Fistula: Sababu, dalili, athari na tiba

Kila tarehe 23 mwezi Mei ni Siku ya Kimataifa ya Kutokomeza Fistula ya uzazi. Kaulimbiu ya mwaka huu ni “TUMAINI, UPONYAJI NA HESHIMA KWA WOTE.”

Kwa Tanzania matibabu ya Fistula ni BURE kabisa ikijumuisha nauli ya kumtoa mgonjwa alipo hadi hospitali, chakula, upasuaji na nauli ya kumrudisha. Hii ni katika kuhakikisha Fistula ya Uzazi inatokomezwa kabisa nchini ambapo kwa takwimu za mwaka 2014, wanawake takribani 20,000 walikuwa na fistula nchini.

‘Wanawake 20,000 wana ugonjwa wa fistula Tanzania’

FISTULA NI NINI?

Fistula si neno geni kwa wengi wetu ingawa inawezekana tusijue maana halisi ya neno hili. Fistula ni tundu linalounganisha njia mbili za mwili zilizo wazi. Kuna fistula za aina nyingi lakini inayozungumziwa hapa ni Fistula ya Uzazi(Obstetric Fistula).

FISTULA YA UZAZI

Fistula ya uzazi ni tundu lisilo kawaida ambalo halikutakiwa kuwepo kati ya kibofu cha mkojo na njia ya uke(Vesico-Viginal Fistula – VVF) au kati ya njia ya haja kubwa na uke(Recto-Vaginal Fistula – RVF). Wanawake wengi hupata VVF, wachache RVF na wachache zaidi hupata zote kwa pamoja.

SABABU ZA KUTOKEA KWA FISTULA

Uzazi Pingamizi

Fistula mara nyingi hutokana na Uzazi pingamizi(Obstructed labour) wa muda mrefu ambao haukuhudumiwa kwa wakati mwafaka. Hali hii inapotokea kunakuwa na msuguano kati ya mfupa katika nyonga na kichwa cha mtoto unaopelekea jeraha katika njia ya haja kubwa au ndogo ambalo baadaye hugeuka kuwa tundu.

Uzazi au uchungu pingamizi ni uzazi usioendelea aidha kwa sababu mtoto ni mkubwa kuliko njia ya uzazi, nyonga za mama kuwa na tatizo(aidha mama hakuwa na ukuaji mzuri kutokana na utapiamlo utotoni au ajali iliyoathiri nyonga) ama ulalo mbaya wa mtoto tumboni.

Upasuaji

Upasuaji kwa ajili ya uzazi au matibabu mengine katika viungo vilivyopo maeneo ya nyonga huweza kusababisha fistula. Hii hutokea pale daktari ama kwa bahati mbaya ama uzembe anatoboa kuta za njia ya haja kubwa au ndogo ya mgonjwa na kusababisha fistula.

Mionzi

Mionzi kwa ajili ya matibabu ya Saratani ya Shingo ya Uzazi huweza kusababisha fistula kwa kuua seli na kupelekea tundu.

Majeraha/Magonjwa ya Kuambukiza

TB ya Kibofu

Majeraha ukeni


DALILI ZA FISTULA


Dalili kuu ya fistula ni mwanamke kutokwa na haja kubwa au ndogo bila ridhaa yake au bila kujua.

Nyinginezo:-

Vidonda sehemu za siri

Kuchechemea kutokana na maumivu yatokanayo na uzazi pingamizi

MADHARA YA FISTULA

Kimwili

Mwanamke kutokwa na haja ndogo au haja kubwa ama vyote kwa pamoja bila kutambua wala kuwa na uwezo wa kuzuia hali hiyo.

Kuungua au kutokwa na vidonda sehemu za siri vitokanavyo na kemikali zilizopo kwenye mkojo.

Kupoteza uwezo wa kuzaa.

Kupoteza uwezo wa kujamiiana.

Kijamii

Unyanyapaa wa mtu binafsi na jamii kwa ujumla

Kutelekezwa ama kutalikiwa na mume au mwenza

Kushindwa kushiriki shughuli za kijamii


Kisaikolojia

Kushuka moyo (Sonona)

Aibu na Kutojiamini

Kujiua kwa baadhi ya wanawake kwa kukosa tumaini (85% hupoteza watoto wao pia)

Kiuchumi

Kushindwa kufanya shughuli za kiuchumi na kuishi maisha ya dhiki.

MATIBABU

Matibabu ya Fistula ni kwa nja ya Upasuaji wa kuziba tundu/matundu yaliyojitokeza.

Baada ya hapo mwanamke huwekewa mpira wa haja ndogo kwa muda wa siku 14 ili njia iweze kupona na baada ya hapo huangaliwa kama amepona.

Baadhi ya wanawake hufikishwa hospitali wakiwa na kibofu cha mkojo kilichoharibika kabisa hivyo hufanyiwa upasuaji na kutengenezewa kibofu cha bandia katika sehemu ya haja kubwa hivyo hujisaidia haja zote kwa pamoja.

Fistula ni ugonjwa wa aibu na fedheha kwa wanawake na hupelekea waathirika kupoteza maana ya maisha hivyo sambamba na upasuaji, huduma za ushauri wa kisaikolojia hutolewa ili kuweza kuwarudishia thamani yao. Mafunzo ya Ujasiriamali pia hutolewa pia ili kuwawezesha wanawake hawa kujiinua kiuchumi na kumudu maisha yao mapya.


KINGA YA FISTULA

Fistula ni ugonjwa ambao unaweza kutokomezwa kabisa endapo hatua sahihi zitachukuliwa

Kuwahi kwenda kujifungulia kwenye kituo cha kutoa huduma za afya

Mama kuhudhuria kliniki ili kujua hatari zozote zilizopo na kupanga mipango ya kuzikabili

Kuzuia mimba za utotoni(Ni rahisi kwa mtoto kupata fistula kwani maungo hayajakua vizuri)

Serikali kuboresha miundombinu na huduma za afya ya uzazi hasa vijijini. Uwepo wa huduma za dharura kama upasuaji au uwepo wa magari ya wagonjwa na barabara thabiti ndio njia pekee ya kutokomeza janga hili.
 
Mola awajaalie wamama wote wenye hili tatizo wapone haraka,

Pia atuepushe sote na tatizo hili,

Na kwa wale wanaoogopa kwenda hospital tiba ipooo na Fistula inatibika, si vema kujifungia ndani na kujitenga.
 
Matibabu ni bure lakini huko vijijini wengine hata hawalijui hili. Watafikiwaje na taarifa?
 
Ni muhimu kwa mjamzito kuanza kuhudhuria kliniki mapema ili kulinda afya yake na mtoto aliye tumboni. Kwa kutambua umuhimu wa kulinda afya ya mama na mtoto, serikali imefanya mapinduzi katika sekta ya afya ikiwa ni ku- jenga miundombinu hasa ujenzi wa vituo vya afya kwa kila kata lengo likiwa ni kusogeza huduma karibu na wananchi.

Serikali na taasisi binafsi zime- kuwa na ushirikiano hasa katika kukabiliana na magonjwa yanay- owasibu wajawazito hususani tatizo la fistula.

Fistula ni aina ya ugonjwa ambao huweka shimo kubwa kati ya njia ya uzazi na njia ya mkojo unatokana na mama kuwa na uchungu wa muda mrefu bila matibabu.

Kwa mujibu wa Daktari Bingwa wa Upasuaji kutoka hospitali ya CCBRT, Dk. James Chapa, tatizo hilo huwaathiri zaidi wasichana ambao wanapata mimba wakiwa na umri mdogo na kujifungua kabla mifupa ya sehemu za kizazi ikiwa bado haijakomaa ipasavyo.

Anasema wanawake ambao tundu la kizazi chao ni dogo au wale ambao wamekeketwa wako katika hatari kubwa ya kupata maradhi hayo.

Anaeleza kuwa wanawake ambao wameathirika na mara- dhi hayo huvuja mkojo mara kwa mara bila kukusuadia, harufu mbaya ya mkojo hufanya waathirika kutengwa na kunyan- yapaliwa kwa kudhaniwa kuwa ni wachafu.

“Mtatizo mengine yanayoto- kana na maradhi hayo ni ukosefu wa maji ya kutosha mwilini na utapiamlo,” anabainisha.
Dk. Chapa anasema ugonjwa wa fistula humdhalilisha mwan- amke na kumsababishia madhara mengine ya kiafya.
“Ili mwanamke apone ugonjwa huu ni vyema akatibiwe hospi- tali kwani hakuna eneo mbadala ambalo tiba inapatikana.

“Matibabu yakifanyika mape- ma na kuwa na ufasaha majibu huwa mazuri kwa zaidi ya asil- imia 90 hivyo, kama yupo mwe- nye tatizo hili na bado hajafika hospitali afike CCBRT kwaajili ya matibabu,” anasema.

TAKWIMU ZILIVYO
Takwimu za Shirika la Afya Duniani (WHO), za mwaka 2018 zinaonyesha kuna wanawake takribani milioni mbili wanaishi na fistula duniani.

Inakadiriwa kuwa wagonjwa wapya kati ya 50,000 na 100,00 hupatikana kila mwaka, wakati juhudi za kutibu fistula duni- ani huishia kutibu wagonjwa 20,000 tu.

Idadi kubwa ya wagonjwa wenye fistula wapo zaidi barani Afrika hususan kusini mwa Jangwa la Sahara huku nusu wakiwa nchini Nigeria, mabara mengine ni Asia na Amerika ya Kusini.

Hapa nchini, takwimu za Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto zinakadiria kuwa na wanawake takribani 2,500 ambao hupata fistula kila mwaka, huku idadi ya wanaopatiwa matibabu kila mwaka ikiwa ni takribani wa- nawake 1,000 kwa mwaka.

“Katika kipindi cha miaka mitano kuanzia 2015 hadi De- semba, 2019 wanawake zaidi ya 5,500 walitibiwa fistula.

“Mafanikio haya yanatokana na kampeni iliyoendeshwa kwa ushirikiano baina ya serikali na wadau ambayo imeweka mabalozi wa fistula zaidi ya 3,000 nchi nzima wanaosaidia kuratibu rufaa na usafiri kwa wagonjwa kwenda hospitali zinazotoa huduma ya fistula,” anasema Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu.

AINA ZA FISTULA
Dk. Chapa anasema zipo fistula ambazo hazisababishwi na masuala ya uzazi.

“Upo ugonjwa wa saratani unaweza kusababisha aina ny- ingine ya fistula, pia matibabu ya mionzi yanaweza kusababi- sha ugonjwa huo.

“Mtu akipata jeraha kuto- kana na ajali yoyote anaweza kupata fistula na magonjwa mengine kama kichocho na kibofu cha mkojo ambayo husababisha fistula,” anasema.

Dk. Chapa anasema upas- uaji nao husababisha fistula na hii huhusisha mirija inapotoa mkojo kwenye figo kupeleka katika kibofu.

“Mirija hii mara nyingi hupita karibu na kizazi na upasuaji huhusisha kizazi, mirija hii ikitokea kukatwa au kufungwa wakati wa upasuaji, pia kibofu cha mkojo kipo ka- ribu na kizazi hivyo wakati wa upasuaji jeraha hutokea eneo la kibofu na kusababisha fistula,” anasema.

INAWEZA KUJIRUDIA
Dk. Chapa anasema mama aliyefanyiwa upasuaji kabla ya kuondoka hospitali ni vyema akamuuliza daktari endapo ku- likuwa na tatizo lolote wakati wa tukio hilo.

“Kuna uwezekano wa kutokea majeraha wakati wa upasuaji hivyo mama anapofa- hamu kama kulikuwa na tatizo akashauriwa nini cha kufanya baada ya kuruhiusiwa.

“Kama kulikuwa na jeraha katika kibofu mama huwekewa mpira wa kutolea mkojo ili apumzishe kibofu cha kutolea mkojo kuanzia siku 10 hadi 14. “Pia mama huyu atashauriwa kunywa maji na kuwa msafi ili kuepusha maambukizi katika viungo vya uzazi,” anasema.

Dk. Chapa anasema mgonjwa aliyetibiwa fistula upo uwezekano wa kuupata ugonjwa huo kwa mara nyingine.

“Tunapowatibu wagonjwa masharti tunayowapa ha- waruhusiwi kujifungua kwa njia ya kawaida baada ya upas- uaji huo, uzazi utakaofuata ni kwa upasuaji ili kumwepusha mtoto kupita njia ya kawaida na kufumua eneo ambalo lilirekebi- shwa,” anasema.

Dk. Chapa anasema mama anashauriwa baada ya miezi minne ndio hupendekezwa kushiriki mapenzi na ataka- poanza kinyume na muda huo uwezekano wa ugonjwa huo kurudi ni mkubwa.

WANAOATHIRIKA ZAIDI
Dk.Chapa anasema wa- naoathiriwa zaidi na fistula ni ambao hawajafika umri salama kwaajili ya uzazi, kuanzia miaka 18 na kuendelea.

“Mtu akipata mimba kabla ya umri huo uwezekano wa kupata fistula ni mkubwa kwa sababu nyonga yake haijakomaa, pia inawapata kina mama wa umri wowote, ukilinganisha na wenye miaka 18 na kuendelea waliopata ujauzito na wenye umri chini ya hapo wanauwezekano wa kupata fistula mbaya zaidi kwa sababu wanapata majeraha makubwa,” anasema.

UELEWA MDOGO
Dk. Chapa anasema bado uelewa wa jamii juu ya ugonjwa fistula ni mdogo. “Watu hawajui chanzo cha ugonjwa na matib- abu yake nini kwahiyo inaathiri mtiririko wa wagonjwa kuja kupata matibabu.

“Kama mtu haamini hili ni tatizo la kawaida ni ngumu kum- shawishi kutafuta matibabu, pia wanapofika hospitali tunakutana na changamoto za afya zao.

“Mtu anakuja akiwa na upungufu wa damu, magonjwa mengine ambayo hayakutibika vizuri kama presha na kisu- kari ambayo hutupa changamoto kumhudumia mgonjwa vizuri,” anasema.

Changamoto nyingine anayoi- taja Dk. Chapa ni tatizo la kiakili ambalo huwakumba wagonjwa hao.“Wengine wanakuja tayari wana shida ya kiakili kum- saidia inakuwa changamoto, kwa sababu matibabu yetu yanahitaji ushirikiano baina ya wataalamu na mgonjwa mwenyewe.

Baada ya upasuaji mgonjwa anapaswa kuwa katika mashine ya kutolea mkojo kwa siku 14 na anahitajika kunywa maji kila siku.

“Kwahiyo, mtu ambaye akili haikuwa sawa hawezi kufuata masharti baada ya upasuaji hivyo tunajitahidi muda wote kukabiliana nao.

Pia baada ya upasuaji watu hawafuati masharti tunayotoa baada ya upasuaji ndio maana utakuta wengine ugonjwa hu- rudi,” anasema.

UMASKINI NI TATIZO
Furaha Mafuru, ni Ofisa Programu Kitengo cha Mama na Mtoto Shirika la Kimataifa linaloshughulikia Idadi ya Watu (UNFPA), anasema tatizo la fis- tula huwapata wanawake wengi wasio na kipato cha kutosha, hali ambayo huwasababisha kwenda kujifungulia kwa wakunga wa jadi au nyumbani.

“Kwa sababu hawana uwezo inakuwa ni changamoto kwao ku- toka nyumbani kwenda hospitali kwaajili ya matibabu, hii huwa chanzo cha wao kupata ugonjwa huu kutokana na kuchelewa mat- ibabu,” anasema.

Anasema katika kuimarisha huduma za haraka za kujifungua, serikali ikishirikiana na wadau uboreshaji mkubwa wa vituo vya kutoa huduma haraka ume- fanyika.

“UNFPA ikishirikiana na serikali imeboresha vituo katika Mkoa wa Simiyu Kigoma katika kipindi cha miaka miwili, tume- karabati vituo vya afya 40 Simiyu na vituo sita Kigoma na sasa kina mama walio mikoa ya pembezoni kwasasa hawapati shida kwa sababu vituo vilivyoboreshwa vimewekwa vifaa na kina mama wanapatiwa mafunzo ya kukabili- ana na hatari yoyote wakati wa kujifungua,” anasema.

HATUA ZINAZOCHUKULIWA NA SERIKALI
Kutokana na kuimarishwa kwa huduma, Waziri Ummy anasema idadi ya wanawake wanaojitokeza kutibiwa fis- tula katika hospitali za CCBRT, Bugando, Nkinga na Kuvulini Maternity Center, imepungua kwa zaidi ya asilimia 30.

“2016 walikuwa wagonjwa 1356; mwaka 2017 idadi hiyo ikashuka na kufikia 1060, mwa- ka 2018 ikashuka tena na kufikia idadi ya wanawake 900, na 2019 ikashuka zaidi na kufikia wa- nawake 852.

“Hii imetokana na kuimarika kwa upatikanaji wa huduma za upasuaji wa dharura chini ya uongozi wa Rais Dk. John Magu- fuli,” anasema.

Ummy anasema serikali imei- marisha huduma kwa wajawa- zito, hatua ambayo imesaidia kupunguza matatizo ya fistula kwa wanawake wengi nchini.

“Wajawazito waliotimiza mahudhurio manne au zaidi (ANC4+) mwaka 2019/20 wali- fikia asilimia 77 ikilinganishwa na asilimia 41 kwa kipindi kama hicho mwaka 2015/2016.

“Kina mama wanaojifungulia vituo vya kutolea huduma imeendelea kuongezeka hadi kufikia asilimia 83 Machi mwaka huu ikilinganishwa na asilimia 64 kwa kipindi kama hicho mwaka 2015/16. “Idadi ya vituo vya afya vinavyotoa huduma ya dharura kwa wajawazito (CEMONC) im- eongezeka na kufikia vituo 352; Machi mwaka 2020 ikilingan- ishwa na vituo 115 mwaka 2015,” anasema.
 
Wakuu ninasumbuliwa na huu ugonjwa, naomba mwenye uelewa wa mahali kwa kupata tiba nisaidie kwani unanitesa sana. Hii siyo fistula ya akina mama wakuu,atakayetoa msaada ajikite kwenye hili angalizo,mimi ni mwanaume. Vile vile Ccbrt hawatoi hii huduma.
 
Pole sana! Umejuaje kama una hiyo Perinal Vistula? kama umepimwa huko ulikopata majibu watakuwa na uelewa zaidi. Hata hivyo endelea kusubiri kuna wataalam humu wanaweza kukupa msaada.

Sio vibaya ukatueleza inakuwaje na sisis tukaijua.
Yote katika yote Mungu muumbaji wetu akuponye.
 
Pole sana! Umejuaje kama una hiyo Perinal Vistula? kama umepimwa huko ulikopata majibu watakuwa na uelewa zaidi. Hata hivyo endelea kusubiri kuna wataalam humu wanaweza kukupa msaada.

Sio vibaya ukatueleza inakuwaje na sisis tukaijua.
Yote katika yote Mungu muumbaji wetu akuponye.

Pole sana! Umejuaje kama una hiyo Perinal Vistula? kama umepimwa huko ulikopata majibu watakuwa na uelewa zaidi. Hata hivyo endelea kusubiri kuna wataalam humu wanaweza kukupa msaada.

Sio vibaya ukatueleza inakuwaje na sisis tukaijua.
Yote katika yote Mungu muumbaji wetu akuponye.

Amina mkuu,ni jipu flani linaota karibu na sehemu ya haja kubwa ila linakuwa na mzizi ndani sana. Nilienda hospitali flani wakaniambia linahitaji operation ila wao hawafanyi. Nimejaribu kufuatilia operation ya hii kitu inasemekana siyo kila daktari anafanya na huwa inarudi isipofanyika vizuri,kwa kifupi inaogopesha mkuu
 
Amina mkuu,ni jipu flani linaota karibu na sehemu ya haja kubwa ila linakuwa na mzizi ndani sana. Nilienda hospitali flani wakaniambia linahitaji operation ila wao hawafanyi. Nimejaribu kufuatilia operation ya hii kitu inasemekana siyo kila daktari anafanya na huwa inarudi isipofanyika vizuri,kwa kifupi inaogopesha mkuu

Pole sana. Inapokuwa ni issue ya vijipu au vivimbe haishauriwi kuichelewesha. Nenda hospitali kubwa zenye vipimo vya kueleweka na ninaamini ufumbuzi utapatikana. USIOGOPE
 
Unaumwa kweli wewe hayo maumivu unayavumilia vipi wakati hata kukaa ni shida pia iyo kitu inachimba kuingia ndani zaidi mm ni muhanga kama wewe ila now nipo vzr kabisa.

Labda nikudadavulie kidogo ili ujue kama niliwahi pitia hali kama yako Wengi wanafananisha na bawasiri lkn sio yenyewe hutokea pembeni ya njia ya haja kubwa kwenye Tako kwa chini bawasiri hutokea pale pale kwenye njia ya haja kubwa.

Huo uvimbe mara nyingi unakuwa na usaa mweusi wenye harufu mbaya sana pia pia linakuwa kinauma hatari hata ukienda haja kubwa ila bana achia mzee ni noma.

Pia kinachimba zaidi kuingia dani inafata mafuta futa ya huko chini. Ukienda hospital ambazo hamna daktari bingwa wa huo ugonjwa watakuja kata hata hayo marinda kabisa ya njia ya haja kubwa ni hatari.

TIBA
Ni upasuaji tu hakuna njia nyingine kidonda hakishonwi kinakuwa hivyo hivyo kama tundu mzee kunatokana na kuwa sehemu mbaya na kuna mafuta futa kinakuwa kinawaga majimaji damudamu mpk kianze kukauka.

Dawa kubwa ni kukalia maji ya uvuguvugu yenye detto ndani yake kwa siku mara 2 pia utapewa dawa za maumivu na za kukausha kwa wiki 2 za mwanzo kukaa itakuwa ngumu kidogo pia kinapona haraka kutokana na sehemu kilipo ila usafi muhimu sana kuna mda wa kujisaidia haja kubwa mtihani na chembe chembe zinaingia kwenye kidonda.

Upasuaji ni kawaida tu ngazi unapigwa ya kukata mawasiliano chini unadanyiwa ukiwa na fahamu zako ila utohisi chochote kwa wakati huo ila ngazi ikija isha baadae ndio utakuja ipata.

Dawa zipo nyingi za kukusaidia kwenye hizi hospital kubwa kubwa sindano za kukausha maumivu kinapona haraka sana

Nenda pale rabinisia tegeta namanga kuna daktari bingwa pale nimemsahau jina lake atakusaidia
 
Suluisho la hilo tatizo ni kufanyiwa operesheni. Ugonjwa huu ni ngumu sana kumwelezea mtu kama unaaibu ila jinsi siku zinavyokwenda aibu inabidi uweke pembeni. Chanzo kikuu cha tatizo ni constipation na pia epuka vyoo vya kukaa.
 
Suluisho la hilo tatizo ni kufanyiwa operesheni. Ugonjwa huu ni ngumu sana kumwelezea mtu kama unaaibu ila jinsi siku zinavyokwenda aibu inabidi uweke pembeni. Chanzo kikuu cha tatizo ni constipation na pia epuka vyoo vya kukaa.

Mkuu unaufahamu vizuri huu ugonjwa?
 
Kidonda kilichukua muda gani kupona mkuu? Kwani nina wiki lakini bado kinatoa maji maji
Tumia maji ya uvuguuvugu yakiwa na mchanganyiko wa sabuni ya Detto ya maji baada ya siku 10-14 kidonda kinakuwa kimepona.Angalizo mimi nilifanyiwa operesheni mara ya kwanza alafu baada ya mwaka tatizo likatokea tena ikabidi nifanyie tena. Ili kuepuka tatizo kujirudua usitumie choo cha kukaa na epuka vyakula vinavyoleta costipation.
 
Tumia maji ya uvuguuvugu yakiwa na mchanganyiko wa sabuni ya Detto ya maji baada ya siku 10-14 kidonda kinakuwa kimepona.Angalizo mimi nilifanyiwa operesheni mara ya kwanza alafu baada ya mwaka tatizo likatokea tena ikabidi nifanyie tena. Ili kuepuka tatizo kujirudua usitumie choo cha kukaa na epuka vyakula vinavyoleta costipation.

Asante kwa angalizo mkuu,je kama ni mtu wa kufanya mazoezi hasa ya kukimbia naweza endelea kufanya mkuu kwa uzoefu wako? Samahani kwa usumbufu mkuu
 
Asante kwa angalizo mkuu,je kama ni mtu wa kufanya mazoezi hasa ya kukimbia naweza endelea kufanya mkuu kwa uzoefu wako? Samahani kwa usumbufu mkuu
Mazoezi yanasaidia sana kwa sababu toka nianze kufanya mazoezi tatizo la constipation halipo tena . Mazoezi yamenisaidia kupata kiu ya kunywa maji, wakati zamani nilikuwa si mpenzi wa kunywa maji kabisa naweza kukaa siku mbili hadi tatu bila kunywa maji.
 
Mazoezi yanasaidia sana kwa sababu toka nianze kufanya mazoezi tatizo la constipation halipo tena . Mazoezi yamenisaidia kupata kiu ya kunywa maji, wakati zamani nilikuwa si mpenzi wa kunywa maji kabisa naweza kukaa siku mbili hadi tatu bila kunywa maji.

Asante mkuu kwa ushauri,ubarikiwe sana
 
Back
Top Bottom