Personal Plea Kwa Rais Magufuli: Kama ameweza kuwasamehe wabakaji, wauaji, mafisadi, wahujumu, anaweza pia kumsamehe Eric Kabendera, amzike mama yake

Pole Pascal Mayalla naona watu wanakuhukumu kwa hisia bila kuangalia uhalisia.
Watu wanamhukumu Pascal wakidai kua kamchongea Kabendera lakini wanasahau kua Kabendera alikua anamchongea Magufuli kwa Mabeberu lakini hawakuliona hilo.

Kabendera na Pascal wote ni waandishi na wanaandika habari za uchunguzi sioni uchonganishi wowote alioufanya Pascal.
Kabendera kahukumiwa kwa kosa lingine tofauti na kazi yake ya uandishi.
Mkuki kwa nguruwe kwa binadamu mchungu
 
Rais alishauri kupitia kwa DPP kutoa msamaha kwa watakaojutia makosa yao.. kwa nini Pasco hukumshauri rafiki yako kabendera kutumia fursa hiyo??? sidhani ni Sawa na ni adabu kurejea kumuomba Rais atoe msamaha wakati alishafanya hivyo.. yaliyotokea yanatokea kwa binadamu wote, kitu muhimu kujifunza ni vyema kuishi maisha huku ukitambua wajibu wako kwa wazazi, watoto, ndugu na marafiki ukikumbuka wajibu huu siku zote utajiepusha na mambo yanayoweza kuleta huzuni na fadhaa kwa hao niliowataja!!
 
Kwa swala hili mr P nafsi inamsuta, na haita msaidia hata afanyeje litabaki kuwa kovu katika maisha yake. Ji be kweli nia yake katika makala zake alikuwa na lengo la kumshitaki Kabendela.
Amekuwa kama Yuda Eskaliote na tangu wakati ule mr P hakutulia pole ulimazi kazi yako sasa nikushurehejea matokeo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Namalizia kwa kusisitiza karma is real na haina mswalie Mtume.
Achana na hayo,kama ni hivyo ndio imemrudia huyo kibendera inamuumiza mara 100 kwa kusababisha kifo cha mama yake
Badala ya kumtisha Rais na karma,ungemshauri kibendera atumie plea bargain law atoke ile ipo wazi na kwa hatua iliopo kesi yake,inakubalika tu
Kibendera aliandika barua ya kuomba msamaha,akaambiwa ataje walio nyuma yake amekataa,hapo unamlaumu Rais kwa lipi
Kibendera ana mchango mkubwa kwenye kifo cha mama yake,hakujali hisia za mama yake alitanguliza mbele maslahi yake na mabeberu
Ikumbukwe kuwa yule mama alikiri kumuonya mwanawe aachane na mambo hayo ya kutukana watu,lakini hakumsikiliza
 
Paskali umekuwa kama wayahudi enzi za Kristo hawakueleweka walikuwa wanatangatanga,mwanzo walimpokea Yesu kristo,badae haohao wakamgeuka wakamuadhibu kwakumchapa mijeledi na haohao walipomaliza kumuua na kuziona zile ishara kuuu kama Giza baada ya kifo chake wakajirudi wakasema kumbe alikuwa mwana wa Mungu.

Kama hii unayoiita Karma ipo,unafikiri kwa sakata hili la kifo cha mama Kabendera kufuatana na zile makala zako ambazo watu wanakutuhumu ndio chanzo cha kukamatwa kabendera unafikiri karma itakuacha?
 
Rais hapangiwi. Usitake Rais Magufuli afanye vitu kwa matakwa yenu. Leo atamwachia Kabendera kesho mtataka amwachie mwingine. Pia kutoa mfano wa wabakaji kuachiwa huo ni upuuzi. Hata Yesu aliwasamehe wazinzi ambapo kwa akili ya kibinadamu lilionekana ni kosa Kubwa na kuuwawa kwa mawe.

Pia ndugu yangu njaa ujue Rais Magufuli ana vyombo vingi vya kiuchunguzi tofauti na akili yako ndogo na kisheria uliyo nayo. Rais ana wataalam wasomi mahiri wengi wa kumshauri iwe wewe na katambaza, kailboru na kadigrii kako kamoja kasheri.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hatutaki msamaha wowote ule! Yule mama aliomba kijana wake asamehewe mpaka akamwaga machozi lakini watu wakakaza shingo, leo amefariki kwa kukosa huduma ndio watu waombe msamaha? HAKUNA ABAKI HUKO NA LI MSAMAHA LAKE!

Nyie kama team kabendera mnamsupport kwa keyboard tu mama yake mmeshindwa kumsaidia mnabki kelele RIP apa
 
Back
Top Bottom