Peru imeongeza zaidi ya mara mbili idadi rasmi ya vifo na kuwa nchi yenye kasi kubwa ya vifo vilivyosababishwa na ugonjwa wa COVID-19

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,482
9,242
Peru imeongeza zaidi ya mara mbili idadi rasmi ya vifo na kuwa nchi yenye kasi kubwa ya vifo vilivyosababishwa na ugonjwa wa COVID-19 kote ulimwenguni

Serikali ya Peru imesema imeongeza idadi ya vifo kutoka 69,342 hadi 180,764 kufuatia ushauri wa jopo la wataalamu wa afya, lililogundua kulikuwepo na mapungufu katika kuhesabu.

Kwa mujibu wa takwimu za shirika la habari la AFP, kufuatia usahihishaji huo, Peru sasa inaongoza kwa kuwa na kasi kubwa kabisa ya vifo vilivyosababisha na virusi vya corona kuliko nchi yoyote duniani, ikiwa na vifo 5,484 katika kila wakazi milioni moja.

Kwa mujibu wa data za AFP, Peru, yenye wakazi milioni 33 awali iliorodheshwa katika nafasi ya 13 duniani ikiwa na vifo 2,103 kwa kila watu milioni moja. Peru imeorodhesha zaidi ya maambukizi milioni 1.9 hadi leo, na katika siku za hivi karibuni imekabiliwa na uhaba mkubwa wa gesi ya oksejeni kuwatibu wagonjwa wa corona.

Waziri Mkuu wa Peru, Violeta Bermudez amesema idadi ya vifo ilisahihishwa kufuatia ushauri wa jopokazi lililopendekeza marekebisho ya mfumo wa kuweka data wa Peru.

"Mojawapo ya changamoto za janga hili imekuwa kuweka rekodi ya watu waliokufa katika daftari, kwa kuwa mienendo ya iana mpya ya virusi ilihitaji mbinu maalumu, miundombinu na itifaki ambazo sio kila taasisi ilikuwa imeandaliwa kuzishughulikia".

Jopo hilo lilisema katika ripoti yake kuwa mfumo uliopo ulitoa matokeo yasiyo sahihi yalioonesha idadi ndogo ya vifo kutokana na ugonjwa wa COVID-19.

Majina mapya ya aina za virusi vya corona

Wakati haya yakiarifiwa shirika la afya duniani WHO limetangaza mfumo mpya wa kuzipa majina aina mbalimbali za virusi vya corona kutumia alfabeti ya Kigiriki. Aina hizo awali zilikuwa na majina kutegemea na herufi na nambari au nchi zilikogunduliwa kwanza.

Shirika hilo limesema linatumai kuleta uwiano katika usawa na uelewa juu ya aina za virusi vya corona zinazotia wasiwasi, kwa kutumia mfumo huo mpya.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom