Pesa Zilizotolewa na NMB zitavyoshindwa Kuwafikia walengwa Kanda ya Ziwa, masharti magumu bado pia kikwazo kikuu

mgt software

JF-Expert Member
Nov 1, 2010
13,767
7,115
Wana Jf

Baada ya kusikiliza video inayotrend kwenye mitandao mbalimbali ikionyesha umahiri wa benk ya NMB kuwa mkombozi kwa wanyonge kufuatia benk hiyo iliyovyojipambanua kwa kugusa kila seksheni ili kuwapata walengwa sahihi,kuanzia mdogo hadi mkulima mkubwa.

Benki hii inaweza kuzua vichekesho na ikajikuta inaangukia mikononi mwa wajanja wanaojua jinsi ya kucheza na akili za wakopeshaji,hivyo walengwa wakakosa.

Nilitembelea benk za NMB matawi mbali mbali kuulizia uhalisia wa mkopo huu pamoja na kujua vigezo na mashart. Bado nikakuta NMB wanamtegemea sana mkuu wa idara ambaye ndiye ana utaalam na mambo ya kilimo ambaye wanasema anatoka kanda kuu mwanza kuja kukagua na kuridhia nani akopeshwe!. Kutokana na mazingira ya kila sehemu na zao lake, wapo watakaokosa mikopo japokuwa wanauwezo wa kulipa.

Wapo wataokosa kutokana na location ya mteja alipo. Wakulima wengi hufuata sehemu iliyo na rutuba au mazao yanapokubali. Kwa kumtegemea meneja mmoja kutoka kanda ya ziwa.

Huenda tukatengeneza mianya ya rushwa ya upendeleo kwa wakopeshwaji. Lakini pia kutokana na wingi wa waomba mikopo uenda sehemu nyingi asifike. Na kutona na mazao kwenda na msimu meneja huyu huenda akawachelewesha wahitaji wa mikopo hii wakapitwa na majira.

Bado kuna tatizo la mashart magumu kwa wanaokopeshwa, hivyo kumwinua mkulima wa kawaida itabaki story tu.

Rai yangu kwa NMB kama inataka kusaidia nchi hii na kauli mbiu kazi iendelee, aina budi kuongeza group la wataalum kuhudumu kadhia hii.
 
Back
Top Bottom