Pesa za korosho zitalipwa kweli?

GAZETI

JF-Expert Member
Feb 24, 2011
5,278
6,672
mimi nauliza tu, maana naona jamaa wako 'Bize' na audio za Membe na makamba.
Ina maana ndio tushaumizwa, Tatizo hata ufafanuzi wa nini wanakifanya hawautoi.
Wenzenu wana njaa, semeni chochote basi.................... hata kama mmeshindwa semeni
ili watu washukuru wajue tumemwachia Mungu maisha yaweze kuendelea.
 
Yaani hili suala linaleta ukakasi sana..
Fikiria mkulima hajalipwa, bado anahitaji pembejeo, anahitaji shamba kulimwa,pia akiangalia hata kama anakopesheka,inakuwa ngumu kwa taasisi za fedha kumkopesha kwani hawana uhakika kama mazao yake yatakuwa na mfumo gani wa kuuzwa ili wachukue chao.. akijaaliwa kupita huko kote(kwa wanaofahamu ni fedha za kutosha), atafute wavunaji, atafute usafiri wa kutoa mazao yake kuyapeleka kwake kwa ajili ya usalama(huku akisubiria msimu utakapotangazwa kuanza rasmi), na hapo abahatike kukuta ghala kuu limekwisha hamisha mazao ya msimu uliopita ambayo kwa lugha ya zamani ya mitaani yanaitwa "yaliyododa", atafute usafiri kupeleka kwenye chama chake cha msingi.
Hapo sasa asubirie majaaliwa ya mfumo gani utakaotumika.
Yaani mkulima yupo yupo tu...
Acha kabisa...
 
Bado tunatafuta Wateja, vuta subra

Juzi Mwenyekit wetu Wa Mkoa Kate Kamba hukumsikia akitafuta wateja wakati alipokaribishwa kuzungumza na Mh.Ndugu Rais?
 
mimi nauliza tu, maana naona jamaa wako 'Bize' na audio za Membe na makamba.
Ina maana ndio tushaumizwa, Tatizo hata ufafanuzi wa nini wanakifanya hawautoi.
Wenzenu wana njaa, semeni chochote basi.................... hata kama mmeshindwa semeni
ili watu washukuru wajue tumemwachia Mungu maisha yaweze kuendelea.
Wewe unatafuta kutekwa
 
Aisee wanalipa, jana nimekula mil 2 Hamdullah lakini safar bado ndefu hiyo hata nusu tani haifki
 
Shetani alipe ,wakati akiona wakulima wa korosho wanateseka huko lindi ,mtwara ,dar na pwani yeye anaona raha kishenzi mpaka anapiga na vigelegele .
 
Shetani alipe ,wakati akiona wakulima wa korosho wanateseka huko lindi ,mtwara ,dar na pwani yeye anaona raha kishenzi mpaka anapiga na vigelegele .
Akamwambia msigwa ampige na kapicha ka kupambia gazeti la yanga
Teh tehhh
 
Back
Top Bottom