Personal Plea Kwa Rais Magufuli: Kama ameweza kuwasamehe wabakaji, wauaji, mafisadi, wahujumu, anaweza pia kumsamehe Eric Kabendera, amzike mama yake

Rais hapangiwi. Usitake Rais Magufuli afanye vitu kwa matakwa yenu. Leo atamwachia Kabendera kesho mtataka amwachie mwingine. Pia kutoa mfano wa wabakaji kuachiwa huo ni upuuzi. Hata Yesu aliwasamehe wazinzi ambapo kwa akili ya kibinadamu lilionekana ni kosa Kubwa na kuuwawa kwa mawe. Pia ndugu yangu njaa ujue Rais Magufuli ana vyombo vingi vya kiuchunguzi tofauti na akili yako ndogo na kisheria uliyo nayo. Rais ana wataalam wasomi mahiri wengi wa kumshauri iwe wewe na katambaza, kailboru na kadigrii kako kamoja kasheri.

Sent using Jamii Forums mobile app
Rais hapangiwi ?shame sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Uteuziiii.....2020 subiria tu unakuja.......
Achana na hayo,kama ni hivyo ndio imemrudia huyo kibendera inamuumiza mara 100 kwa kusababisha kifo cha mama yake
Badala ya kumtisha Rais na karma,ungemshauri kibendera atumie plea bargain law atoke ile ipo wazi na kwa hatua iliopo kesi yake,inakubalika tu
Kibendera aliandika barua ya kuomba msamaha,akaambiwa ataje walio nyuma yake amekataa,hapo unamlaumu Rais kwa lipi
Kibendera ana mchango mkubwa kwenye kifo cha mama yake,hakujali hisia za mama yake alitanguliza mbele maslahi yake na mabeberu
Ikumbukwe kuwa yule mama alikiri kumuonya mwanawe aachane na mambo hayo ya kutukana watu,lakini hakumsikiliza

Vijana wengi ni chanzo cha madhila yanayowapata wazazi wao kwa kutanguliza.. Pesa, umaarufu na starehe za muda mfupi, kijana anayejua wajibu wake kwa wazazi hawezi kuwa chanzo cha madhila haya au hata kifo kwa wazazi wake.. utamaduni wa kuweka picha za wazazi au watoto mezani ofisini kwa baadhi ya watu ni picha hizo zimkumbushe wajibu alionao kwao asije sahau akafanya matendo yatakayoleta huzuni kwao!
 
Pascal Mayalla,
Paskali nimesoma ombi lako la msamaha wa Kabendera uliliolielekeza kwa Mh. Rais wa JMT. Nimefarijika kusikia kuwa wewe umesoma sheria na unajua mipaka ya mamlaka ilivyo kisheria. Ombi hili likisikilizwa na kukubaliwa na muwombwaji utakuwa umeleta mgogoro wa kisheria.

Siku zote kwa taaluma yetu tunaaamini sheria ni maisha bila busara ingawa na sheria nayo inabusara zake. MBANE DPP mwambie atumie busara zote mbili -ile busara halisi na busara ya sheria- usimuchomekee Rais wa JMT.
 
Pole Pascal Mayalla naona watu wanakuhukumu kwa hisia bila kuangalia uhalisia.
Watu wanamhukumu Pascal wakidai kua kamchongea Kabendera lakini wanasahau kua Kabendera alikua anamchongea Magufuli kwa Mabeberu lakini hawakuliona hilo.
Kabendera na Pascal wote ni waandishi na wanaandika habari za uchunguzi sioni uchonganishi wowote alioufanya Pascal.
Kabendera kahukumiwa kwa kosa lingine tofauti na kazi yake ya uandishi.
Mkuki kwa nguruwe kwa binadamu mchungu
Yaonekana alikuwa yeye. Tangu atiwe kibano hatuoni tena makara za aina hiyo. Alijua ni mtu muhimu ktk familia yake, a bread winner, bado akajiingiza ktk uandikaji wa kijinga. Akisifiwa na kugusw mgongoni eti ni shujaa. That was rubbish of him!
 
Kama hawakuweza kumpa msaada mama yake pindi mgonjwa wakijua fika Eric ndo alikua tegemeo lake basi haina maana kumtoa kwaajili ya kumzika tu. Tuthamini watu pindi wakiwa hai.

Kuna mambo yanaendelea bongo chini ya huu utawala yanasikitisha sana. Sheria ya uhujumu uchumi inaidi ipitwe upya ASAP
 
Of all days leo ndio umeona ujitokeze kwenye msiba kukanusha habari za wewe kumchongea Erick?
Alafu what changes kujitambulisha kama Pascal au mwandishi wa habari mwenye LLB (hons)
Guy!
Anajaribu kujitofautisha na wakina Maulid Kitenge😂😂😂,walioingia kwenye utangazaji baada ya kufeli masomo yao ya sekondari
 
Wanafiki ni wengi sana duniani. Kuna siku nilisoma mahali kuwa huyo mama alimlilia Mh. Rais amwachie mwanaye kwa kuwa ndiye Tegemeo lake kwa uzima na afya yake. Kama ni kweli aliomba tena akiwa analia basi Mungu ampumzishe sasa ila machozi yake yale yatageuka laana kwa baadhi ya viumbe duniani. Tumwogope Mungu narudia Tumwogope Mungu.
 
Kama hawakuweza kumpa msaada mama yake pindi mgonjwa wakijua fika Eric ndo alikua tegemeo lake basi haina maana kumtoa kwaajili ya kumzika tu. Tuthamini watu pindi wakiwa hai.

Kuna mambo yanaendelea bongo chini ya huu utawala yanasikitisha sana. Sheria ya uhujumu uchumi inaidi ipitwe upya ASAP
Too hysterical! Woote walioko magereza, wana baba, mama, watoto, wajukuu, nk. Eric is no exception.
 
71 Reactions
Reply
Back
Top Bottom