi mapema na kurudi usiku sana,hana matumizi makubwa ya pesa,hali vizuri,havai vizuri na hana hata nyumba na wala hana ujenzi wowote wala majukumu ya aina yoyote lakini mtu huyo anakuwa hana hela.hapo ndipo watu tunapojiuliza je raisi Magufuli pesa anapeleka wapi ??mbona hana matumizi mabaya lakini kwa nini hazionekani huku mtaani?? Wengine sisi tunafanya biashara zetu za halali kabisa tangu miaka yote,lakini sasa mambo yamekuwa tofauti,je tatizo nini? Anapeleka wapi hela?
 
Hiyo hali jibu lake ni rahisi kwamba kama huna hela ww ulikuwa mpiga deal!!
 
1. Ananunua Bombardiers
2. Anajenga uwanja wa ndege Chato
3. Ametenga fungu kwa ajili ya kuwanunua madiwani na wabunge wa upinzani watakaofika bei
4.Atamnunulia kila mtanzania Noah yake kutokana na pesa ya makinikia

Unaweza nawe ukaongezea unayoyajua
 
Hoja dhaifu ndo hizo za hapo juu manake mnashindwa kufahamu kwamba uchumi una pande mbili, macroeconomic and microeconomic! Uchumi bora kama sio endelevu ni ule ambao kuna better macro- and microeconomic policies! Uchumi bora ni ule unaozingatia the growth of both, macroeconomic and microeconomic sectors!

Utawala wa JPM ume-impose TIGHT macroeconomic policy kiasi cha ku-affect microeconomic part of the economy! Hakuna mwenye akili timamu anayeweza kupinga harakati za JPM katika kuhahakisha kila anayepaswa kulipa kodi basi alipe kodi ili hatimae serikali iweze kutoa public services kwa wananchi wake! Na kwa hili NAMPONGEZA SANA!

Lakini ikiwa katika kuhakikisha watu wanalipa kodi kunaathiri miserably the development of microeconomic sector basi hapo LAZIMA kutakuwa na tatizo kwa sababu, hakuna inversely proportionality kati ya ukuaji wa macroeconomic and microeconomic sectors... maana yake ni kwamba; si kwamba, unavyo-impose better macroeconomic practice, automatically microeconomic sector inaathirika... HELL NO! Ukiona hilo linatokea basi maana yake ni MOJA TU... kuna tatizo mahali na hili sio la kujivunia!

Ni kweli, serikali inapokusanya kodi inaweza kutoa huduma za elimu! REMEMBER, hiyo elimu inatakiwa kutolewa kwa wanafunzi walioshiba! Majority ya hawa hawatapata shibe yao kutokana na better macroeconomic policy bali better microeconomic policy!

Itoshe tu kusema kwamba, uchumi unajengwa kwa ajili ya watu na si vinginevyo! Kusanya hata Trilion 1000 kwa mwezi. Lakini ikiwa bado majority ya wananchi wako hawana uhakika wa kesho; basi Trillion 1000 hiyo ni upuuzi mtupu kwa mwananchi ukilinganisha na makusanayo Billion 1 yanayompa uhakika wa kesho! Hata ukijenga barabara za vioo wakati sina uwezo hata wa kununua baiskeli; barabara hiyo nayo itakuwa ni upuuzi mwingine kupata kutokea duniani! Hata kama shule zetu zitajaa walimu kutoka Harvard lakini watoto wakirudi nyumbani wanalala njaa; basi walimu hao nao itakuwa ni moja ya upuuzi mwingine! Hata kama hadi shule za msingi zitakuwa na viyoyozi hadi chooni wakati watoto wanaenda shule bila viatu; basi viyoyozi hivyo vitakuwa ni upuuzi mwingine! Upuuzi huo utakosa nafasi endapo tu kutakuwa na better microeconomic policy kwa sababu ndiyo inayotoa ugali wa walio wengi!

Je unajua kuwa katika nchi zilizokufundisha uchumi wa kukariri kama huo uliojitahidi kutaka kelezea 20% ya raia wake wanamiliki 80% ya uchumi wa nchi yao? maana yake 80% ya raia wa nchi hizo wanagombea 20% ya uchumi huo.

Je unajua ni kwa nini ulipofundishwa uchumi ulifundishwa kitu kinaitwa Payback Period,mlifundishwa ili muelewa nini? Nitakukumbusha kwa lugha rahisi.Gharama ya kulima mchicha ni ndogo kuliko gharama ya kuzalisha kahawa kwa ukubwa wa eneo linalofanana ukubwa( ceteris paribus),lakini mapato na uhimili wa kahawa ni kubwa zaidi ya mapato na uhimili wa mchicha.

Jikumbushe the vicious cycle of povety inatufundisha nini? mtazamo wako kuhusu maamuzi ya serikali yanaashiria mtazamo wa uchumi wako na familia yako.Kama unafurahia mbwe mbwe za leo bila kuangalia kesho itakuwaje utarithisha tabia ya kulalamika kwa wanao na wana wa wanao.Kesho yako inajengwa leo.
 
Kaongea ukweli kiasi fulani. Kuna Mh.mmoja UK ashawahi ongea.
Houses are for people and not people for houses. Likewise, real development is 'people development'
 
Ziko zimebanwa

Hakuna fedha zilizobanwa,zinatumika kwa faida ya kesho wataka mbwe mbwe za leo leo hawazioni zilipo,si jambo jipya.Hata katika familia zetu kuna wanaotaka vizuri leo,kuvaa vizuri leo,kutembelea maeneo mazuri leo,kesho haiwahangaishi.Wapo tayari kuahirisha hata elimu kwa watoto wao ili wafanye mbwe mbwe na mikogo leo kesho ikifika waandelee kulia,serikali haitusaidii.
 
Kitendo cha serekali kumiliki pesa maana yake ni kuwa in a long run uchumi utakuwa mbaya sana kwani kutakuwa hakuna mzunguko wa pesa.Nchi zilizoendelea zilowawezesha wananchi kuwekeza kwa wingi kwenye secta ndogo mpaka zile kubwa kwa kulinda uzalishaji wao pamaja na uwekezaji.Nimeona nchi kama Marekani kama kampuni wanaona inafilisika wanakulazimisha ama kuuza share au wana uza wenyewe .Ukikataa wanafanya hostile takeover.Na serekali inabaki kusimamia policies tu na kuzitunga na kukusanya kodi.Tanzania basi sasa ni kinyume cha kila kitu ukiuloza WAPIGAJI sasa mnataka mfanye wenyewe kila kitu.Hihi ni dalili ya serekali ku anguka kiuchumi.Mwakani hakuna rangi mtaacha kuona.Mark my words.
 
Dada yangu nchi kubwa zimegawa kiasi gani kwa watu wake? uwekezaji wa miundo mbinu ya Marekani imetumia miaka mingapi? tunatamani barabara nzuri,umeme wa uhakika,magari mazuri yanayotengenezwa kwetu kama Marekani ila gharama za muda,fedha,maarifa na uvumilivu wao hatutaki kuiga.Pitia historia ya matajiri wa awali wa Marekani ujue ni wangapi walipita njia ngumu kuliko tunayopita hawakulalamika hadi wakazifikia ndoto zao.

Serikali haimiliki fedha inakusanya kodi na kuboresha miundo mbinu na huduma za jamii.
 
Je unajua kuwa katika nchi zilizokufundisha uchumi wa kukariri kama huo uliojitahidi kutaka kelezea 20% ya raia wake wanamiliki 80% ya uchumi wa nchi yao? maana yake 80% ya raia wa nchi hizo wanagombea 20% ya uchumi huo.

Je unajua ni kwa nini ulipofundishwa uchumi ulifundishwa kitu kinaitwa Payback Period,mlifundishwa ili muelewa nini? Nitakukumbusha kwa lugha rahisi.Gharama ya kulima mchicha ni ndogo kuliko gharama ya kuzalisha kahawa kwa ukubwa wa eneo linalofanana ukubwa( ceteris paribus),lakini mapato na uhimili wa kahawa ni kubwa zaidi ya mapato na uhimili wa mchicha.

Jikumbushe the vicious cycle of povety inatufundisha nini? mtazamo wako kuhusu maamuzi ya serikali yanaashiria mtazamo wa uchumi wako na familia yako.Kama unafurahia mbwe mbwe za leo bila kuangalia kesho itakuwaje utarithisha tabia ya kulalamika kwa wanao na wana wa wanao.Kesho yako inajengwa leo.
Kama hufahamu effects za kuibana microeconomic sector basi unaonesha wazi hujui lolote kuhusu uchumi zaidi ya kukariri economic terminologies!! Na ndo maana pia haishangazi kuona umeishia kuuliza maswali badala ya kuweka hoja mezani au ku-challenge hoja kwa hoja!
 
Dada yangu nchi kubwa zimegawa kiasi gani kwa watu wake? uwekezaji wa miundo mbinu ya Marekani imetumia miaka mingapi? tunatamani barabara nzuri,umeme wa uhakika,magari mazuri yanayotengenezwa kwetu kama Marekani ila gharama za muda,fedha,maarifa na uvumilivu wao hatutaki kuiga.Pitia historia ya matajiri wa awali wa Marekani ujue ni wangapi walipita njia ngumu kuliko tunayopita hawakulalamika hadi wakazifikia ndoto zao.

Serikali haimiliki fedha inakusanya kodi na kuboresha miundo mbinu na huduma za jamii.
Maisha ya sasa si ya kupitia njia ngumu hata kidogo.Haina maana mimi niliyesoma kijijini miaka ya 80 natembea kilometa 5 basi leo na mimi mtoto wangu au mjukuu aende hivyo hivyo.Unajifunza kutoka kwa waliofanikiwa huo ndio msemo wetu kule uchagani.Sasa serekali inajenga barabara wenyewe,majengo wenyewe nk unafikiri secta ninafsi zitakuwa lini.Leo BOT ndio inawalipa watumishi wa umma kweli hiyo ndio kazi ya benki kuu?haya bwana yangu macho na masikio.Uzuri post hizi hazifutwi
 
Back
Top Bottom