PEsa ZA MFUKO WA JIMBO!!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

PEsa ZA MFUKO WA JIMBO!!!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by mizambwa, Apr 24, 2012.

 1. mizambwa

  mizambwa JF-Expert Member

  #1
  Apr 24, 2012
  Joined: Oct 8, 2008
  Messages: 4,409
  Likes Received: 569
  Trophy Points: 280
  Ndugu Wabunge wa Bunge la JF;

  Mimi binafsi huwa nashindwa kuelewa kuhusu MFUKO WA JIMBO, ambao kwa maelezo ni kwamba kila Jimbo la Uchaguzi kuna mfuko kwa ajili ya shughuli za maendeleo ya Jimbo husika. Kipindi cha Kampeni mwaka 2010 ulikuwa ndio kauli mbiu ya Wagombea wengi kuwa "Wakichaguliwa watasimamia mfuko huu ili ufanye kazi" walienda mbali zaidi kwa kusema kuwa "Ni pesa nyingi sana Serikali inatoa katika Mfuko wa Jimbo na wajanja wachache wanakula hizo pesa, hivyo tuwachague ili wakazisimamie"

  Ni mwaka mmoja na nusu sasa toka tufanye uchaguzi; na baadhi wale wale waliokuwa wanasema haya maneno wapo madarakani, lakini sijajua au kupata tetesi zozote kuhusu ule wimbo wa "MFUKO WA JIMBO" maana umekuwa kimya.

  Je, Wabunge JF, kuna anayeelewa kuhusu Mfuko wa Jimbo au mfano ni Majimbo yepi yanayonufaka na mfuko wa Jimbo??? NAOMBA ANIJUZE TAFADHARI!!!  MIZAMBWA
  NABII MTARAJIWA!!!
   
Loading...