Pesa huzima ndoto za vijana wengi mwisho wa siku wanaishi maisha ambayo si yao kabisa.

Naja naja

JF-Expert Member
Sep 13, 2016
747
1,452
Asilimia 99% ya vijana huishi maisha ambayo si yao kiundani kutokana na ukosefu wa fedha.

Pesa inaharibu future ya kijana angali mdogo kabisa na ndio maana asilimia kubwa ya mateja ,malaya ,wakabaji,wezi, wanatokea uswahilini ambapo asilimia kubwa maisha ni magumu.

Kuna kundi kubwa la vijana walikuwa wanauwezo mkubwa sana wa darasani lakini mwisho wa siku wanashindwa kutimiza ndoto zao za kielemu kutokana na ufukara unaowakabili mwisho wa siku stress zinawapelekea mpaka kuanza kutumia bangi,vilevi vikali vikali kupunguza mawazo na wakishakuja huku hapa sasa zinaibuka tabia nyingine mpya kabisa kuanzia udokozi,uwizi, umalaya kwa watoto wa kike nk.

Pesa inafanya kijana ashindwe kumudu kusoma anachokitaka mfano masomo ya sayansi mwisho wa siku anasoma kitu ambacho hakikuwa katika ndoto zake, kwa watoto wa matajiri huakikisha vijana wao wanasoma wanachokitaka hata iweje ikiwezekana hata kupeleka mtoto nje ya nchi kusoma.

Tukija upande wa biashara vijana wengi wana idea nyingi sana za biashara changamoto kubwa inakuja kwenye kupata mtaji wa kufanya hiyo biashara mwisho wa siku inabaki kuwa ndoto tu miaka nenda miaka rudi.
 
Kutengeneza mazingira mazuri kwa watoto wasizaliwe wakute mazingira ya shida sana mpaka kushindwa kufikia ndoto zao.
Lakini hata ukiweka mazingira kabla hujaitwa mzazi chochote kitatokea, muhimu kupambana na kuwalea watoto katika njia impendezayo Bwana, mimi naamini umaskini si chanzo cha maovu na maskini wa Leo ndo tajiri wa kesho, na tajiri wa Leo ndo maskini wa kesho tumeona hata kwenye biblia maisha ya Ayoub alikuwa tajiri makubwa aliamka tajiri, akashinda tajiri Lakini kabla jioni haijafika akawa amefilisika.

UMASKINI SI CHAKA LA UOVU
 
Under the current economic situation hakuna asiyelia lia wanalia hadi akina nape wazee Wa Bao LA mkono.
 
Sipendi hii kauli "SINA MTAJI AU HATUNA MTAJI". Tatizo wengi tunakimbilia kuwaza kuwa ukiwa na mamilioni ndio utaweza kufanya biashara. Ukweli ni kwamba mtaji namba moja ni: 1. Akili yako ya kuzaliwa (uwezo wa akili yako kutafakari na kujitambua wewe ni nani, unatoka wapi na unakwenda wapi na huko unakotaka kwenda utafikaje), 2. Afya na nguvu zako. (ambavyo umejaliwa na mwenyezi Mungu)

Hakuna mtu mwingine atakayekupa huo mtaji kama wewe binafsi hufanyi bidii za kuutafuta hicho kitu kinachiitwa mtaji. Utaendelea kulialia tu kwamba sina mtaji na siku zinasonga mbele.
 
Huwezi kuelewa kama hujapitia changamoto kama hiyo
 
Asilimia 99% ya vijana huishi maisha ambayo si yao kiundani kutokana na ukosefu wa fedha.

Pesa inaharibu future ya kijana angali mdogo kabisa na ndio maana asilimia kubwa ya mateja ,malaya ,wakabaji,wezi, wanatokea uswahilini ambapo asilimia kubwa maisha ni magumu.

Kuna kundi kubwa la vijana walikuwa wanauwezo mkubwa sana wa darasani lakini mwisho wa siku wanashindwa kutimiza ndoto zao za kielemu kutokana na ufukara unaowakabili mwisho wa siku stress zinawapelekea mpaka kuanza kutumia bangi,vilevi vikali vikali kupunguza mawazo na wakishakuja huku hapa sasa zinaibuka tabia nyingine mpya kabisa kuanzia udokozi,uwizi, umalaya kwa watoto wa kike nk.

Pesa inafanya kijana ashindwe kumudu kusoma anachokitaka mfano masomo ya sayansi mwisho wa siku anasoma kitu ambacho hakikuwa katika ndoto zake, kwa watoto wa matajiri huakikisha vijana wao wanasoma wanachokitaka hata iweje ikiwezekana hata kupeleka mtoto nje ya nchi kusoma.

Tukija upande wa biashara vijana wengi wana idea nyingi sana za biashara changamoto kubwa inakuja kwenye kupata mtaji wa kufanya hiyo biashara mwisho wa siku inabaki kuwa ndoto tu miaka nenda miaka rudi.
Natafuta sehemu za bata Tabora
 
Back
Top Bottom