Pesa wanazokusanya friends of slaa ziko wapi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Pesa wanazokusanya friends of slaa ziko wapi?

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Gurudumu, Oct 28, 2010.

 1. Gurudumu

  Gurudumu JF-Expert Member

  #1
  Oct 28, 2010
  Joined: Feb 5, 2008
  Messages: 2,350
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Ndugu wana JF na wale ambao tumechangia kampeni kwa namna mbalimbali,

  Uamuzi wa kuchangia kampeni za Dr. Slaa na CHADEMA kwa kupitia njia mbali mbali ulikuwa mzuri sana. Hivi karibuni kuna kundi linalojiita Friends of Slaa ambalo nalo linakusanya pesa kwa njia za electronic. Nawapongeza na kuwatakia ufanisi mzuri. Hata hivyo ningependa kuuliza taarifa ya mapato na matumizi na vile walivyojipanga katika lala salama.

  1. Election materials kama bendera, kofia, T-shirts, stickers, beji za dr. slaa, n.k hazipatikani. Wakifika kwenye kampeni waliovaa ni wale tu ambao wamekuja na msafara vinginevyo kuna chache ambazo zinauzwa na tunatangaziwa ni kwa ajili ya kutunisha mfuko wa kampeni. Je, muda huu ambao watu wameshaamua si hizi materials zingegawiwa bure na kwa wingi kwa kutumia pesa ambazo zimeshakusanywa? Hatuwezi kuweka biashara pembeni ili kusaidia anguko la nguvu la CCM?

  2. Kampeni za dr. slaa tunazichungulia kwenye taarifa za habari tu. Majuzi tulimuona kwenye mdahalo ITV na live kupitia TBC1 na Agape TV. Pia alialikwa kwenye mahojiano na Clouds FM. Lakini hata hizi hazikutangazwa kwa wingi ili wananchi wengi wawe na taarifa waweze kusikiliza/kutizama. Za kwenye TV wala hazikurudiwa na CHADEMA hawajalipia marudio. Swali ni kwamba, kwanini hizi pesa ambazo zinakusanywa zisitumike kulipia vipindi vya TV na redio? Kwa nini air time isinunuliwe kwenye radio za mikoa ile ambayo anatembelea ili warushe hotuba zake live? Siyo wananchi wote wanapata nafasi ya kufika eneo analohutubia lakini wangefaidika sana kama wangeweza kumsikiliza kwenye redio au TV. Hata kulipia matangazo ya ratiba yake pia imeshindikana? Kwa mfano, siku ya Jumamosi Dr. atakapohitimisha kampeni zake huku mbeya wananchi wanaweza kutizama na kusikiliza live? Hili ni muhimu ili aweze kujibu hoja za mkutano wa JK na waandishi wa habari wa tarehe 29 October.

  Marafiki wa Dr. Slaa mnaweza kutolea haya mambo ufafanuzi. Kama maswali ya mapato na matumizi yanaweza kuwa magumu kwenu, basi tuarifuni tu mipango ya wananchi wote kupata fursa ya kusikiliza/kutazama hotuba yake ya mwisho hapo jumamosi. Mzee Mwanakijiji alikwisha tahadharisha kwamba hii hamasa iliyopo JF inahusisha watu wachache sana sana kwa hiyo tusidanganyike na ushabiki uliopo hapa tukadhani tayari tumeshashinda, ukiacha majimbo yale machache ambayo tayari tuna uhakika wa kushinda.
   
 2. K

  Kilembwe JF-Expert Member

  #2
  Oct 28, 2010
  Joined: Aug 19, 2009
  Messages: 1,132
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Hili nalo neno!
   
 3. M

  Malunde-Malundi JF-Expert Member

  #3
  Oct 28, 2010
  Joined: Jan 10, 2008
  Messages: 1,287
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Subiria Ag atatoa report; uechangia kiasi gani maana changia kwanza ndio uweze kuwa na sauti
   
 4. Kilasara

  Kilasara JF-Expert Member

  #4
  Oct 28, 2010
  Joined: Dec 21, 2008
  Messages: 578
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Ndugu Gurudumu,

  Friends of Slaa (FOS) au Supporters of Slaa (SOS = Save Our Souls) walishauriwa mwanzoni kwamba waweke michango yao katika akaunti za benki. Akaunti mojawapo ipo CRDB Bank na ni nambari 01J1080100600 kwa jina: "CHADEMA M4C". Mimi nime-deposit fedha jana ktk akaunti hii na nimethibitisha kwamba Dk. Slaa na Mwenyekiti Mbowe ndio wana-operate hiyo akaunti. Of course wengine wanaendelea kuchangia electronically.

  Kuhusu bendera na mavazi yanayotambulisha CHADEMA haya yaliagizwa mapema hata kabla ya kampeni kuanza. Vifaa vingine vya matangazo vinatengenezwa kadri fedha zinavyopatikana, I assume. Lakini fedha nyingi sana zinahitajika kwa helikopta na magari (fuel, tairi na matengenezo ya mara kwa mara), pamoja na vipindi ktk redio na TV etc. na michango ya FOS au SOS ndiyo inawezesha hayo.

  Tuendelee na ukarimu huu hadi tumwingize SLAA Ikulu na Chadema idhibiti Bunge.
   
 5. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #5
  Oct 28, 2010
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  Ungekuwa unatumia jina halali na sio bandia ningeweza kukujibu kwa undani na kukupa mawasiliano ya watu wa kuuliza kuhusu suala hilo lakini FOS Kazi yao kubwa ni kuhamasisha michango na kutoa habari zingine kuhusu mgombea uraisi lakini sio wanaomiliki hizo account za pesa ambapo hutumwa either kwa njia ya simu au kwa njia ya benki hilo ni chadema na chadema wana uongozi wao kwahiyo ufike kwa uongozi uulize swala hilo - unapouliza usisahau masuala mengine ya sheria za uchaguzi na mengine mengi
   
 6. Gurudumu

  Gurudumu JF-Expert Member

  #6
  Oct 28, 2010
  Joined: Feb 5, 2008
  Messages: 2,350
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Kilasara na shy,

  Nawashukuru sana kwa ufafanuzi. Nawashukuru pia kwa jitihada hizo za kuhamasisha michango kwa niaba ya uongozi wa chadema. Nafurahi kujua kwamba mnatumia akaunti za benki za chadema zinazosimamiwa na uongozi wa chama. Ni matumaini yangu kwamba uongozi wa chadema utanijibu maswali yangu yaliyobakia kwa mujibu wa thread yangu hapo juu.
   
 7. Gurudumu

  Gurudumu JF-Expert Member

  #7
  Oct 28, 2010
  Joined: Feb 5, 2008
  Messages: 2,350
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  jamani chadema tupeni majibu, angalau mkakati wa live coverage jumamosi
   
 8. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #8
  Oct 28, 2010
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,762
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  subiri utapewa kila kitu, we changia tuuu!
   
 9. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #9
  Oct 28, 2010
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  ndugu come out open kwa jina lako na mawasiliano yako utapewa taarifa zote kwa mtindo huu sijui utapata nini - tume ya uchaguzi ndio anayetakiwa kupatiwa taarifa hizo wewe huna mamlaka kisheria
   
 10. nguvumali

  nguvumali JF Bronze Member

  #10
  Oct 28, 2010
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 4,864
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  nazitakazo baki tutapleka kule Bagamoyo kusaidia maendeleo ya Shule hii.

  [​IMG]
   
 11. Gurudumu

  Gurudumu JF-Expert Member

  #11
  Oct 28, 2010
  Joined: Feb 5, 2008
  Messages: 2,350
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  sijui kama sasa tuko pamoja, siulizi tena mapato na matumizi nimeshawaelewa. naulizia kama mmepanga kutoa kampeni za mwisho za dr. live tuweze kumsikiliza nchi nzima kwenye redio na TV? kuchanga nimechanga

  au hilo nalo ni siri? mmezoea kutushutukiza dakika chache kutuambia kuna live coverage ama TBC au Agape, au Clouds. kutokana na kutokujua mapema kama kutakuwepo na live coverage watu wanashindwa kujipanga kusikiliza/kutazama.
   
Loading...