Pesa hizi zilirudishwa na nani? au zilitoka hazina? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Pesa hizi zilirudishwa na nani? au zilitoka hazina?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by BAK, Nov 2, 2008.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Nov 2, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,586
  Likes Received: 82,136
  Trophy Points: 280
  Soo la Epa: Bilioni 17 zabwagwa benki Dar

  2008-10-31 21:21:37
  Na Mwandishi Wetu, Jijini

  Ukisikia namna ile mijamaa iliyojichotea mabilioni ya pesa kutoka Benki Kuu (BoT) kupitia Akaunti ya Malipo ya Madeni ya Nje, EPA ilivyohaha jana kurejesha pesa hizo kabla ya kipenga kupulizwa leo, walahi utadhani ni simulizi za kubuni za elfu lela ulela!

  Ilikuwa patashika nguo kuchanika kwenye mabenki. Kwa mahesabu ya haraka haraka, inadaiwa kwa jana tu, shilingi 17,000,000 zililereshwa.

  Habari za kuaminika kutoka kwa chanzo cha gazeti hili zinadai kuwa, mapesa hayo yalibwagwa benki jana alasiri na kutokana wingi wake, makarani wakayahesabu hadi usiku wa manane.

  Kwa mujibu wa taarifa ambazo Alasiri imezinyaka toka kwenye tawi la benki moja maarufu Jijini (jina linalihifadhiwa), mapesa hayo yaliyokuwa kwenye maboksi ya mbao, mengi yakiwa ya noti za alfu kumi-kumi na alfu tano.

  ``Haikuwa kazi rahisi. Noti zenyewe zilikuwa ni nyingi mno na zilifikishwa katika muda ambao tayari wengine walishachoshwa na shughuli za mchana... wakajikuta wakikesha kwa ajili ya kukamilisha zoezi hilo ambalo lilianza muda mbaya wakati benki zinakaribia kufungwa,`` kikadai chanzo chetu.

  Imedaiwa kuwa mmoja wa wahusika hao alirejesha kiasi cha shilingi bilioni 12 taslimu na mwingine akarejesha bilioni tano.

  Watu hao ni miongoni mwa waliokuwa wakitajwa tajwa kujichotea mapesa hayo.

  Imedaiwa kuwa pesa hizo zilifikishwa katika tawi la benki hiyo zikiwa katika magari mawili ambayo yalifika kwa nyakati tofauti na kupakua maboksi yaliyosheheni minoti hiyo.

  Urejeshwaji huo wa staili ya aina yake, ulifanyika zikiwa zimesalia saa chache kabla ya kufika tarehe ya mwisho aliyoitoa Rais Jakaya Kikwete kwa waliochota pesa hizo kuwa wamezirejesha.

  SOURCE: Alasiri
   
 2. K

  Kokolo JF-Expert Member

  #2
  Nov 2, 2008
  Joined: Mar 20, 2008
  Messages: 487
  Likes Received: 98
  Trophy Points: 45

  Inaamana hawa Jamaa wanatunzia pesa nyumbani! au zilitoka Benki Kuu kwa ujanja. Billion 17, sijui ni risk gani ya namna hiyo kuweka pesa zote nyumbani. au wanamabenki kwenye majumba yao yako chini ya ardhi.
   
 3. M

  Masatu JF-Expert Member

  #3
  Nov 2, 2008
  Joined: Jan 29, 2007
  Messages: 3,285
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Typical Alasiri....
   
 4. M

  Mkora JF-Expert Member

  #4
  Nov 3, 2008
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 360
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Hao walioleta hizo pesa kwanini wasikamatwe kwa makosa ya kuhujumu uchumi kuweka kiasi kikubwa cha pesa nyumbani kunasababisha Inflation ndio maana Nyerere alikuwa anabadilisha pesa na ukipeleka kiasi kikubwa cha pesa unazaa nao
   
 5. Maarifa

  Maarifa JF-Expert Member

  #5
  Nov 3, 2008
  Joined: Nov 23, 2006
  Messages: 2,880
  Likes Received: 1,050
  Trophy Points: 280
  Ingaewa wengi wanafurahia kitendo cha wezi hao kurudisha pesa hadharani, Mie bado nina maswali kibao kichwani. Who were those people? nina maana majina yao! pili je vyombo vya sheria havina ubavu wa kuwakamata hao mafisadi? Je sheri ianasemaje kuhusu kuhodhi manoti ndani au walipakuwa benki wakati mmoja?
  Je wanarusha na faida? this is ridiculous for what happened! Ni aibu tupu kwa serilaki na wal wasijitape!!
   
 6. k

  kalld Member

  #6
  Nov 3, 2008
  Joined: Jun 14, 2007
  Messages: 89
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Duhhh kweli ndio tuliwao!pesa zote hizo ziko nyumbani? na wengine kipande cha muhogo kukipata kwa siku ni mashaka!
  niko hoi bin taaban !tutafika tu!
   
 7. Zero

  Zero JF-Expert Member

  #7
  Nov 3, 2008
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 301
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  The million dollar question still remains the validity of statements issued by the government. How do we speak of monies we havent seen? Hao alasiri wanaosema 17 bilion zimerudishwa in day, mbona hawasemi nani karudisha? Mbona habari za Manji walikuwa wanaandika sana? Hizi za EPA mbona kigugumizi? Lakini cha msingi ni kwamba hatuna uhakika kama hizi hela zinarudihwa kweli. Nani anafanya ukaguzi?
   
 8. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #8
  Nov 4, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,586
  Likes Received: 82,136
  Trophy Points: 280
  Hakuna yeyote anayeweza kuthibitisha kwamba pesa hizo shilingi 69 billoni zimerudishwa. Kikwete anataka tuamini kauli yake pamoja na kuwa Watanzania hatumuamini tena. Ndiyo maana nasema sasa amekuwa dikteta anafanya mambo ndani ya serikali na CCM ili kulinda madaraka yake badala ya yale ya Watanzania. Hata mkaguzi Mkuu wa serikali hajui chochote kuhusiana na pesa zilizorudishwa. Kikwete anadai yeye anatenda utawala bora wakati mambo anayoyafanya yanaashiria udikteta. Anavunja katiba ya nchi kwa kupindisha sheria za nchi halafu anatamba kwamba utawala wake ni utawala bora.
   
 9. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #9
  Nov 4, 2008
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Urudishaje fedha kisheria ungetafsirika kama "admission of guilt".Hii peke yake ni ushahidi tosha wa kumpata mtu na hatia.Ama kweli nchi yetu sasa inaweka precendent mbaya sana kwa uhalifu na wahalifu!
   
 10. Sajenti

  Sajenti JF-Expert Member

  #10
  Nov 4, 2008
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 3,673
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  ....Hizo pesa sio za EPA mi nadhani ni wale wafanyabiashara wa ng'ombe kutoka Bariadi ndio walikuwa wanapeleka pesa ya mauzo benki...Bilioni 17 ghafla kiasi hicho ina maana hata hao benki hawawezi kumuuliza mteja wao? au wao wanapokea tu lazima wangetilia shaka....I don't believe this at all!!!!!!!!!!!!!!!!!!
   
 11. w

  wajinga Senior Member

  #11
  Nov 4, 2008
  Joined: Jun 25, 2008
  Messages: 148
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hii ni hadhithi ya alfu ulele ulela siku mia na moja.
   
 12. Halisi

  Halisi JF-Expert Member

  #12
  Nov 4, 2008
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 2,810
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Jamani kwanza kabisa ni kweli kulikuwa na marundo ya fedha katika benki ya Exim na waliopeleka wanajulikana, lakini kitaaluma huwezi kuwataja ktk gazeti
   
 13. Maarifa

  Maarifa JF-Expert Member

  #13
  Nov 4, 2008
  Joined: Nov 23, 2006
  Messages: 2,880
  Likes Received: 1,050
  Trophy Points: 280
  I believe you. Tz bwana usanii everywhere
   
 14. Mwanaukweli

  Mwanaukweli JF-Expert Member

  #14
  Mar 19, 2013
  Joined: May 18, 2007
  Messages: 4,451
  Likes Received: 288
  Trophy Points: 180
  Leo nilikuwa napitia tu masuala ya kesi zenye kugusa maslahi ya viongozi wa chama, au chama chenyewe....
   
Loading...