Pesa za Ikulu na Kampuni za Simu katika Kampeni za CCM - HUU NI WIZI | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Pesa za Ikulu na Kampuni za Simu katika Kampeni za CCM - HUU NI WIZI

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Chapakazi, Oct 24, 2010.

 1. Chapakazi

  Chapakazi JF-Expert Member

  #1
  Oct 24, 2010
  Joined: Apr 19, 2009
  Messages: 2,881
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Wadau...niona hili lisipite bila kuwekewa msisitizo zaidi. Katika mdahalo wa ITV jana, mgombea wa Chadema na Rais mtarajiwa Dr Slaa alitamka wazi kuwa Ikulu imetoa $1.5million (DOLA MILLION MOJA NA NUSU) katika ku-print mabango ya Kikwete yaliyosambazwa nchi nzima!!!
  Na zaidi, ikatoa $48,000 nyingine katika mchanganuo huo wote wa ku-print na kusafirisha kuja nchini. Na juu ya hapo, hawajalipa USHURU wa haya mabango!

  Baada ya kusikia ivyo...nikajiuliza...ivi kweli tunaacha hii ishu iishie hapa hapa kwenye mdahalo au tufanyaje? Ivi kweli kuna mtu anayedhubutu kumtetea kikwete, huyu mhujumu wetu mkuu? Yani kuna watu wanadhubutu kwenda kwenye kampeni za MWIZI? Ningependa kuona majibu ya watu wa ccm katika hili swali. Tuweni serious, tuache siasi za kipuuzi...kama kweli Tanzania inataka kupiga hatua, ni lazima tuiondoe ccm. Yani huu ni wizi wa pesa zetu uliokithiri. Hakuna mwananchi anayetaka kodi yake itumike katika kampeni bila idhini yake. Mbali na hii, kuna scandal inayohusisha kampuni za simu. Angalia thread hii: https://www.jamiiforums.com/habari-na-hoja-mchanganyiko/79371-hujuma-nzito-ndani-ya-makampuni-ya-simu.html

  Kumbe tulikuwa tunachangia kampeni ya kikwete kisirisiri! Hii ni haki? ccm inatudhulumu katika kila sekta: mawasiliano, ikulu, madini. Ivi wataendelea kutuburuza mpaka lini? Ningeomba ukae chini ufikiria kwa ndani juu ya hizi tuhuma. Sambaza huu ujumbe kwa ndugu, jamaa, rafiki, jirani. Hatuweza kutawaliwa na wezi hata siku moja. Ukichagua mwizi, huwezi kulalamika pale atakapokuibia. Kwa hiyo jilinde na wizi, sambaza ujumbe na kapige kura.

  Maswali yangu ninayojiuliza:
  1. Bajeti ya Ikulu kwa mwaka ni kiasi gani?
  2. Msimamizi wa fedha ikulu ni nani? Ingekuwa muhimu kujua structure administration huko ikulu.
  3. Inawezekanaje Ikulu, Ofisi ya juu kabisa nchini kufanya uchafu huu?
  4. Hao wengine wote wanaogombea nafasi mbalimbali za uongozi kupitia ccm...mnawaza nini na mnaonaje juu ya hili?
  5. Kwa nini nyie mlio 'wasafi' ndani ya ccm msing'atuke na kujenga ccm mpya iliyo safi?
  6. Si lazima kutakuwa ufisadi mwingine mwingi zaidi ya huu huko Ikulu!
  7. Kwa nini WaTz tunakuwa kama punda, mnyama anayezoea kubeba mzigo bila malalamiko yoyote?

  Muda wa kuiondoa CCM ni sasa, ama sivyo utabaki kuwa mtumwa katika nchi yako. Uwe Chadema, CCM, CUF, nk....nakusihii...usimpigie kikwete kura mnapo tarehe 31 Oct. Fikiria nchi, fikiria jasho lako, fikiria watoto wako na familia yako. Tumechoka kuibiwa na kufanywa matija.

  video Slaa akiongelea kuhusu pesa za ikulu hii hapa: YouTube - Screencast by @mwanakijiji from Screenr.com

  P.S: Msisahau kuwa Rostam na Mkapa walitajwa live kuhusi na Kagoda!

  Mtanzania aliyechoka kuibiwa na ccm
   
Loading...