Pesa ni hazina ya mkuu wa anga, Jihadhari nazo

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
269,632
697,795
Mungu hahitaji mali, Mungu hahitaji ufahari. Hata sadaka tutoazo haziendi kwake Japo tunamtolea yeye. Zile pesa hubaki hapa hapa na hutumiwa na binadamu hawa hawa.

Pesa ziwapo nyingi huvutia ufuasi wa mkuu wa anga maana milki ya dunia na vyote vilivyomo kapewa yeye. Ni rahisi mno tena sana kuwa mchaji mnyofu na mwomba Mungu ukiwa kapuku tofauti kabisa na ukiwa nazo.

Utajiri hulindwa na nguvu za giza. Hili ni halisi na halikwepeki. Ni rahisi sana kumdhulumu masikini akasamehe kuliko tajiri. Tajiri yuko tayari akuue kwa pesa ambayo hata kama angeisamehe isingempunguzia chochote.

Nimeliangalia kwa tafakuri kuu suala la watuhumiwa wa uhujumu uchumi kutakiwa kurudisha pesa walizotuhumuwa nazo ili wasamehewe.

Kiroho hizi si pesa salama tena ndio maana hata wakati ule wa uhujumu uchumi mwaka 1984 ilikuwa kuna namna ya kushughulika nazo. Tayari ile ni pesa chafu ni pesa yenye maagano na makafara.

Ukitaka kuzichukua zichukue kwa tahadhari kuu, si kila arudishaye anarudisha kwa moyo mweupe.

Hao wenye hizo pesa licha ya kuzipata kwa njia haramu pengine lakini kwa vyovyote vile kwenye mchakato wa kuzipata ama kuzitunza ama kuzilinda zimemwaga damu nyingi isiyo na hatia.

Hizo pesa zimefanyiwa visomo
Hizo pesa zimenuiziwa mabaya
Hizo pesa zimefanyiwa viapo
Hizo pesa zimefanyiwa makafara

Kwamba atakayejaribu kuzikwapua kwa namna yoyote ile adhurike na kama mjuavyo makafara hayana rivasi. Hata kama atajitokeza mtu aamue kuzirudisha kwa moyo mmoja bado hazifai kwakuwa zilishanenewa umiliki usiotengulika.

Lakini mbaya zaidi kuna wanaozirudisha huku wakiwa wameziongezea sumu ya kisasi chuki na laana.

Waliotutangulia waliona mbali sana kwenye haya mambo ndio maana ukawekwa utaratibu wa kesi na mahakama, sheria na taratibu kwa hiyo inakuwa ngumu kudhuru mtu.

Tukienda mbali zaidi yalifanyika makosa makubwa sana kwa yule mtuhumiwa wa mamlaka ya mapato kupigwa picha na yale maburungutu ya manoti kama kithibitisho kuwakarudisha.

Yani mtuhumiwa kapiga selfie akionesha furaha kubwa, kwa haraka utadhani kafurahi kufutiwa mashtaka na kurudi uraiani kuungana na familia yake lakini kiuhalisia pale katangaza ushindi. Ushindi wa nini? Muda utasema.

Bado tuna nafasi ya kukwepa laana na manuizi ya pesa za uhujumu uchumi.

Kupotea/kuibiwa kwa zile computer za DPP si jambo dogo wala rahisi kama tunavyodhani.

ANGALIZO KUU ni kwamba hatuko salama kwenye hili na adui yuko kati yetu. Tena ni adui mwenye nguvu na dhamira thabiti.

Tujifunze kwenye chenchi ya radar toka Uingereza na mabilioni ya San Abacha wa Nigeria toka Uswisi. Hatukurudishiwa tasilimu. Tuliletewa vitu kwa manufaa ya jamii nzima.

Ili kama ni laana itupate sote
Ili kama ni viapo tuvipate sote
Ili kama ni mabaya tuyagawane sote.

Tusipokee mabilioni zaidi tuyaache hukohuko yaliko. Kwakuwa kama tayari watuhumiwa wako kwenye mkono wa sheria, acha sheria ichukue mkondo wake. Fedha za kinyongo sio nzuri
Kikulacho daima ki nguoni mwako.!
 
Selfika mwana wane... Ila natamani ya rohoni yangekuwa bayana..... Duniani tungekimbiana
IMG-20191017-WA0064.jpeg
 
Kama shida zikituacha labda nasi tutaacha hizo fedha!,lkn Kama mtindo ni uleule Mimi ni nani mpaka nikatae fedha..? Siku hizi si tu kikulacho ki nguoni mwako bali ki moyoni mwetu!
On serious note..!!!
Kuna pesa za fasta huwa tunazipata na kuzifanyia mambo ya kukumbukwa... Na kuna pesa za fasta tunazipata na mabalaa huanzia hapo... Si kila pesa ni safi kiroho... Nyingine ni chafu na zinanuka... Ukizichukua umeingiza uvundo kwenye milki yako unaweza ugombane mpaka ma mwandani wako
 
Kitu ambacho kimetengenezwa na mitambo,karatasi,madini n.k kina uhusiano gani na mambo ya roho..?
 
Kitu ambacho kimetengenezwa na mitambo,karatasi,madini n.k kina uhusiano gani na mambo ya roho..?
Hiyo mitambo haikujitengeneza yenyewe... Ilianza kama wazo la rohoni kisha ikaundiwa mchoro ndani ya fikra ndio ikaja implementation kwenye dunia ya macho butu

Huu uzi unahitaji "ufahamu wa juu" ili kuweza kuelewa.
Dunia na mifumo yake ya maisha imetawaliwa sana na mambo ya kiroho. Ni kama tairi ya baiskeli (mzunguko) ni ule ule.
Maamuzi rahisi na mepesi katika ulimwengu wa mwili yanaweza kuwa ni mwanzo wa matokeo angamizi katika ulimwengu wa roho. Matokea ambayo wakati mwingine hutengeneza "series of consequences" na zikakuacha bila kuelewea kosa lilifanyika wapi.

"Knowledge is power"
 
Imeandikwa ya Kaiser MPE kaiser ,mataifa ,serikali na mamlaka za dunia hii zimepata kibali cha yeye ,

Kuna wengine wanarudisha hizo fedha kwa kuonewa na hizo fedha ni hatari sana ni kwa vile tu mahakama haijawatendea haki .
 
Kuna wengine wanarudisha hizo fedha kwa kuonewa na hizo fedha ni hatari sana
 
On serious note..!!!
Kuna pesa za fasta huwa tunazipata na kuzifanyia mambo ya kukumbukwa... Na kuna pesa za fasta tunazipata na mabalaa huanzia hapo... Si kila pesa ni safi kiroho... Nyingine ni chafu na zinanuka... Ukizichukua umeingiza uvundo kwenye milki yako unaweza ugombane mpaka ma mwandani wako
Tutazijengea vyoo
 
Back
Top Bottom