PERAMIHO WANAMSUBIRI HECHE: Wasema walifurahia taarifa ya Mbowe

kuku dume

JF-Expert Member
Apr 22, 2012
414
62
Wana JF,
Ikumbukwe kwamba mimi ni mwanaharakati wa kujitegemea kutoka katika ambaye kwetu CCM ni chama cha upinzani kama ilivyo CUF Unguja na CCM Pemba.
Niko huku Ruvuma kueneza falsafa na itikadi za CHADEMA.

Nilikuwa katika maandamano ya 22/02 ambapo nilipigwa na askari kipigo cha mwizi lakini nasema bado MAPAMBANO YANAENDELEA.

Juzi pia nilihudhuria maandamano 'kamata mwizi' kudai umeme kwa Wanasongea.

Leo nimefunga safari kwenda Peramiho kusoma upepo huku nikiwa nimetupia gwanda langu kama utambulisho. Nikikutana na watu ni 'peoples power'; nikasema ya Arumeru yamefika Peramiho? Raia wa kule wameniambia kwamba wanasubiri sana ujio wa Heche.

Nimekuta watu wakisoma Tanzania Daima. Pia nimekuta bendera ya Chadema ikipepea maeneo mbalimbali.

Picha zinakuja.

Nawasilisha.

Kuku dume- kokolikooooo
 
kaka chadema sasa hivi ni kama coca cola baridi wakati wa jua kali na ccm ni sawa na chai muda huohuo.

PIGENI KAZI WAKATI NDIO HUU.
 
Yani una maana ni nguvu ya coca siyo??? ebu edit haraka hiyo hapo kwenye red plss!
 
Wana JF,
Ikumbukwe kwamba mimi ni mwanaharakati wa kujitegemea kutoka katika ambaye kwetu CCM ni chama cha upinzani kama ilivyo CUF Unguja na CCM Pemba.
Niko huku Ruvuma kueneza falsafa na itikadi za CHADEMA.

Nilikuwa katika maandamano ya 22/02 ambapo nilipigwa na askari kipigo cha mwizi lakini nasema bado MAPAMBANO YANAENDELEA.

Juzi pia nilihudhuria maandamano 'kamata mwizi' kudai umeme kwa Wanasongea.

Leo nimefunga safari kwenda Peramiho kusoma upepo huku nikiwa nimetupia gwanda langu kama utambulisho. Nikikutana na watu ni 'peoples power'; nikasema ya Arumeru yamefika Peramiho? Raia wa kule wameniambia kwamba wanasubiri sana ujio wa Heche.

Nimekuta watu wakisoma Tanzania Daima. Pia nimekuta bendera ya Chadema ikipepea maeneo mbalimbali.

Picha zinakuja.

Nawasilisha.

Kuku dume- kokolikooooo
Hiyo ni habari njema saana hayawi hayawi sasa yanaelekea kutimia, kina Rejao wako wapi Ritz na Nape wao ili waipate hii!!!!! VIVA PERAMIHO NA SONGI SONGI, VIVA UKOMBOZI WA NYONGE!!!!

Picha ntatupia mda wowote wakuu.

My take: Ritz, Rejeo musisite ku-download vile ntakavyo-upload maana UKOMBOZI ni kwetu sote. Au mtahama nchi kuikimbia Kisutu?
 
kamanda hongera kwa kazi nzuri sisi tupo nyuma yenu na sisi tunafa kampeni nyumba kwa nyumba mpaka kieleweke 2015
 
Jamani chonde chonde ndugu zangu....hii kasi inatisha na mimi naona kama vile 2015 ni kesho tu....!!! Jamni tusilale. Tusilalamike kwa nini viongozi wa chadema Taifa hawafiki katika maeneo yetu...tuangalie sisi tunafanya nini katika maeneo yetu....Tabora mmelala sana, au nyie mtabaki na magamba hadi lini? Dodoma na nyie kimya kabisa...jamani Ukombozi wa nchi hiii na kuondoka kwa ccm katika uongozi wa nchi hii itakuwa ni faida kwa wote....tupige kazi....hakuna kulala...BIG UP BROTHER...NIMEIPENDA SANA KAZI YAKO....KEEP IT UP....NEXT MONTH NAMALIZA COLLEGE NARUDI KABENDE KWA PINDA TUKAPAMBANE.....KITAELEWEKA TU....
 
Jamani Kombani nasikia anajitanua kuapa kuwatumikia watanzania huku akifanya madudu si kwa Watanzania na kwa wana Ulanga Magharibi. Morogoro tukitulia itakuwa Chadema 2015. Morogoro Mjini wanampenda Afande Sele( Selemani Msindi) na ametangaza kusimama kwa chadema, Ulanga( Haji Mponda alipita kwa magumashi ya wizi huku Kombani akiwa mbunge wa CCM maana hakuhitaji kura za wananchi kuwa Mbunge), Kilombero jamani sisemi ila wapo makamanda makini kama Arachuga, Mbeya nk: Mashahidi nyie.
 
Nafurahi sana kusikia watu wanajitolea kuelimisha wananchi,sehemu mbalimbali safi sana kila mwananchi awe katibu mwenezi wa CDM.
 
Jamani Kombani nasikia anajitanua kuapa kuwatumikia watanzania huku akifanya madudu si kwa Watanzania na kwa wana Ulanga Magharibi. Morogoro tukitulia itakuwa Chadema 2015. Morogoro Mjini wanampenda Afande Sele( Selemani Msindi) na ametangaza kusimama kwa chadema, Ulanga( Haji Mponda alipita kwa magumashi ya wizi huku Kombani akiwa mbunge wa CCM maana hakuhitaji kura za wananchi kuwa Mbunge), Kilombero jamani sisemi ila wapo makamanda makini kama Arachuga, Mbeya nk: Mashahidi nyie.

Kuweni serious hapo kwenye red msije mkafanya Bunge kama jukwaa la Kili Music award na sehemu ya kuvutia bangi. Tafuteni watu wenye busara na wanaoweza kujenga hoja siasa tuwaachie wanasiasa na wanamuziki wakaimbe muziki kuburudisha watu
 
Wasap!
Eh.....
 
dah mkuu swafi mnoo elimisha watu huko tuikatae ccm. M4C ni zaidi ya kimbunga jenister hakuna lolote analofanya huyo!
 
Back
Top Bottom