Pesa na Muda

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
74,850
155,799
*PESA NA MUDA*.......
Bila shaka upo uhusiano mkubwa kati ya pesa na muda..
-Ndio maana nauli ya ndege ni kubwa kuliko ya basi, why..?
Because ndege hutumia mda mchache (mf. Ukitoma dar kwenda moshi ni saa 1na dakika 10 fast jet kwa ndege bt kwa gari ni takriban masaa 7-8)
*Linapokuja suala la MUDA NA PESA, duniani kuna makundi manne ya watu...!
1. wapo wenye muda wa kutosha bt hawana pesa mf watu wasio na kazi maalum au wa kijiweni(ukimwambia akusindikize mahali yuko tayari muda wowote)
2. wapo wenye pesa lakini hawana muda. Unaweza kumualika ktk harusi akaacha kuja lakini akakuchangia hela ya maana tu.. hili ni kundi la madirector na mameneja wa vitengo muhimu ktk makampuni.
3. wapo wasio na PESA wala MUDA.. takwimu zinaonyesha kuwa hawa ni 95% ya watu wote ulimwenguni. Hili ni kundi la wafanyakazi na vibarua ( unaweza ukamualika ktk shughuli yako na akakosa nafasi lakini pia hana hela ya kukuchangia)
Yaani mtu yuko busy 24/7 bt ukimwomba hata elfu 50,000/= hana..Why..?
Mtu huyo unakuta ana mshahara mdogo halafu ana mikopo mingi mf kakopa nyumba, gari, mtaji wa biashara ambapo kutokana na kukosa usimamizi makini napo hakuna pesa, hivyo neno MAREJESHO ndio msamiati mkuu kwao.
4 wapo watu wana PESA na MUDA wakutosha..
Ndio matajiri au watu waliofanikiwa sana. Why..?
Hawa wameandaa mfumo ambao hata wasipokuwepo pesa inaingia (mf Mengi au Bakhresa akienda likizo hata miezi mitatu bado akirudi biashara znaendelea vizuri)
Hapa unakuta yeye ndio CEO na pengine asbh yuko anawaandaa na anawapeleka wanae shule huku mm na ww ndio tunakomaa na mafoleni tukielekea kufanya kazi za kujenga ndoto za hao watu kwa masaa mengi na tunalipwa kidogo..
-Wapo watu wanasema, usipoitengeneza FUTURE yako mtu mwingine atakutengenezea kadiri atakavyoona inakufaa
AU
usipojenga ndoto zako kuna mtu atakuchukua(kukuajiri) ukajenge ndoto zake...!
JE WEWE UPO KUNDI GANI?
WASWAHILI HUSEMA, USIPOJIPANGA UTAPANGWA..
Amka na TAFAKARI sana.
 
Nimejifunza kitu muhimu, nitajilaumu kama nitabaki kusoma bila kufanyia kazi hayo uliyoandika. Ahsante kwa elimu bure.
 
Kundi la kwanza kulibafilidha ni kazi ndio wale walipoambiwa match ya yanga bure walifika saa 10 alfajiri masaa 12 kabla ya mechi

Kundi LA pili ni sisi wafanyakazi tunaenda kazini Kama utumwani bila kificho hatupati kitu kuishia kulalamika TU
Muda hatuna pesa hatuna ila uzuri kundi hili lina uwezo kubadilika
 
Ila Tanzania hauwezi kulipwa kutokana na muda...maana tuliona mkono advocates walipokua wanasimamia kesi za Tanescco walicharge $1000 kwa lisaa ikawa balaa Tanzania hapa....pia kwa mazungira yetu mfano wewe ni mpiga picha huwezi waambia watu mfano kwenye tenda ya harusi kwamba wewe utachaji 18,000 kwa lisaaa kwa kutoa huduma hio....kwa minaajili hio in Africa Time is not money hence there is no hurry in Africa....
 
*PESA NA MUDA*.......
Bila shaka upo uhusiano mkubwa kati ya pesa na muda..
-Ndio maana nauli ya ndege ni kubwa kuliko ya basi, why..?
Because ndege hutumia mda mchache (mf. Ukitoma dar kwenda moshi ni saa 1na dakika 10 fast jet kwa ndege bt kwa gari ni takriban masaa 7-8)
*Linapokuja suala la MUDA NA PESA, duniani kuna makundi manne ya watu...!
1. wapo wenye muda wa kutosha bt hawana pesa mf watu wasio na kazi maalum au wa kijiweni(ukimwambia akusindikize mahali yuko tayari muda wowote)
2. wapo wenye pesa lakini hawana muda. Unaweza kumualika ktk harusi akaacha kuja lakini akakuchangia hela ya maana tu.. hili ni kundi la madirector na mameneja wa vitengo muhimu ktk makampuni.
3. wapo wasio na PESA wala MUDA.. takwimu zinaonyesha kuwa hawa ni 95% ya watu wote ulimwenguni. Hili ni kundi la wafanyakazi na vibarua ( unaweza ukamualika ktk shughuli yako na akakosa nafasi lakini pia hana hela ya kukuchangia)
Yaani mtu yuko busy 24/7 bt ukimwomba hata elfu 50,000/= hana..Why..?
Mtu huyo unakuta ana mshahara mdogo halafu ana mikopo mingi mf kakopa nyumba, gari, mtaji wa biashara ambapo kutokana na kukosa usimamizi makini napo hakuna pesa, hivyo neno MAREJESHO ndio msamiati mkuu kwao.
4 wapo watu wana PESA na MUDA wakutosha..
Ndio matajiri au watu waliofanikiwa sana. Why..?
Hawa wameandaa mfumo ambao hata wasipokuwepo pesa inaingia (mf Mengi au Bakhresa akienda likizo hata miezi mitatu bado akirudi biashara znaendelea vizuri)
Hapa unakuta yeye ndio CEO na pengine asbh yuko anawaandaa na anawapeleka wanae shule huku mm na ww ndio tunakomaa na mafoleni tukielekea kufanya kazi za kujenga ndoto za hao watu kwa masaa mengi na tunalipwa kidogo..
-Wapo watu wanasema, usipoitengeneza FUTURE yako mtu mwingine atakutengenezea kadiri atakavyoona inakufaa
AU
usipojenga ndoto zako kuna mtu atakuchukua(kukuajiri) ukajenge ndoto zake...!
JE WEWE UPO KUNDI GANI?
WASWAHILI HUSEMA, USIPOJIPANGA UTAPANGWA..
Amka na TAFAKARI sana.
Wewe jamaa nimeipenda bure mada yako. Usipojipanga watakupanga
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom