KakaKiiza
JF-Expert Member
- Feb 16, 2010
- 11,578
- 8,600
Tukiwa tunatoka katika Miaka 60 ya Uhuru na kuanza miaka 61 ya Uhuru, kama Taifa tuna historia katika hili taifa, moja ya historia ni kumpoteza kiongozi wajuu kitaifa kwamaana Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania!
Hili alikuwa jambo la kawaida kwani ilikuwa ni mara ya kwanza kama taifa hivyo tulihitaji ujasili wa hali ya juu sana! Lakini Mungu akatuongoza na tukaweza kuvuka na tukaka tukatuliza akili tukaisoma katiba yetu ikatwambia lazima Makamu wa Rais ndiye atashika Madaraka kwa kipindi kilichobakia!! Na makamu wa Rais alikuwa Mama Samia Suluhu hassani akasimikwa kuwa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania na leo anatuongoza kama taifa.
Lakini katika historia ya nchi hii hili lilikuwa tukio la kwanza kuongozwa na Mwanamke hata mchifu watemi hawakuwa kuongoza wanawake kama wapo walilithishwa na hawakuongoza!
Hivyo kitendo chakuwa na Rais Mwanamke ni Historia nyingine.
Historia kwa mtazamo wangu naziona hizi katika hili taifa!
Leo tupo na Rais wa Kwanza katika Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mwanamke hii ni Heshima Kubwa kwetu watanzania
Katika matukio yote niliyoyataja ni alama katika Taifa letu.
Leo kuwa na Rais Mwanamke katika Taifa letu la Tanzania kwa mara yakwanza ni heshima kubwa sana kwani kwa Afrika mashariki nadhani ni wakwanza na katika afrika atakuwa Rais wa tatu mwanamke!lazima kama watanzania tujivunie kwa hilo.Rais Samia amekuwa Rais wa kuigwa kwanza ni Rais ambaye amekuta nchi imevurugika ikiwa na chuki kiwango cha 178% lakini ameweza kushusha chuki kabisa hadi sasa tunaona maridhiano baina ya taasisi na serikali yakifanyika kiwango cha chuki kikiwa kimeisha labda kwa sasa ni 1.0% yachuki. Kwa haya yote lazima tuwe nakitu cha kuweka alama hata kizazi kijacho kikija kijue kabla ya kusoma katika vitabu kuwa tulikuwa na Rais Mwanamke!
Mimi kwa Maoni yangu na nionavyo mimi nimuombe Waziri Mwenye dhamana Mh Lameck Mwigulu Mchemba Akishirikiana na Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Prof. Florens Luogaa wapendekeze Itengenezwe pesa yenye Sura ya Rais wetu Mama Samia Suluhu Hassan kama ukumbusho wa Taifa hili la Tanzania na Afrika Mashariki na kwa Afrika.
Kwani itakumbukwa ni Rais wa (3) Mwanamke kwa Afrika. Rais wetu amefanya kazi kubwa kwa uwezo wake wakushawishi, kwani hata Jumuiya za kimataifa zinatambua mchango wake.
Hii itakuwa Heshima kwa Rais wetu na vizazi vijavyo mnaweza wanaweza kuweka katika Noti hizi:-
Noti ya 2000
Noti ya 5000
Noti ya 10000
Moja wapo ya hizi noti Rais wetu akiwepo kwani itakuwa heshima kwa watanzania na vizazi vijavyo pia.
Tusikumbatie sana mifumo ya kimagharibi maana hapa watakuja watu wakisema mbona dola au paund haijawahi kubadilishwa ule ni utamaduni wao na sisi tuendele na utamaduni wetu.
Asanteni.

- Kupata Uhuru
- Muungano wa Tanganyika na Zanzibar
- Kumpoteza Rais Serikali ya Mapinduzi Zanzibar
- Nchi kuingia katika vita na Uganda na Kuikomboa Ardhi ya Tanzania katika mikono ya Nduli Idi Amin
- Kumpoteza Rais wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania akiwa madarakani kwa mara ya kwanza tangu kuumwa taifa hili.
- Kupata Rais wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania Mwanamke kwa mara ya kwanza tangu kundwa kwa Taifa hili.