Pesa za Mashabiki Simba vs Yanga zilizolipwa machi ya leo,Serikali izichukue

Chukwu emeka

JF-Expert Member
Jan 12, 2018
15,830
2,000
Kufuatia sintofahamu ya mechi ya Simba kuahirishwa na Bodi ya Ligi, nashauri hela zote zilizokusanywa zichukuliwe na Serikali na ziwekwe kwenye budget ya huduma za kijamii. Kuwaachia hela hizo TFF na matapeli wenzao ni wizi wa waziwazi kabisa.

Karia juzi tu ulisisitiza kanuni hazifuatwi, ndiyo maana unawafungia baadhi ya Viongozi, ingependeza nawewe ukajiuzulu maana taasisi yako imeshindwa kufuata kanuni, pia waziri Bashungwa ingekupendeza ukapumzika

Meck Mexime apewe ulinzi, maana alisema juzi tu wakati anatambulishwa na viongozi wa Cambiaso sports kuwa viongozi wengi wa mpira ni WAJINGA WAJINGA TU......Hata week haijPita imedhihirika.

Mpira wetu haupo serious kabisa, ndiyo maana sponsor's wamekuwa wachache, unaahirisha mechi kienyeji tu, hata walio na haki ya kurusha matangazo, Azam Tv 📺 ,sijui mikataba yao ipoje, maana wanapelekeshwa pelekeshwa tu......

Tukiacha ujinga aliousema Mecky tutasonga mbele
FB_IMG_1620496055696.jpg
 

NAWATAFUNA

JF-Expert Member
Nov 14, 2019
10,949
2,000
Mashabiki wa timu zote susieni kwenda viwanjani huu ni upumbavu.
Labda kwa Uto kama ikiwapendeza,lakini kwa Simba ambae ubingwa unamnukia sidhani swala la kususia kama mashabiki wa Simba watakubali,ingawa baadhi ya mashabiki wa Simba nao wamechukizwa na haya mabadiliko ya muda.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom