Pesa ya Uswis inachanganya akili; vitisho vilivyoanza vitafanikiwa kufifisha? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Pesa ya Uswis inachanganya akili; vitisho vilivyoanza vitafanikiwa kufifisha?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Candid Scope, Jul 12, 2012.

 1. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #1
  Jul 12, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Kwa kusoma upepo tu tangu maficho ya fedha za walipa kodi huko Uswisi kuanikwa hadharani, kuna kila dalili ya vitisho dhidi ya hasa wanaoonekana wanaweza kuvalia njua suala hilo. Kinachoendelea ni kusimama kwenye hoja dhaifu wakati nyuma ya pazia ni kuzima suala la Pesa za Uswis. Wengi wataitwa na kutishiwa kwa njia mbalimbali lakini ukweli hatimaye utajulikana. Je, nini hatua zinafanywa na serikali juu ya kufichuka kwa pesa hizo ambazo ni hazina kubwa kwa taifa na papo serikali kugeukia hoja za kutishia wenye kutaka kulindwa na vyombo vya dola wanapotishiwa uhai wao?

  Swiss stashed billions in a new twist
  [​IMG] [​IMG]
  [​IMG]

  A cabinet-ranking government official yesterday claimed that the state was very much aware of the stolen billions hidden in Swiss banks, but failed to act because of the ingrained culture of protecting the culprits—some of whom are members of the ruling clique.
   
 2. N

  Ninaweza JF-Expert Member

  #2
  Jul 12, 2012
  Joined: Dec 14, 2010
  Messages: 7,170
  Likes Received: 1,173
  Trophy Points: 280
  Hawa viwavi wetu kukanusha ni jadi yao subiri uwone.
   
 3. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #3
  Jul 12, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  [​IMG] [​IMG]

  Serikali inaelekeza nguvu kubwa sana katika kupambana na Chama cha Chadema ambacho ni mwiba mkali wakati huu ambapo mbio za uchaguzi mkuu imebakia miaka kama miwili. Licha ya kupambana na chama hivyo, pia inapambana na individuals ambao wanaonekana ndio silaha kubwa kwa chama hicho.

  Kufumuliwa kwa Pesa za mafichoni Uswis ni mkuki uliopenya hadi ndani ya maini ya walio nyuma ya pazia kuficha pesa hizo. Tukumbuke kuwa pesa katika bank kwa kawaida kuzificha nje ya nchi vigumu taasisi kufungua acount ila hutumia njia ya watu binafsi kwa makubaliano wanayojua wenyewe.

  Amini usiamini si rahisi mtu binafsi kuwa na kiasi kikubwa hicho cha pesa kwenye bank hapa nyumbani au nje ya nchi. Hizo ni pesa za serikali au chama fulani uwezekano mkubwa unaweza ila sina hakika lakini ni mtazamo wangu, kwani si rahisi mtu binafsi kuwa na kiasi kikubwa hivyo bank.
   
 4. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #4
  Jul 12, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Dr. Slaa kuanza tu kupata mwaliko wa kuhudhuria mkutano huko Ujerumani siku chache zilizopita ni mwiba mkali kwa serikali kwani ni dalili anaanza kutambuliwa kimataifa, na mizengwe ndio hiyo inaanza kwa kumwekea pingamizi la kutofunga ndoa na mchumba wake. Huyo Josephine ana shahada ya ndoa na Dr. Slaa? Mikingamo mingine hata haina chembe ya akili ndani hata mtoto mdogo anacheka kuona kuchanganyikiwa kwa kukusanya matofali yasiyochomwa kuwa eti ni blocks zilizoimarishwa kwa saruji.
   
 5. F

  FJM JF-Expert Member

  #5
  Jul 13, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Nchemba na Manyanya wanatumia nguvu kubwa sana kushambulia upinzani. Na sasa Nchemba anatamba kuwa ameshanasa mambo ya CHADEMA. Labda ni umri, maana angekuwa mtu mzima angejiuliza ni kitu gani kimemfanya Mukama akawa na bubu? Nchemba na wengine wanaokwenda kichwakichwa watajikuta 2015 imefika na bado wanapambana na scandal after scandal. Wewe uzo wa miaka 15 na ushee utaanzia wapi? Swiss itaisha yatakuja mengine!
   
 6. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #6
  Jul 13, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Na kweli kwani kila kukicha yanazuka mapya, hakuna dawa, sikio la kufa ni kupoteza nguvu kugharimia dawa.
   
 7. King2

  King2 JF-Expert Member

  #7
  Jul 13, 2012
  Joined: Nov 16, 2011
  Messages: 1,289
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Yani mizengo Pinda kwa Wassira anaonekana handsome.. Ama kweli wassira balaa tupu.
   
 8. Papizo

  Papizo JF-Expert Member

  #8
  Jul 13, 2012
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 4,611
  Likes Received: 392
  Trophy Points: 180
  Walikuwa wakina NAPE now wametulia kimya kabisa..... so CCM now haina mwelekeo kabisaaa, humo ndani kumegawanyika na siri nzito zitatoka hivi karibuni, kaeni mkao wa kula.
   
 9. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #9
  Jul 13, 2012
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,202
  Likes Received: 864
  Trophy Points: 280
  Wasitudanganye bwana, kwa kupitia msukumo wa World Bank, siku hizi mabenki yote ya uswisi yanatoa record za account za wanasiasa wa nchi zote zinazopata misaada na mikopo kutoka world bank. Utaratibu huu uliletwa na Paul Wolfowitz alipokuwa president wa world bank. Ndiyo maana pesa zote za Sanni Abacha na majenerali wote waliowahi kutawala Nigeria zilirudishwa kwenye hazina ya Nigeria. Labda hawa jamaa wa kwetu wa kwetu hawataki tu kuzirudisha pesa hizo kwa sababu zao binafsi tu; hakuna cha culture ya benki za uswiss wala nini. In fact, benki yoyote duniani leo inaruhusiwa kabisa kutoa account information za wanasiasa wote wanotoka kwenye nchi maskini zinazotegemea misaada na mikopo ya world bank.
   
 10. Richard

  Richard JF-Expert Member

  #10
  Jul 13, 2012
  Joined: Oct 23, 2006
  Messages: 8,253
  Likes Received: 4,275
  Trophy Points: 280
  Ufaransa na Ujerumani wao tayari wameanza kuwahoji maofisa wa benki kuu za nchi hizo ambao walikuwa wakishirikiana na wafanyabiashara kutoroshea fedha nchini Uswiss.

  Hio ni baada ya kuona kwamba watu wengi wenye pesa wamekuwa wanakwepa kulipa kodi katika nchi zao husika na kuzihifadhi nchini humo katika benki ikiwemo ile maarufu ya credit suisse.

  Tangu mwaka 1934 nchi ya Uswiss ilitunga sheria kuzuia utoaji wa taarifa za akaunti ambazo ni za watu wasio wananchi wa nchi hiyo ambao wamehifadhi pesa katika mabenki nchini humo kwa siri na hio ikasemwa kwamba ni siri ya serikali.

  Lakini mwezi uliopita nchi hiyo imebadili sheria hiyo kwa shinikizo la nchi za Ujerumani na Ufaransa ambazo zimeona kwamba katika kutafuta pesa ya kusaidia nchi zenye matatizo ya kiuchumi pia kuna pesa ambayo hailipiwi kodi na inahifadhiwa nchi Uswiss.

  [TABLE]
  [TR]
  [TD][​IMG]
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  Mbunguni kumehifadhiwa mabilioni ya fedha za nchi mbalimbali duniani ziliwemo shilingi
  za kitanzania bilioni zaidi ya 300

  Fedha zinazohifadhiwa nchini humo ni zile ambazo ni mapato ya milungula, zawadi na vyanzo vingine ambapo ikiwa vitagundulika vinaweza kumtia mtu hatiani kwa kuhujumu uchumi wa nchi, hupatikana kwa kubadilishana na huduma fulani, biashara katika ya nchi na nchi na utiaji saini mikataba mbalimbali kama ile ya Richmond na Buzwagi.

  Akili zitachanganyikiwa kwani hizo ndizo pesa ya uzeeni, na watu wanataka ndio watesee kama pedeshee.
   
 11. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #11
  Jul 13, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Kitu kama hicho ambacho tulikuwa tunakionea aibu change ya rada wametusaidia kwa kuwa haikuwahusu wenyewe moja kwa moja kuvujishwa, hili lina wenyewe, ndio maana makucha yamekunjuliwa sasa kwani mambo yako hadharani.
   
 12. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #12
  Jul 13, 2012
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,202
  Likes Received: 864
  Trophy Points: 280
  Na huo ndio ukweli wenyewe. Viongozi wetu wengi hawatumii akili sawasawa katika mambo yanayohusu matumbo yao ndiyo maana wataumbuka hata kama wakiweka mkwara gani. Interpol inawajua wote walioweka pesa hizo, na record zote zitatoka hadharani muda si mrefu tu. Time will tell, nadhani data hizo zitatoka ndani ye miezi sita ijayo, bila kuihusisha serikali ya Tanzania.
   
 13. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #13
  Jul 13, 2012
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,313
  Likes Received: 5,605
  Trophy Points: 280
  Aibu sijui huko ulaya kuna msitu?watawatupa wapi hao waliovujisha siri toka Swiss bank?
   
 14. KIWAVI

  KIWAVI JF-Expert Member

  #14
  Jul 13, 2012
  Joined: Jan 12, 2010
  Messages: 1,747
  Likes Received: 376
  Trophy Points: 180
  thanks kichuguu... sasa kuna uwwzekano wa kuswma cxm haihusiki?
   
 15. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #15
  Jul 13, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Thats is good news. Maana kilichonishtua na kunishangaza ukali usio wa kawaida utokao serikalini dhidi ya Chama pinzani, kwa vyo vyote ni taratibu za kinga ya pesa hizo huko.
   
 16. T

  Topical JF-Expert Member

  #16
  Jul 13, 2012
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 5,176
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Waumbuliwe hawa wanaohifadhi fedha nje badala ya ku-invest Tanzania..

  Dawa yake hata wazichukue hao waswiss..shz typ
   
 17. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #17
  Jul 13, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Pesa hizo ambazo zimechota hazina zimefichwa huko kwa ajili ya mambo ya kisiasa hasa gharama ya uchaguzi mkuu kubakisha serikali iliyopo madarakani. Ndio maana unaona wanajiumauma na kutolea makucha yote kwa Chadema kuficha ukweli.
   
 18. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #18
  Jul 13, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Yale mabilioni yaliyoko South Afrika ambayo yaliwekwa kwa jina la kigogo mmoja wa jeshi la wananchi yameishia wapi?
   
 19. WA-UKENYENGE

  WA-UKENYENGE JF-Expert Member

  #19
  Jul 13, 2012
  Joined: Oct 1, 2011
  Messages: 2,904
  Likes Received: 227
  Trophy Points: 160
  Na ndiyo janja yao ya kuweka pesa mapema ili waje wawavalishe watanzania khanga na kofia, huku wakionekana wanakubalika kumbe wizi mtupu. Hawa ni kuwapiga risasi tu tena mbele ya TV.
   
 20. T

  Topical JF-Expert Member

  #20
  Jul 13, 2012
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 5,176
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Ngoja waswiss wazitumie ndio itakula kwao.
   
Loading...