Pesa ya Magu haitaki dharau za kijinga. 2017 kila Mtanzania atakuwa na nidhamu ya pesa

Zero Hours

JF-Expert Member
Apr 1, 2011
12,944
18,652
Miaka ya nyuma kuna walioita million kadhaa kuwa ni pesa za mboga. Kuna waliokuwa wanasema laki sio pesa. Kuna waliosema elfu 10 ni kama buku tu. Sasa hii misemo mwisho ni mwaka huuu. Pesa ya magufuli haitaki dharau.

Jelo itaitwa miatano
Buku itaitwa elfu moja
Buku tano itaitwa elfu tano
Buku teni sijui msimbazi itaitwa elfu kumi.

Mpaka mshike adabu. Sasa hivi tunamaliza mchakato wa kuhamisha pesa zote za halimashauri BOT. Mkulu anataka pesa ziwe kwenye kapu moja sio kuzisambaza ovyo ili mumuibie kirahisi. Anataka akienda kununua sijui ndege pesa zinatoka kwenye kapu moja sio kuanza kukusanya kusanya sijui banki ya CRDB, mara NMB mara fixed account bank ya post!

Kuna wale wengine wanategemeaga ndugu zao wa mijini wao wapo vijijini hata hawajishugulishi na lolote na mjiandae. Mtakula pumba kama sio mawe mwaka 2017. Na ole wenu mkimbie familia zenu kama mlivyozoea mtawajibishwa.

Kundi lingine ni wale walioendaga vyuo kwa malengo ya kukaa maofisini full kiyoyozi wakisubiri mishahara mwisho wa mwezi. Sasa hivi izo ajira sahau. Kama huwezi kuwa mbunifu jiandaeni kisaikolojia.

Sio kuwa mimi nafurahia hii hali. Hapana ni vizuri kuambizana ukweli ingawa watz huwa hatupendi kuambiwa ukweli but U will thank me latter.

Wapo watakaopunguza idadi ya michepuko.
Wapo watakaotulia na wake zao
Wapo watakaokuwa wabunifu na kubuni mirija ya kuzalisha pesa.
Wapo watakaoheshimu mishahara yao.
Wapo watakaojua maana ya pesa.
Wapowatakaojua jinsi ya kufanya maamuzi sahii.
 
Ndio maana yake..
Tatizo mkuu ana roho mbaya sana hata ccm wenyewe walimpa kijiti kama ajali tu sasa hivi wanaisoma namba vile vile
Cc wakudadavua, lizzy, mudawote NA maandazi yote yanayotafunwa jf.....
Wanaendelea kujifaragua
Halafu
 
585642acdf450a64f33b209366ba2647.jpg
 
Ili uwe Mama kubali kupoteza Bikra!

Ili kutokomeza Ufisadi lazima tuondoe Fedha za Ufisadi kwny Mzunguko

Ili kuzuia Inflation tuliyokuwa tunamtukania Jakaya lazima kupunguza Fedha kwny Mzunguko na Matumizi ya Serikal
 
Huu ni mfano hai kwa wanawake, msikubali watu wenye maneno na ahadi tamu tamu na kujifanya wao ni ma mwamba na bado mpaka 2019 matajiri pekee watakaobak mjini watakua wachaga na wakinga tuu maana hawajali kuuza kiberiti, tambi za kibatari, wala mchele
 
Ili uwe Mama kubali kupoteza Bikra!

Ili kutokomeza Ufisadi lazima tuondoe Fedha za Ufisadi kwny Mzunguko

Ili kuzuia Inflation tuliyokuwa tunamtukania Jakaya lazima kupunguza Fedha kwny Mzunguko na Matumizi ya Serikal
Sidhani kama wengi wamekuelewa, ila huo ndio ukweli.
 
Back
Top Bottom