Pes ni jipu

LH XiV

JF-Expert Member
Nov 27, 2016
346
350
Hawa jamaa wanajiita ProEmploymentSolution ni hatari kwa afya yako. Ni kampuni inayojihusisha na udalali wa ajira, kwa maana ya wao kukutafuta then wanakutafutia ajira au makampuni kuajiri wafanyakazi kupitia wao.

Sasa naona wafanyakazi wao wanafanya kazi kama traffic. Wanauwezo kutoka nyumbani bila kitu na kurudi na rundo la pesa wanazojipatia kwa utapeli tu.

Wanatangaza ajira kadhaa uki apply unaitwa kwajili ya interview na hapo ndipo jamaa wanapopigia pesa, ukimaliza tu interview unaambiwa sasa kuna jamaa mwingine naye kaja leo anasifa kama zako ila hana hela....lazima mwanaume upinduke anakutajia kiasi anachohitaji ili akufanyie wepesi kutoka kwenye wimbi la kukosa ajira.

Basi kama kawa unaanza kushukuru Mungu na wengine wanaanza kuaga ndugu jamaa na marafiki kwamba muda wowote kuanzia sasa naitwa kazini basi utazeeka ukisubiri parachichi chini ya mgomba.

Kuweni makini na haya yanayojiita makampuni ya ajira.
 
M nishatapeliwa lak i nilifanyiwa interviw nkaambiwa nilipe lak jtatu niende kazn nkarud nyumban nkakopa laki tena kwa riba ya elf 50 nkawatumia lak jumatatu nmefika akiba pale nampigia kasem nmsubir wapo shel nilikalishwa ad sasa sita badae hawapatikan ad leo nlichanganyikiwa ad leo naogopa ku apply kaz tuwen makin
 
Hivi hawa jamaa ni kwamba hawaonekani na serikali?
Au nao ni mradi wa wakubwa kama tulivozoea kuambiwa kwa kila kinachoumiza wananchi
 
wameanza lini hawa watu? washanitaftia kazi flan na sikutoa hata kumi. ila invoice yao ilienda kwenye ile kampuni
 
M nishatapeliwa lak i nilifanyiwa interviw nkaambiwa nilipe lak jtatu niende kazn nkarud nyumban nkakopa laki tena kwa riba ya elf 50 nkawatumia lak jumatatu nmefika akiba pale nampigia kasem nmsubir wapo shel nilikalishwa ad sasa sita badae hawapatikan ad leo nlichanganyikiwa ad leo naogopa ku apply kaz tuwen makin
Pole sana, siku nyingine uwe makini
 
Hivi hawa jamaa ni kwamba hawaonekani na serikali?
Au nao ni mradi wa wakubwa kama tulivozoea kuambiwa kwa kila kinachoumiza wananchi
Tukisubiri serikali iwashughulikie wataendelea kutapeli watu kila siku. Kinachotakiwa mtu ambaye ametapeliwa kuanza kushughulika nao cha msingi ni kuwa na ushahidi mzuri.
 
HAWA JAMAA, NI WABAYA SANA , HUU MWAKA SASA KAMPUNI YETU INATUMA PESA ZA MAFAO KWAO , LAKINI MPAKA SASA BADO HAWAJAWEKA , YANI HAWAFAI ,UKIFIKA PALE BOSS YUPO NDANI ILA WANAKWAMBIA HAYUPO. YANI HAWA NI JIPU. TENA KUNA MFANYAKAZI WAO ANAITWA NEEMA ANA ROHO MBAYA SANA KWA KWELI
 
Hawa jamaa kumbe wanapokea mpaka mafao duh
 
M nishatapeliwa lak i nilifanyiwa interviw nkaambiwa nilipe lak jtatu niende kazn nkarud nyumban nkakopa laki tena kwa riba ya elf 50 nkawatumia lak jumatatu nmefika akiba pale nampigia kasem nmsubir wapo shel nilikalishwa ad sasa sita badae hawapatikan ad leo nlichanganyikiwa ad leo naogopa ku apply kaz tuwen makin
Duh aisee pole sana..We endelea tu ku apply kazi wala usiogope ila ukiambiwa habar za pesa ndo ukimbie bila kugeuka nyuma
 
Back
Top Bottom