Pesa za mabango kulipwa kwenye kampuni binafsi badala ya Halmashauri

Pdidy

JF-Expert Member
Nov 22, 2007
56,667
30,584
Nasema kuna vitu vingine mnaruhusu wenyewe mianya ya rushwa rushwa rushwa

Waziri wa TAMISEMI, Meya wa jiji na Rais tumeona ripoti ya CAG Halmashauri nyingi wezi sipendi tumia neno hili ama wana hati chafu. Kwakuwa uchafu hauna grade nalazimika kuita wezi.

Rais na Waziri husika sioni mantiki kwanini pesa za mabango zilipwe kwenye akaunti za kampuni binafsi na sio akaunti za Halmashauri ambazo mnaweza kujua mna mabango mangapi kila Halmashauri.

Najiuliza kwanini na leseni za biashara nazo hatukupewa akaunti za kampuni binafsi tuwawekee huko mkatujaza kwenye mafoleni.

Sioni mantiki ya kupigia kelele rushwa ya stendi ya mkoa na kwingineko kama hatujajipanga kupambana na mianya ya rushwa.

Siafiki kuruhusu mtu akalipe akaunti za kampuni binafsi kisa ameshinda zabuni.Yule atumike kusimamia tu kila bango limelipiwa na malipo yafanyike akaunti za serikali yaani za Halmashauri

Ttusiruhusu shetani aingie jamani mkimpa nafasi mtajuta huko mbele nadhani ile mikataba yote ya manispaa kama mmedhamiria kweli kukusanya pesa za Manispaa.

Wananchi waende kulipa akaunti za serikali wao wafuatilie waulizie risiti tu na sio vinginevyo

Akisema mabango wamekusanya sh kadhaa mabango yako kadhaa mtahakikije hili.Yapo mambo mengi tu ya kutoruhusu hayo.

Mkitoa zabuni mhusika awe sio mpokeaji hela za serikali akae kama msimamizi na kusimamia huyu amelipa hiyu ajalipa ama lah.

Nawatakia makusanyo mema lakini sio design hizi.
 
Mmh sio kuna mawakala wa kukusanya mapato! Ngoja nisubiri maoni na michango ya wanajamvi
 
Hivyo hiźi kampuni za auction zinamilikiwa na nani? Nilishawahi kushauri humu pesa zikusanywe na halmashauri na manispaa. Naamini wenyewe wana uwezo wakufanya hizo kazi. Hawa madalali wanapunguza pato. Kama Sasa hivi hapa Dar kuna moja imepewa kazi nyingi mpaka za TRA.
 
Sheria ya manunuzi inaluhusu kitu hiki kwa serikali kutangaza tenda ambayo wazabuni watajaza kuna fomu inaitwa MAOTEO yaani wazabuni wanaotea watatoa sh ngapi tenda husika na kumbuka wakati huo halmashauri wanakuwa na wanajua chanzo husika kina mapato ya kiasi gani na kama wazabuni watakuwa chini ya viwango wataitangaza mara ya pili hiyo tenda
 
NENA SERIKALI NZIMA IMEJAA MIANYA YAKIFISADI NDIOMAANA KABLA YAKUPIGA KELELE WAZIBE MIANYA HII

KWANINI LESENI TUSILIPE KWAO
 
Sheria ya manunuzi inaluhusu kitu hiki kwa serikali kutangaza tenda ambayo wazabuni watajaza kuna fomu inaitwa MAOTEO yaani wazabuni wanaotea watatoa sh ngapi tenda husika na kumbuka wakati huo halmashauri wanakuwa na wanajua chanzo husika kina mapato ya kiasi gani na kama wazabuni watakuwa chini ya viwango wataitangaza mara ya pili hiyo tenda
Uwezikuniambia wenye mabango yabbiashara Leo walewale wamwakajana kaka wizi huu
 
Rais analengo la kuikomoa Ukawa.

swissme
Kumbe apo nyuma. Ndio nimepata picha zilikuwa zinaingia kwy mifuko ya vyama vya siasa. Duh hatari Sana, hii nchi kama apa kata yote ya Ubungo Kuna mabango mengi sana. Wameona Ukawa watapata pesa mingi
 
Sheria ya manunuzi inaluhusu kitu hiki kwa serikali kutangaza tenda ambayo wazabuni watajaza kuna fomu inaitwa MAOTEO yaani wazabuni wanaotea watatoa sh ngapi tenda husika na kumbuka wakati huo halmashauri wanakuwa na wanajua chanzo husika kina mapato ya kiasi gani na kama wazabuni watakuwa chini ya viwango wataitangaza mara ya pili hiyo tenda
Pumbaaavuuuu huuu wazabuni wanatuchaguliaa sh ngapiii shamee
 
Uwezikuniambia wenye mabango yabbiashara Leo walewale wamwakajana kaka wizi huu
ni kweli inaweza kuwa ni walewale wazabuni lakini hapa huwa wanacheza na sheria ya manunuzi pia hakuna sheria inayosema aliepata tenda mwaka jana asipewe mwaka mwingine na pia sio lazima anaesema anatoa pesa nyingi au ndogo ndio achaguliwe
 
Hii ndiyo iliyosababisha Kabwe atumbuliwe kwani kumpata mzabuni mwingine imechukua miezi kwa kisingizio cha "mchakato unaendelea!"
 
Mimi nishagomea kulipa kodi ya mabango maana hata hizo barua wanazokuja nazo unauhakika gani ni genuine dunia ya leo mtu anaweza foji hadi mihuri. Kibaya zaidi mtu anataka umlipe pesa mkononi huu ni wizi. Mm nishagoma nitaanza kulipa siku nikiwa nalipa kwenye ac ya serikali moja kwa moja
 
Deeson m niliwambia nangoa kesho usiku nkatoa Feb ilikuwa nan anataka shida
 
Ni wazo zuri mno.Kupiga vita hii issue ya mawakala.Bora kila mwenye Bango akalipie Bank.Kama wafanyavyo TRA
 
Rais analengo la kuikomoa Ukawa.

swissme

Sidhani.Hapa inabidi uongozi wa Halmashauri ukae chini kutafuta njia mbadala.Hili la ku-outsource halina faida kwa halmashauri.Maana sidhani kama kweli Account za Halmashauri zinafanyiwa Reconciliation.

Wafanye kama TRA kuweka dirisha kwa ajili ya mapato ya halmashauri
 
Zabuni ya mabango kwa jiji la Dar iko chini ya halmshaur na kwa kuwa ni UKAWA basi wavunje MIKATABA na hawa sijui outdoor wanapiga sana pesa
 
Watanzania bana, cjui tunatakaje. Mawakala wana faida tofauti na mnavyofikiria mawakala wanaongeza efficiency ya ukusanyaji wa mapato pia ni namna nyingine ya kuishirikisha sekta binafsi. Imagine sehemu uliyokuwa ukusanye sh 1000 ukaingia mkataba na wakala wa kukupa 800, manake wakala ataajili vijana vijana watalipa kodi, bima za afya nk pia watasaidia familia zao huko hivyo kupunguza umaskin kwa njia moja au nyingine kwa ile margin ya sh 200.

Ukisema ukusanye ww mwenyew kwanza huwezi kuleta hiyo 1000 yote sababu utaongeza manpower ambao ni waserekali ambao usimamiz wao ni mdogo hivyo pengine kujikuta unalipa watu mishahara wasiofanya kazi na mambo mengi tunayoyajua cku zote na kuyajadili humu.

Me nadhani ambacho ungesema ni kuhakikisha tenda za ukusanyaji zinakidhi vigezo wanapewa wenye sifa, na wanapewa malengo ambayo yataisaidia halmashauri kuraise hela nyingi na kuwaachia margin kidogo mawakala waendeshe ofisi.

Hivi fikirieni wale watu wa parking unadhani jiji lingeweza kuajili watu wote wale, lakin wasingekuwepo unadhani ni vijana wangapi wangekuwa hawana kaxi ya kufanya?

Hii nchi ni masikin ni lazima mipango yote tunayopanga ireflect umaskin wa watu wetu, me nadhan tungeongeza condition za mikataba ya ajira kwa wafanyakaz wa mawakala wakat wa kutoa tenda.
 
Back
Top Bottom