Ndallo
JF-Expert Member
- Oct 1, 2010
- 7,619
- 4,298
Wana JF habari za hapa? Natumaini wote mu wazima wa afya, Naomba kuwauliza wana Greaty Thinkers tokea uchaguzi uishe kwenye kile kinyanganyiro cha kuwapata Madiwani/Wabunge na Raisi sijapata kumtia machoni yule muheshimiwa wa kule Rombo baada ya mshikaji wake kumnadi lakini akapigwa chini hivi yuko wapi jamani? Hata kwenye matokeo ya Uraisi hakuonekana na hata kwenye sherehe za kumwapisha hasimu wake pia hajaoneka! Kulikoni jamani? Kwangu mimi sintamsahau kwa ile kauli yake aliyoitoa kua Nyasi mtakula lakini penda msipende Ndege ya Raisi lazima inunuliwe! pia sintamsahau kwa kutuachia SIGNATURE yake kwenye noti halali kwa malipo ya TZ Mungu ambariki huko aliko na pia namtakia apambane na ile kesi yake inayomkabili.