Perfume kali kupitiliza ni utanashati au ulimbukeni?

Ni kweli watu tunazitumia hizi ila ukiwa umejipulizia nyingi inakera pia sasa kama unatumia daladala ndo kabisa unawakera watu wengine ila ikiwa kidogo na yenye harufu ambayo si kali sana inakua nzuri tu. kila kitu kinatakiwa kiwe kwa wastani tu ndio maana hata ulafi hautakiwi hata unyaji na ulevi ni tofauti
 
queeny kwa hiyo ulitaka mtu ajipulize perfume halafu ajifungie chumbani? Acheni hizo wapeni watu uhuru wao as long as havunji sheria na haki za binadamu.Dunia ni ya wote

Like like like!!!
kwa hiyo hata smoking in public unaona ni sawa tu just bcoz uko huru? hujui kuwa mapafyum makali yana madhara kwa watu wengine?...LIVE AND LET OTHERS LIVE
 
Kuna mtu alizaliwa anajua?
Hata wewe kujua hii perfume ni ya maiti si ulielekezwa?
Ukimkuta kajipulizia ya maiti na wewe mwelekeze....remember ignorance is bliss!!

it doest matter ya maiti ama la, just be moderate in anything u do..
 
Si lazima kujipulizia perfume, unaweza kuogea sabuni kama Protex Herbal inatosha au sabuni nyingine inaitwa Breeze. cha msingi utakiwi kunuka kama beberu.
Tihi tihi tihihii. Wenzako hiyo harufu ya Beberu wenzio ndo raha yao...Hivi umewahi kwenda nyumbani kwa wahindi au maeneo ya posta na kukutana na ile harufu yao? Lakn si ndo utamaduni wao??Utawakataza wakati wenyewe wanasikia raahaa kumoyo?
Sikujua kama na wewe Matola ni mzito wa kuelewa au labda unafanya makusudi.
 
kwa hiyo hata smoking in public unaona ni sawa tu just bcoz uko huru? hujui kuwa mapafyum makali yana madhara kwa watu wengine?...LIVE AND LET OTHERS LIVE
Sasa unachanganya habari.Kuna sheria ya kukataza kuvuta sigara public hasa kimataifa katika mambo ya haki za binadamu japo hapa bongo haifuatiliwi.Lakn perfum public sijawahi sikia...
 
Then, how moderate is moderate to every people?
Ujinga kwenda sikuzote, ukishamuelekeza mtu siku ya pili hatorudia
Ili la kulaumiana na kuitana washamba, limbukeni sio mpango....

it doest matter ya maiti ama la, just be moderate in anything u do..
 
Sasa unachanganya habari.Kuna sheria ya kukataza kuvuta sigara public hasa kimataifa katika mambo ya haki za binadamu japo hapa bongo haifuatiliwi.Lakn perfum public sijawahi sikia...

its not about the law but public morality...wewe unajipulizia wenzio wanapata madhara unasema sheria haijakataza uko huru. is that fair? kwani ukijipuliza kiasi na wengine wakaishi kwa amani kuna ubaya? otherwise that would be selfishness.
 
Mie nimekujibu kutokana na points zako na sasa unageuka..Kila mtu hapa ni selfish hata wewe ndo maana unalazimisha watu wawe kama wewe wakati ni ngumu.Yawezekana mwenzio kapaka udi mkali na yeye ni dawa inamtibu. Kutofautiana is natural my dear utake usitake we will never be the same.Na sio kwa kuwa mwenzio hataki unavotaka basi ndo umuite mshamba au wakuja..Big NO.
 
Tatizo siku hizi watu wengi wametopea katika ushirikina...
Utakuta mtu huyohuyo pia amevaa mapete makubwa,
minyororo shingoni,nk. Nimechunguza nimebaini wengi wao
wanafuata masharti ya Masangoma na watabiri wa nyota
eti ili kuvutia bahati au kupendwa/kusikilizwa na bosi n.k.
KWELI HUU NI UGONJWA WA MAWAZO WANAIBIWA SANA
 
Mie nimekujibu kutokana na points zako na sasa unageuka..Kila mtu hapa ni selfish hata wewe ndo maana unalazimisha watu wawe kama wewe wakati ni ngumu.Yawezekana mwenzio kapaka udi mkali na yeye ni dawa inamtibu. Kutofautiana is natural my dear utake usitake we will never be the same.Na sio kwa kuwa mwenzio hataki unavotaka basi ndo umuite mshamba au wakuja..Big NO.

kila mtu akiishi anavyotaka dunia haitakalika...we should learn to live with others.
 
Then, how moderate is moderate to every people?
Ujinga kwenda sikuzote, ukishamuelekeza mtu siku ya pili hatorudia
Ili la kulaumiana na kuitana washamba, limbukeni sio mpango....

hivi utakutana na mtu kwenye daladala uanze kumpa lecture ya perfume? wengine ni wakubwa wetu wa kazi. ndo maana kuna JF watu tunajifunza kimya kimya
 
NDO MAANA KUNA BIA aina nyingi lakini baa ni moja. Kuna bingwa, castle, safari c- lite, konyagi, power na nyinginezo. Hizi zote viwango vya ukali vinatofautiana. Je, kila kinywaji chake kipewe baa yake. Wote si tunaingia humo humo bila kujali huyu anakunywa nini na bila kusahau wavuta sigara? Kwa hiyo kila mtu apendacho mwache. Kama inakukera tafuta ofisi yako uwe safe. But kumbuka kuna watu wengine wanavutiwa sana na vilema ili kufanya nao mapenzi!!!!!!!!!! HAPO SASA UNASEMAJE, Utahama NCHI?:target:
 
Unajua unajichanganya sana..sasa kama huyu unayemsema wewe kwenye daladala atakuwa anakukera wewe tu?..Kama kweli anakera basi watu walio karibu yake ukute anawakera na ni lazima watamwambia tu..vinginevyo haramu kwako halali kwa mwingine...Mtu yeyote yule anao ndugu zake wa karibu na majirani zake..Haiwezekani eti mtu apake perfume mwezi mzima afu mkerwaji uwe peke yako tu?..Mimi nikipaka kitu au nikivaa hovyo wala sifiki mbali... kuanzia ndugu zangu home hadi makazini watakuwa washaniambia...Ndiyo maana Zion Daughter anakuambia tukubali tu kuvumiliana our differences..kwa sababu we'll never like or feel the same taste at a time....

hivi utakutana na mtu kwenye daladala uanze kumpa lecture ya perfume? wengine ni wakubwa wetu wa kazi. ndo maana kuna JF watu tunajifunza kimya kimya
 
Last edited by a moderator:
kwani ukiingia bar ukaagiza KILI hilo si ndilo chaguo lako? je utawalazimisha watu wote wanywe KILI? elewa sipingi matumizi ya perfume, nachosema isiwe too much mpaka kuhatarisha afya za wenzio.
 
habari wana JF

kuna jambo huwa linanitatiza. unakuta mtu anajipulizia perfume kali kupitiliza, akiingia ofisini watu mnaanza kupiga chafya. akiingia kwenye daladala, basi ukishuka tayari una mafua, akipita coridoni lazima aache alama siku nzima.

hivi kweli huu ni ustaarabu? hivi kila mtu akipuliza perfume hivyo kutakalika kweli?

watu tujirekebishe.

what is good for u may not be good for everyone.

Good day.......

wanaume ndio mna tabia hii huwa mnajipulizia airfresh au dawa za kuulia wadudu...
 
Unajua unajichanganya sana..sasa kama huyu unayemsema wewe kwenye daladala atakuwa anakukera wewe tu?..Kama kweli anakera basi watu walio karibu yake ukute anawakera na ni lazima watamwambia tu..vinginevyo haramu kwako halali kwa mwingine...Mtu yeyote yule anao ndugu zake wa karibu na majirani zake..Haiwezekani eti mtu apake perfume mwezi mzima afu mkerwaji uwe peke yako tu?..Mimi nikipaka kitu au nikivaa hovyo wala sifiki mbali... kuanzia ndugu zangu home hadi makazini watakuwa washaniambia...Ndiyo maana Zion Daughter anakuambia tukubali tu kuvumiliana our differences..kwa sababu we'll never like or feel the same taste at a time....

dont make assumptions kwamba lazima watu wamemwambia, always kumwambia mtu waziwazi huwa ni ngumu kwa wengi ndo maana tunaambizana huku. utashangaa mtu ananuka mdomo yeye hatakaa ajue kamwe but people around wanamuavoid bila yeye mwenyewe kujua.
mwingine anaambiwa lkn anachulia anaonewa gele...huo ni ulimbukeni
yes we will never be the same but dont do something to the detriment of others.
 
Zitakuwa za bei rahisi hizo... kuna ile imechorwa mwanamke amejitanda ushungi, boksi lake ni la purple ni balaa...house gril wangu alikuwa anatatumia, nilishindwa kuvumilia, ikabidi nimnunulie body spray atumie ili aachane na ile perfume.

Mi napenda perfume inayokaa muda mrefu, ila sio inayonukia mpaka kero ila nahisi watu wengine sense zao za ku-smell hazifanyi kazi vizuri, maana ananukia mpaka ananuka!!
 
uuuwiiii...umenichekeshaje?
wa kwangu alikuwa anatumia SIMLA. basi akipuliza nyumba nzima tunakohoa na mafua kibao, mpaka mwanangu mdogo akapata mafua yasiyoisha... nikamwambia ahakikishe anapuliza kidogo, nikaona amejirekebisha.
 
Sasa unachanganya habari.Kuna sheria ya kukataza kuvuta sigara public hasa kimataifa katika mambo ya haki za binadamu japo hapa bongo haifuatiliwi.Lakn perfum public sijawahi sikia...
Kwahiyo hata kujamba ushuzi kwenye Public unataka kutungiwe sheria ya kuban? mbona unaleta ligi isyokuwa na mpango?
 
Kwahiyo hata kujamba ushuzi kwenye Public unataka kutungiwe sheria ya kuban? mbona unaleta ligi isyokuwa na mpango?

Haya baba.Hata nikikesha naelekeza hapa it seems umeshaji tune kubishana..Lakn ukweli utabakia kuwa uleule....WANADAMU TUMETOFAUTIANA interests na ndio maana Mungu alituwekea uvimilivu..Hata hivo nimekupa kombe.Umeshinda
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom