Pesa Zinapozidi, Matumizi Mengine Huwa ni kama Kufuru | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Pesa Zinapozidi, Matumizi Mengine Huwa ni kama Kufuru

Discussion in 'Celebrities Forum' started by MziziMkavu, Aug 26, 2009.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Aug 26, 2009
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,616
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  Sultan wa Brunei alitumia zaidi ya Tsh. Milioni 30 kwaajili ya kukata nywele zake Monday, August 24, 2009 8:14 AM
  Wakati wengine wakihaha usiku na mchana kutafuta pesa za kununulia hata unga wa ugali, upande mwingine wa dunia watu wenye fedha kama huyu Sultan wa Brunei wanatafuta njia za kuyatumia mabilioni yao. Sultan wa Brunei alitumia zaidi ya Tsh. Milioni 30 kwaajili ya kukata nywele zake tu. Wakati kwa kawaida kukata nywele katika saluni mbali mbali duniani huwa ni wastani wa tsh. 5,000 hadi 20,000 na pengine pungufu zaidi ya hapo, Sultan wa Brunei alitumia jumla ya paundi 15,000 (Zaidi ya Tsh. Milioni 30) ili kukata nywele zake tu.

  Sultan wa Brunei ni miongoni mwa watu matajiri sana wa dunia, utajiri wake ukikisiwa kuwa zaidi ya dola bilioni 30.

  Sultan wa Brunei alikodisha siti maalumu kwenye ndege ya Singapore Airlines kwaajili ya kinyozi Ken Modestou wa nchini Uingereza ili aende mpaka Brunei kwaajili ya kumkata nywele zake tu.

  Ken anaendesha saluni yake ya kukata nywele katika mitaa ya katikati ya jiji la London akiwachaji wateja wake pesa ambazo ni sawa na Tsh. elfu 60 kwa kukata nywele zao.

  Mbali na kukodishiwa ndege, Ken aliandaliwa hoteli maalumu kwaajili ya makazi yake ya siku chache nchini Brunei na alilipwa maelfu ya dola kwaajili ya kumkata nywele zake.

  Katika ndege hiyo aliyoandaliwa, sultan wa Brunei aliagiza kuwa kinyozi wake atenganishwe na abiria wengine ili kumuepusha na ugonjwa wa mafua ya nguruwe.

  Ken inasemekana amekuwa akimkata sultan wa Brunei nywele zake kwa miaka 16 sasa, wakati mwingine akienda Brunei kila baada ya wiki tatu au nne, liliripoti gazeti la Sunday Times la Uingereza.

  Gharama hizo za kukata nywele za mtu mmoja tu ziliibuliwa kwenye magazeti baada ya saluni moja ya kukata nywele jijini Manchester kuanza kukata watu nywele kwa kuwalipisha paundi 2.5 tu.

  Mbali na kuwachaji wateja wao kiasi hicho kidogo cha fedha, saluni hiyo pia huwagawia wateja wake bia za bure, chai na kahawa.
   
Loading...